Malaika Gabrieli
JF-Expert Member
- May 28, 2020
- 3,280
- 6,093
Makonda ni comedy sana.
Makonda bhana ...Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Christian Makonda amesema kuelekea mwaka 2030 wapo wanasiasa wengi wanaotaka kutumia shida za wananchi kupata uongozi Mkuu wa Nchi, akiahidi kushughulikia wale wote wanaopanga njama za kuharibu na kudhoofisha jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ili kufanikisha ndoto zao za Urais.
Makonda amebainisha hayo leo Jumatano Machi 25, 2026 mkoani Arusha mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa elimu kwa umma nchini, akiwaonya pia wateule wa Rais ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kupanga safu za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, akiahidi kutomsaliti Rais Samia Suluhu.
"Mimi tukiwa kwenye vita situmi mtu, nakuja mwenyewe kukushughulikia na nina bahati pia ya kusema na Mungu, watu wote hawa wanaojipanga na Urais hawawezi hata kushika Urais mwaka 2030, mtaniona hapa na hili wekeni kwenye kumbukumbu, hawatapata kwani Watanzania si wasahaulifu na pia tutaweka rekodi ulifanya nini awali na ukweli ni kuwa huwezi kuwa malaika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi. Shetani ni shetani tu hata kama akizeeka”, amekaririwa Makonda.
Akibainisha kukerwa na kuona baadhi ya wanasiasa wakiwa kwenye mipango kuelekea 2030 pamoja na kutaja uzoefu wake katika siasa, Makonda ameeleza pia kushangazwa na maigizo ya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiigiza kusikiliza kero za wananchi, kuikosoa serikali pamoja na kutaka kujiweka kando na serikali, akimpongeza Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kusimama imara na Rais Samia Suluhu Hassan, kumtaka kutokatishwa tamaa na kuahidi kusimama na Rais Samia dhidi ya wote wanaompinga.
Duh...!, japo namkubali sana bosi wangu huyu, kwasababu mimi ni sehemu wa tuliompendekeza huyu awe RC DSM, tumelitoa pendekezi hili leo usiku wa saa 2:00 Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Chuma kikaona hiyo post ya JF, ilinyanyuliwa simu moja tuu!, usiku huo huo faili mezani!, ilipita siku moja tuu!, kesho yake ni tangazo kwenye bomba!.
Huwa mnamaanisha nini mkisema suprise??Hapa anawalenga kina Mwigulu na VP au? Maana hao ndio wako moto na mbio za Urais.
By the way Urais wa 2030 utakuwa surprise lakini pia bwana Makonda aweke Akiba ya maneno.
Mwendazake angekuwa anakubalika kihivyo asingetumia dola kuumaliza upinzani na kuharibu uchaguzi wa 2020.Common people wanamkubali kama Mwendazake
mbona mama hajajitanda hapo?Baada ya kumaliza kuwashughulikia wanaSiasawa wa upinzani, sasa wamegeukiana na kuanza kuchapana wenyewe makonde ya nguvu kuhusu nani kuwa rais 2030 tena mapema sana hata ya Oct 29 hayajapoa wala kutolewa report yake.Acha wachapane maana washaanza kulalamika vifo vya ghafla vya wanasiasa wao!!
Amekuwaje waziri?Hivi Bashite anaanzaje kuwa rais?
Ccm kwa namna moja au ingine inakosea sana wananchi!Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Christian Makonda amesema kuelekea mwaka 2030 wapo wanasiasa wengi wanaotaka kutumia shida za wananchi kupata uongozi Mkuu wa Nchi, akiahidi kushughulikia wale wote wanaopanga njama za kuharibu na kudhoofisha jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ili kufanikisha ndoto zao za Urais.
Makonda amebainisha hayo leo Jumatano Machi 25, 2026 mkoani Arusha mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa elimu kwa umma nchini, akiwaonya pia wateule wa Rais ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kupanga safu za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, akiahidi kutomsaliti Rais Samia Suluhu.
"Mimi tukiwa kwenye vita situmi mtu, nakuja mwenyewe kukushughulikia na nina bahati pia ya kusema na Mungu, watu wote hawa wanaojipanga na Urais hawawezi hata kushika Urais mwaka 2030, mtaniona hapa na hili wekeni kwenye kumbukumbu, hawatapata kwani Watanzania si wasahaulifu na pia tutaweka rekodi ulifanya nini awali na ukweli ni kuwa huwezi kuwa malaika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi. Shetani ni shetani tu hata kama akizeeka”, amekaririwa Makonda.
Akibainisha kukerwa na kuona baadhi ya wanasiasa wakiwa kwenye mipango kuelekea 2030 pamoja na kutaja uzoefu wake katika siasa, Makonda ameeleza pia kushangazwa na maigizo ya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiigiza kusikiliza kero za wananchi, kuikosoa serikali pamoja na kutaka kujiweka kando na serikali, akimpongeza Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kusimama imara na Rais Samia Suluhu Hassan, kumtaka kutokatishwa tamaa na kuahidi kusimama na Rais Samia dhidi ya wote wanaompinga.
Sijajua mkuu😀mbona mama hajajitanda hapo?