Makonda angekuwa bado ni RC wa Dar basi CCM ingebeba Majimbo yote jijini

Kadoda nguku

JF-Expert Member
Apr 22, 2019
332
475
Kitendo cha kumuondoa Paul Makonda Dar es Salaam imekuwa kama afueni kwa wapinzani Jijini Dar es Salaam.

Hakika kama Makonda angebakia, wapinzani wasingepata Jimbo hata moja ila kwa sasa naona majimbo yote ya Dar yanaenda tena upinzani

Sijui CCM hawakulifikiria hilo?

Makonda siasa za Jiji la Dar es Salaam anaziweza sana.
 
Acha kumpa Makonda hasizositahili, Makonda ameshindwa kushinda yeye mwenyewe uchaguzi wa ndani (wana CCM wachache wakiwa wapiga kura) tens katika jumbo moja tu ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, alafu unaeleza vitu vya ajabu ajabu humu!.
 
Ndio maana nimesema Dar haihitaji Akili, anahitaji ubabe kwa maana ya kutuma vyombo vyote
Sasa huko si nikuhatarisha amani ndugu, hivi unazani huu utulivu na uvumilivu ni wa milele? JK mwaka 2010 alizidiwa kura na Dr Slaa kwenye vituo vyote nyeti (Makazi ya viongozi, na watu wazito) mfano Mbezi Beach, Masaki, Osterbay, Lugalo jeshini etc.

Kuna jamaa yangu nilisoma nae Ikizu High school (Mara) R.I.P alikuwa TISS alinitonya jinsi hiyo hali ilivyompa simanzi JK. Kwamba familia za viongozi kule Masaki na Osterbay zimeenda kumkataa kwenye sanduku la kura, hadi familia za manajeshi.
 
Nyie wafuasi wa makonda acheni kutusumbua kama angekuwa na uwezo huo asingeshindwa kura za maoni kwa kifupi mirija yenu imeshakatwa
 
Back
Top Bottom