Makonda awasilisha Muswada wa marekebisho ya sheria ya mirathi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
makonzi.jpeg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga muswada wa mapendekezo wa marekebisho ya sheria ya mirathi kwa ajili ya kufanyiwa maboresho na kuwasilishwa bungeni.

Muswada huo umewasilishwa jijini Dodoma na kuzitaja sheria kandamizi ambazo angependa zifanyiwe marekebisho kuwa ni pamoja na Sheria ya kiserikali ya mirathi, Sheria ya Mirathi ya Kimila pamoja na Sheria ya Mirathi ya Kidini kwa madai ya kuwa zimepitwa na wakati na zimekuwa zikileta mateso kwa wajane.

Makonda amekuwa akipigia kelele yafanyiwe maboresho pamoja na kipengele cha kumpa uhalali mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala mali kuhamishwa, pamoja na usawa wa watoto.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa alichokifanya Makonda ni ushujaa wa hali ya juu na ameweka historia ya jambo ambalo halijawahi kufanyika na kuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni.
 
Wataalamu wa Sheria naomba kuelimishwa taratibu za kuwakilisha miswaada mimi ninao wa kwangu binafsi nimeuandaa wa marekebisho ya Sheria ya kutomlazimisha mtoto kwenda shule kama hataki au mzazi hataki naweza upeleka huo mswada wangu binafsi kwa waziri wa Sheria ukafanyiwe Kazi?
 
Wataalamu wa Sheria naomba kuelimishwa taratibu za kuwakilisha miswaada mimi ninao wa kwangu binafsi nimeuandaa wa marekebisha ya Sheria ya kutomlazimisha mtoto kwenda shule kama hataki au mzazi hataki naweza upeleka huo mswada wangu binafsi kwa waziri wa Sheria ukafanyiwe Kazi?
Hahahahah. Mkuu shule ipi? Shule ya msingi, secondary au chuo?
 
Jaman hivi makonda anaweza kufanya marekebisho sheria za mirathi za kiislamu?

Je! Sheria za kimila za uchagani anaweza kuziingilia? Mm nafkir angestic kwenye sheria za mirathi za kiserikal kama anaona zina mapungufu..

Istoshe sheria kandamizi kwenye mirathi ni Ile ya mama kutokuwa msmamizi wa mali na hii naona ni sawa kwasabb mjane below 60 anaweza kuolewa tena. Je uhakika wa mali hizo kuwa salama huko aendako itakuwaje?
 
makonzi.jpeg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga muswada wa mapendekezo wa marekebisho ya sheria ya mirathi kwa ajili ya kufanyiwa maboresho na kuwasilishwa bungeni.

Muswada huo umewasilishwa jijini Dodoma na kuzitaja sheria kandamizi ambazo angependa zifanyiwe marekebisho kuwa ni pamoja na Sheria ya kiserikali ya mirathi, Sheria ya Mirathi ya Kimila pamoja na Sheria ya Mirathi ya Kidini kwa madai ya kuwa zimepitwa na wakati na zimekuwa zikileta mateso kwa wajane.

Makonda amekuwa akipigia kelele yafanyiwe maboresho pamoja na kipengele cha kumpa uhalali mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala mali kuhamishwa, pamoja na usawa wa watoto.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa alichokifanya Makonda ni ushujaa wa hali ya juu na ameweka historia ya jambo ambalo halijawahi kufanyika na kuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni.

Sijaelewa vizuri.
Kumbu kila mtu anaruhusiwa kupeleka muswada bengeni bila ya yeye kuwa mbunge?

Naomba utaratibu ukoje maana sasa mbuge litajaa miswada ya kila mtu anayetaka yafanyike maraekebisho
 
kinacholengwa hapo ni kumsaidia mjane wa Mzee Machache ili aweze kurithi mali zote za Mzee hata zile ambazo Mzee alichuma na Mama Mercy, jamaa anaanza Movie mapema, ila Mungu huwa hachezewi na Haki siku zote huchelewa tu na sio kupotea. inawezekana amehaidiwa asilimia fulani akilifanikisha hili.
 
Jaman hivi makonda anaweza kufanya marekebisho sheria za mirathi za kiislamu?

Je! Sheria za kimila za uchagani anaweza kuziingilia? Mm nafkir angestic kwenye sheria za mirathi za kiserikal kama anaona zina mapungufu..

Istoshe sheria kandamizi kwenye mirathi ni Ile ya mama kutokuwa msmamizi wa mali na hii naona ni sawa kwasabb mjane below 60 anaweza kuolewa tena. Je uhakika wa mali hizo kuwa salama huko aendako itakuwaje?
kabrasha hilo haliendi kokote hapo kwa mahiga ndio mwisho!
 
Mi naona yuko sahihi kabisa kama hutaki mwanamke uliye nae aje kurithi mali zako tafadhari usimuoe wala kuzaa nae
 
Huo mswaada unawalinda vipi wanaume dhidi ya wale wanaoitwa wapelestina kuwarestisha in peace waume zao ili wamiliki mali, haoni ndugu wa mwanaume wataathirika kama hawatakuwa na say yoyote kwenye mali za ndugu yao hasa kama kuna hila zimefanyika, hilo swala liko so complicated asikurupuke
 
Back
Top Bottom