Makonda atangaza siku za tano ukaguzi bure wa magari Dar

Nashangazwa sana na huu utendaji wa RC Makonda. Huwa anatabia ya kudandia mambo na kuyafanya agenda wakati hayana tija kwa wananchi na hata hao anaowafanyia hawana shida nayo.

Sasa kuzungumza na watu wa garage eti kuwafanyia checking magari ya watu wa Dar bure inatija gani kwa maendeleo? Hivi mtu anunue gari lake lakini kufanya service hawezi mpaka apewe ofa?

Na hao wenye garage mnadhani wamekubali kufanya bure kwa mapenzi yao au ni jambo LA kushinikizwa?

Mwenye akili timamu huwezi kupeleka gari lako kuchekiwa bure kwa mtu anayefanya hivyo bila ridhaa yake Bali shinikizo.
Wale washauri wa serikalini wamwambie Makonda Dar ni kubwa sana, kuwa na kiongozi wa fikra za aina yake za kuwaza kutangazwa tuu wakati mambo ya msingi hayashughulikiwi ni upotevu wa muda
 
Kuna sehemu niliwahi soma kuwa kati ya mwanamke na mwanamume ufaham na ukuaji wa akili huwa unatofautiana!hata ukiangalia tu malezi ya watoto wakike na wakiume unaona kns me waachelewa kucope na mazingira!
Huo ni utoto...bora uishi na mtu broke kuliko kuishi na jitu lenye utoto toto!!.makonda ana utoto mwingi sana!lols!
 
Alitaka tu aongolewe, kama hivi wewe ulivyo mwanzishia uzi, UMEMPAISHA BILA KUTARAJIA
Kama anaona ujinga wake kuwekwa hadharani ni kupaishwa basi tatizo alilo nalo yeye au wenye mawazo kama yake ni kubwa zaidi.
Dar kuna changamoto kibao, RC kupoteza muda kwenye mambo kama hayo na kuyapa kipaumbele ni tatizo kubwa
 
Serikali imesema Kuna upungufu wa madawati, wanafunzi waliofaulu mwaka huu kwenda kidato cha kwanza mwakani watakosa nafasi yeye yupo kwenye mambo ya kijinga tu, Sasa anapromote magereji ya watu binafsi, hajui vipaumbele
 
Mkuu hapo hakuna huduma ya bure kihivyo.
Ni sawa anae kuambia kucheck macho ni bure kisha anakuuzia miwani kwa 70,000/- au laki 1.
Hapo kuchekiwa bure ila kutengenezewa na vifaa unapigwa parefu tu.

Hapo kawasaidia mafundi kufanya biashara yao kijanja.
Sema mkuu wa mkoa ni mtu mwenye majukumu makubwa sana ya kuhudumia kada zote na sio kuelekeza nguvu zake kwa kundi dogo la mafundi gari.
Huo ni uongozi mbaya.
 
Mtego wa kunasa magari ya wizi yapo magari mengi sana yamefutwa chases namba zikabandikwa zingine hivyo kuna kitu kinatafutwa hapo

Nashangazwa sana na huu utendaji wa RC Makonda. Huwa anatabia ya kudandia mambo na kuyafanya agenda wakati hayana tija kwa wananchi na hata hao anaowafanyia hawana shida nayo.
Sasa kuzungumza na watu wa garage eti kuwafanyia checking magari ya watu wa Dar bure inatija gani kwa maendeleo? Hivi mtu anunue gari lake lakini kufanya service hawezi mpaka apewe ofa?
Na hao wenye garage mnadhani wamekubali kufanya bure kwa mapenzi yao au ni jambo LA kushinikizwa?
Mwenye akili timamu huwezi kupeleka gari lako kuchekiwa bure kwa mtu anayefanya hivyo bila ridhaa yake Bali shinikizo.
Wale washauri wa serikalini wamwambie Makonda Dar ni kubwa sana, kuwa na kiongozi wa fikra za aina yake za kuwaza kutangazwa tuu wakati mambo ya msingi hayashughulikiwi ni upotevu wa muda
 
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza siku tano, kuanzia Desemba 10 hadi 15, 2019 kwa wenye magari kufanya ukaguzi ili wasafiri salama kwenda mikoani kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Makonda ametangaza ukaguzi huo leo Alhamisi Desemba 5, 2019 baada ya kukutana na wamiliki na mafundi gereji ambao walikubali kufanya kazi hiyo bure ikiwa ni ofa ya mwisho wa mwaka.

Amesema ajali nyingi za barabarani zinatokana na wamiliki wa magari kutojenga tabia ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini kasoro.

"Kwa hiyo tutatangaza gereji zilizo tayari kwa kazi hii pelekeni magari yenu ili safari iwe salama," amesema Makonda.

Awali, baadhi ya wamiliki na mafundi wa gereji walisema wapo tayari kufanya kazi hiyo kwa sababu watu wengi watajua changamoto za magari yao kabla ya kuanza safari.

"Tutawashauri kulingana na changamoto tutakazokutana nazo," amesema Elgius Mndale, fundi gereji kutoka wilayani Temeke.

Mkurugenzi wa Evolution Investment & General Supplies Ltd, Anthony Mganja amesema pamoja na kufanya ukaguzi huo, wapo tayari kutengeneza magari ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi cha miezi sita.

"Tunaunga mkono kazi za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo, kwa hiyo pamoja na ukarabati wa magari ya Serikali tupo tayari kusaidia," amesema Mganja.

Chanzo: Mwananchi

Makonda is a very creative person. Anaona mbali sana. Ubunifu huu sio tu utawapunguzia gharama wamiliki wa vyombo hivyo bali pia kupunguza ajali. Ajali zinazotokea, zaidi ya 85% hutokea kutokana na ubovu wa vyombo (one can conduct a research on this). Tumpe ushirikiano ili kupunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la ajali.
 
Kuna sehemu niliwahi soma kuwa kati ya mwanamke na mwanamume ufaham na ukuaji wa akili huwa unatofautiana!hata ukiangalia tu malezi ya watoto wakike na wakiume unaona kns me waachelewa kucope na mazingira!
Huo ni utoto...bora uishi na mtu broke kuliko kuishi na jitu lenye utoto toto!!.makonda ana utoto mwingi sana!lols!
Hivi anaposema Bure
Kama mtu anataka abadilishiwe engen oil, hydraulic oil etc atapewa Bure pia
Mimi naona kama Kuna mtu anatafutiwa kik tu hapo kwenye garage yake

Ova
 
Kuna sehemu niliwahi soma kuwa kati ya mwanamke na mwanamume ufaham na ukuaji wa akili huwa unatofautiana!hata ukiangalia tu malezi ya watoto wakike na wakiume unaona kns me waachelewa kucope na mazingira!
Huo ni utoto...bora uishi na mtu broke kuliko kuishi na jitu lenye utoto toto!!.makonda ana utoto mwingi sana!lols!
real bora uishi na mtu broke
 
Back
Top Bottom