Makonda awe makini na mji wa Arusha

Makonda awe makini na mji wa Arusha

Huyo jamaa anatamani sana kuwa mbunge,
wakati yupo dar alitaka kuwa mbunge wa kigamboni akafeli,
leo yupo arusha anatamani awe mbunge wa uko, halafu makonda na gambo si walikua vipenzi vya mwenda zake hawa!
sasa mbona wanararuwana wenyewe kwa wenyewe?.
 
Arusha ni mji wa wafanyabiashara huwenda kuliko miji yote Tanzania

Arusha kila mtu ni mfanyabiashara

Arusha wahuni ni wengi saana

Juzi nipo na wazee na viongozi baadhi waandamizi wa CCM mkoa wa Arusha, wengi wanaonesha kukerwa sana na Anayoyafanya Makonda kwa Gambo.

Wazee hawamkubali kabisa kabisa, kwanza anaharibu biashara za watu kila siku anaziba barabara kwaajili ya maslahi yake kisiasa
Bado anaharibu taswira ya chama kwa kuropoka hovyo kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.

Lakini cha muhimu zaidi, tangu aende Arusha hakuna ch maana kilichobadilika Arusha tofauti na Mwanzo

Kiufupi, Makonda ni Mzigo

Kumbe arusha Arusha ni mji wa wafanyabiashara huwenda kuliko miji yote Tanzania!! Aise sometimes muweke na akiba ya maneno

Kuna Dar na Mwanza, sijui unayachukuliaje majiji haya!

Mbona kichwa cha habari ni cha kiume na kina maudhui mazito ila uzi wenyewe hauna hata hoja za msingi?

Mara Arusha ina wafanyabiashara wengi kuliko mkoa wowote,umejaribu kukaa Dar na mwanza?

Halafu mara useme wazee,hao wazee ni akina nani eneo la shughuli za kiserikali au katika maamuzi ya mwisho ya kitaifa?

Jambo lingine,ina maana makonda akikorofishana na Mrisho Gambo ndio amekorofishana na Arusha nzima kwamba hakuna watu wanaomkubali?
 
Ataje hata wazee wawili waandamizi wa CCM aliokutana nao Arusha.
Vimebadilika vingi barabara nyingi za mjini kati zilikuwa sio one road.Sasa zimekuwa za kupanda au kuteremka na hivyo kupunguza sana matatizo ya jam katika mitaa ya Bondeni,Pangani na Kaloleni.Na nyingi zimeanza kufanyiwa ukarabati.
Jiji limekuwa safi na upandaji wa miti milioni 1 na nusu unaendelea.
Hali ya usalama imeimarika sana ndani ya mwaka mmoja tokea Makonda awe Mkuu wa Mkoa.
Wafanyabiashara hawasumbuliwi na TRA kama ilivyokuwa ada.
 
Alipelekwa Arusha kwa kazi maalum mpaka itakapoisha!
Jeuri yake haiko bure!
Kama **** mtu anafikiri kuwa baada ya Magu kufariki ndiyo ulikuwa mwisho wa Makonda anajidanganya.
 
Arusha ni mji wa Wamasai na Wameru. Wachaga ni wakuja tu kama Wasukuma na makabila mengine hapo Arusha. Eti Wachaga wa Arusha!!
Sasa kwa taarifa yako wafanyabiashara wakubwa wengi wa hapo Arusha ni wachaga
 
wewe sio mkazi wa Arusha ni mbea flani hivi kutoka mikoa ya ukanda wa Magharibi.
Mkuu lile soko la Tengeru limejaa tope na vumbi nyie mnaishia kucheza sebene na nyama za bure.

Kumtawala mtu mjinga ni kazi rahisi mno😀😀
 
Arusha ni mji wa wafanyabiashara huwenda kuliko miji yote Tanzania

Arusha kila mtu ni mfanyabiashara

Arusha wahuni ni wengi saana

Juzi nipo na wazee na viongozi baadhi waandamizi wa CCM mkoa wa Arusha, wengi wanaonesha kukerwa sana na Anayoyafanya Makonda kwa Gambo.

Wazee hawamkubali kabisa kabisa, kwanza anaharibu biashara za watu kila siku anaziba barabara kwaajili ya maslahi yake kisiasa
Bado anaharibu taswira ya chama kwa kuropoka hovyo kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.

Lakini cha muhimu zaidi, tangu aende Arusha hakuna ch maana kilichobadilika Arusha tofauti na Mwanzo

Kiufupi, Makonda ni Mzigo
Halafu anataka kugombea Ubunge Arusha!
Huyu Bwana kama atafanya hivo ndo mwisho wake kisiasa hiyo migogoro itamrudia na atafanyiwa fitona na kupotezwa kama mwenzake Gambo anavomfanyia!
Sijui huwa haoni majimbo ya nyumbanikwao Mwanza!
 
Ataje hata wazee wawili waandamizi wa CCM aliokutana nao Arusha.
Vimebadilika vingi barabara nyingi za mjini kati zilikuwa sio one road.Sasa zimekuwa za kupanda au kuteremka na hivyo kupunguza sana matatizo ya jam katika mitaa ya Bondeni,Pangani na Kaloleni.Na nyingi zimeanza kufanyiwa ukarabati.
Jiji limekuwa safi na upandaji wa miti milioni 1 na nusu unaendelea.
Hali ya usalama imeimarika sana ndani ya mwaka mmoja tokea Makonda awe Mkuu wa Mkoa.
Wafanyabiashara hawasumbuliwi na TRA kama ilivyokuwa ada.
Wazee wa kwenye kilabu cha pombe aina ya chang'aa majina yao tatayafahamu kweli hata akiyataja hapa.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
Wewe ndio mzigo. Wafanyabiashara wa Arusha wanamuunga mkono sana Makonda ndio maana kila project anayofanya anapata michango ya wafanyabiashara. Pia wananchi na ccm wanamkubali sana kuliko huyo Gambo wako
Project kama ipi
 
Mbona kichwa cha habari ni cha kiume na kina maudhui mazito ila uzi wenyewe hauna hata hoja za msingi?

Mara Arusha ina wafanyabiashara wengi kuliko mkoa wowote,umejaribu kukaa Dar na mwanza?

Halafu mara useme wazee,hao wazee ni akina nani eneo la shughuli za kiserikali au katika maamuzi ya mwisho ya kitaifa?

Jambo lingine,ina maana makonda akikorofishana na Mrisho Gambo ndio amekorofishana na Arusha nzima kwamba hakuna watu wanaomkubali?
Tusimlaumu sana sio kosa lake, nafikiri unatambua kuwa huo mkoa ndio unaongoza kwa kuwa na vijana wa ajabu ajabu hivyo basi usishangae kuona hata hili bandiko halieleweki kwa sababu hapo zilizoandika ni bangi pamoja na vitoko.

Hii mivijana ya arusha akilini mwao huwa imejaza upumbavu mwingi sana na vilevi vya kila aina japo wao wanaita ujanja.
 
Sasa ushafuatilia kwa karibu maeneo wanakoishi hao Wamasai na Wameru? Maendeleo mengi ya majengo, na mandhari ya mji wa Arusha yameletwa na wageni!
Kama unabisha nenda Matejoo na Sokoni II.
Mimi sikuongerea utajiri bali wenyeji wa Arusha. Kama utajiri hata wamasai wapo hapo Arusha matajiri.
 
Wachaga wakiondoka Arusha kipindi cha mwisho wa mwaka mji unabakigi kama gofu

Labda ww unakaa arusha ya Karatu au ngarenanyuki
Acha uongo. Mimi nimekaa Arusha miaka mitano sikuona hiyo difference unayoisema wewe. Nilikuwa naishi hapo maeneo ya Uzunguni karibu na uwanja wa mgambo.
 
Hao watu ni wakabila na hawawezi kuacha ukabila.
Huyo mambo mwenyewe hapo Arusha hakushinda alitangazwa mshindi kimagumashi kwa nguvu ya jiwe .
Ni hisia zako tu. Kwani huyo unayesema alishinda kimagumashi ni kabila moja na jiwe?
 
Back
Top Bottom