Makonda atoa masharti kupokea ndege ya Serikali

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,940
Wakati kesho Ijumaa Januari 11, 2019 Serikali ya Tanzania ikitarajia kupokea ndege yake ya Airbus A200-300, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanaopaswa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mapokezi hayo wawe ni aina ya watu wanaotekeleza ahadi zao.

Akizungumza leo Alhamisi Januari 10, 2019 na waandishi wa habari, Makonda amesema ujio wa ndege hiyo umetokana na ahadi za Rais John Magufuli za kulifufua shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

“Pamoja na changamoto zote hizo za kupingwa, lakini mwanaume huyu (Magufuli) amekuwa shupavu kapambana na kesho inatua Airbus ya pili ikiwa ni kati ya zile ndege mbili kubwa alizoziagiza kati ya ndege saba zinazopaswa kuletwa kwa ajili ya shirika letu la ndege,” amesema.

“Niwaombe tu kama wewe ni mwananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na ulishawahi kutoa ahadi ukatekeleza, tukutane kesho Uwanja wa Ndege na wale ambao hawajawahi kutekeleza ahadi zao wasije.”

“Kwa watakaobaki majumbani tutakuwa tumepata jibu kwamba ni wale ambao wametoa ahadi lakini hawajawahi kutekeleza.”

Chanzo: Mwananchi

49658208_10157036349729339_7770187139496542208_n.jpg
 
By Nasra Abdallah, Mwananchi nabdalla@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Wakati kesho Ijumaa Januari 11, 2019 Serikali ya Tanzania ikitarajia kupokea ndege yake ya Airbus A200-300, mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanaopaswa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mapokezi hayo wawe ni aina ya watu wanaotekeleza ahadi zao.

Akizungumza leo Alhamisi Januari 10, 2019 na waandishi wa habari, Makonda amesema ujio wa ndege hiyo umetokana na ahadi za Rais John Magufuli za kulifufua shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

“Pamoja na changamoto zote hizo za kupingwa, lakini mwanaume huyu (Magufuli) amekuwa shupavu kapambana na kesho inatua Airbus ya pili ikiwa ni kati ya zile ndege mbili kubwa alizoziagiza kati ya ndege saba zinazopaswa kuletwa kwa ajili ya shirika letu la ndege,” amesema.

“Niwaombe tu kama wewe ni mwananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na ulishawahi kutoa ahadi ukatekeleza, tukutane kesho Uwanja wa Ndege na wale ambao hawajawahi kutekeleza ahadi zao wasije.”

“Kwa watakaobaki majumbani tutakuwa tumepata jibu kwamba ni wale ambao wametoa ahadi lakini hawajawahi kutekeleza.”

Source: Mwananchi
Maelezo Kama hayo hata kiranja was darasa la pili hawezi kuongea mbele ya wanafunzi wenzake

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
 
Wenye vyeti vya ku foji jee?RC dar hajawai fanikia kwa jambo hata moja kama ana bisha aseme ni lipi.
Pia ni ushamba kwenda kila siku uwanjani kupokea ndege.QATAR Emirates vi nchi vidogo huwa wananunua ndege 60 za aina ya AirBus 330 kwa wakati mmoja na hawakeshi airport kuzipokea.
Lizaboni
Mkuu, Kila familia/Kabila/Ukoo na desturi zake. Katiba ya JMT haisemi tuangalie QATAR n.k wanafanyaje ama wanaishije.

Mfano: sisi Tanzania ni REPUBLIC GOVT bali Qatar ni MONARCHY GOVT. na hatujawahi sisi fikiria tuwe Monarchy "why??"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vituko uswahilini hahaha Tanzania kuna vituko ikija ndege viongozi kibao,kuweka jiwe maskani watamwalika rais wao. Tunanunua ndege wakati mashuleni wanao feli kibao, Bashite mmoja wao vyeti feki ajira hupeana wao kwa wao. Madafanta

Ndukiiiii🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
ivi hii ndege mbona kila niki jaribu kui track haionekani ktk flight radar 24, flight aware, flight stat na site zingine embu kama kuna mtu aliye jaribu kui track atume details ili tujue so far wamefika wapi hawa ndugu zetu waliokwenda kuichukua iki chombo,
 
Back
Top Bottom