McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewataka Watanzania kupuuza watu wanaohamasisha uvunjifu wa amani nchini, huku akisisitiza umuhimu wa kumuunga mkono Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makonda ametoa kauli hiyo jijini Mwanza alipokuwa akitembelea Soko Kuu, ambapo alieleza kuwa CCM imeweka misingi bora na wezeshi kwa maendeleo ya wananchi.
Aidha, Makonda amewataka Watanzania kuacha tabia ya kubaguana kwa misingi ya kidini, akisisitiza kuwa mshikamano na umoja wa kitaifa ni nguzo muhimu kwa ustawi wa nchi