Makonda atoa siku 10 kwa Wilaya ya Kigamboni kuhakikisha hospitali inaanza kufanya kazi

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,712
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa siku kumi kwa uongozi wa Manispaa ya Kigamboni kuhakikisha Hospital hiyo inaanza kutoa huduma kwa wananchi ifikapo June Mosi baada ya Majengo yote ya Hospital hiyo kukamilika.

RC Makonda ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo ambapo pia amekabidhi Magodoro 175, Mashuka 1,294 na Ndoo na kueleza kuwa ifikapo Jumanne ya wiki ijayo atakabidhi tena Mashine mbili za Ultrasound zenye thamani ya Milioni 70 na Vitanda 100 ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa.

Aidha RC Makonda amemuelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuhakikisha anapeleka Watumishi 40 kwenye hospital hiyo kwaajili ya kutoa huduma ili kutimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Tano la kupunguza kero za Afya kwa Wananchi.

Akiwa katika Ukaguzi wa Ujenzi wa Barabara na Round about inayounganisha barabara za Kuelekea Feri na Kibada Kutokea Daraja la Mwalimu Nyerere
RC Makonda amewaelekeza TARURA na TANROAD kuhakikisha ujenzi wa Barabara na Mzunguko wa Magari vinakamilika na kukabidhiwa kabla ya Mwezi September Mwaka huu.

Pamoja na hayo RC Makonda amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watendaji wa Jiji hilo kuhakikisha maelekezo na Ahadi zote zinazotolewa na Rais Magufuli vinatekelezwa kwa Wakati pasipo kushurutishwa huku akiwataka wakandarasi wote kuhakikisha miradi yao inakamilika kwa wakati.
 
May 22, 2020
53
125
Kama imekamilika si akae atulie watu wajipange hospitali ifunguliwe? Lazima atoke kujifanya mkali utadhani watu wamelala hawataki kufungua hospitali?

Bashite ni tako huyu jamaa, kufuli aliwatoa wapi vilaza hawa?
 

Riadha jr

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
533
500
Yericko Nyerere upo wapi bwashee?
mzee wa ku copy na ku pasty A.k.A muuza vitabu niliwai kumshauri ya kwamba chama chake ..kili anza na mungu na kikasema kitamaliza na mungu kama ilivo kanuni au msemo wa chama icho ....

sasa haya maswala ya kupiga porojo za kutukana imani za watu mchana kweupe misingi hiyo ameipata wapi? je ujasusi wake ndo unamfanya awe na kiburi cha kujiona wa muhmu kuliko imani za watu walio wapiga kura wa chama chake...hana nafasi yoyote atakayo gombania akaipata si kwa porojo zile..over

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
17,129
2,000
Ndo hii hospital imefanya Ndugulile atemeshwe unaibu waziri. Maana mukulu alisema Naibu kashindwa kupeleka vifaa hospitali ya jimbo lake. Makonda umemchongea Ndugulile. Siasa bwana ni kuharibiana tu.
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
5,468
2,000
Ndo hii hospital imefanya Ndugulile atemeshwe unaibu waziri. Maana mukulu alisema Naibu kashindwa kupeleka vifaa hospitali ya jimbo lake. Makonda umemchongea Ndugulile. Siasa bwana ni kuharibiana tu.
Mkuu kamchongeaje wakati tayari alishatumbuka?

Sema Makonda anakazia hotuba ya Jpm ya 'solidarity...... home.'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom