Makonda atangaza siku za tano ukaguzi bure wa magari Dar

Eng Kamwele waziri wa miundombinu ameshasema hadharani magari ya serikali yatatengezewa Temess tu, ina maana huyu Makonda yupo kwenye serikali ipi asilijuwe hili?

Huu ujanja ujanja wataacha lini? Hivi ukikaguwa gari ukagunduwa tatizo si lazima ununuwe spare ubadilishe umalize tatizo? Sasa hapo si tunarudi kulekule kwenye upigaji? Watu kweli ni manunda.
 
Tatizo siyo service, shida ipo kwenye barabara mbovu na hiyo mituta mliyojaza huko barabarani. unakuta barabara, mfano ya makongo imejaa mashimo utafikiri mgodi wa dhahabu
 
Makonda is a very creative person. Anaona mbali sana. Ubunifu huu sio tu utawapunguzia gharama wamiliki wa vyombo hivyo bali pia kupunguza ajali. Ajali zinazotokea, zaidi ya 85% hutokea kutokana na ubovu wa vyombo (one can conduct a research on this). Tumpe ushirikiano ili kupunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la ajali.
Umetumia kiungo gani kufikiri? Unadhani gari ukiifanyia checkup tu inapona tatizo?
Pia kutakuwa na kudanganywa matatizo kwwnye magari ili kupigwa hela ukienda kichwakichwa. Utasikia Ignition key imetanuka na inavuja inatakiwa 300k.
 
Hivi anaposema Bure
Kama mtu anataka abadilishiwe engen oil, hydraulic oil etc atapewa Bure pia
Mimi naona kama Kuna mtu anatafutiwa kik tu hapo kwenye garage yake

Ova
Ujinga ujinga tu, likionekana tatizo unaingia mfukoni kuliko kawaida.
 
Kwani kikawaida kufanya checkup ya gari kunaghalimu kiasi gani?
Mara nyingi ukifanya check up lazima ujipange Kwanza na pesa ya kununua spare pia inategemea na mafundi wenyewe kuna wengine watakuambia vitu vya kubadilisha karibia engine yote na wengine watakuambia vitu vichache Tu na ukibadilisha unafanya Safari mwanzo mwisho bila shida yeyote
 
Mara nyingi ukifanya check up lazima ujipange Kwanza na pesa ya kununua spare pia inategemea na mafundi wenyewe kuna wengine watakuambia vitu vya kubadilisha karibia engine yote na wengine watakuambia vitu vichache Tu na ukibadilisha unafanya Safari mwanzo mwisho bila shida yeyote
Kwa hiyo hko utafanyiwa Bure hadi kuwekewa spea bure

Ova
 
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza siku tano, kuanzia Desemba 10 hadi 15, 2019 kwa wenye magari kufanya ukaguzi ili wasafiri salama kwenda mikoani kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka.


Makonda ametangaza ukaguzi huo leo Alhamisi Desemba 5, 2019 baada ya kukutana na wamiliki na mafundi gereji ambao walikubali kufanya kazi hiyo bure ikiwa ni ofa ya mwisho wa mwaka.

Amesema ajali nyingi za barabarani zinatokana na wamiliki wa magari kutojenga tabia ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini kasoro.

"Kwa hiyo tutatangaza gereji zilizo tayari kwa kazi hii pelekeni magari yenu ili safari iwe salama," amesema Makonda.

Awali, baadhi ya wamiliki na mafundi wa gereji walisema wapo tayari kufanya kazi hiyo kwa sababu watu wengi watajua changamoto za magari yao kabla ya kuanza safari.

"Tutawashauri kulingana na changamoto tutakazokutana nazo," amesema Elgius Mndale, fundi gereji kutoka wilayani Temeke.


Mkurugenzi wa Evolution Investment & General Supplies Ltd, Anthony Mganja amesema pamoja na kufanya ukaguzi huo, wapo tayari kutengeneza magari ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi cha miezi sita.

"Tunaunga mkono kazi za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo, kwa hiyo pamoja na ukarabati wa magari ya Serikali tupo tayari kusaidia," amesema Mganja.


Chanzo: Mwananchi

Eneo gani nipeleke gari langu likakaguliwe? Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye nguvu sana. Tujifunze unyenyekevu
 
Back
Top Bottom