Makocha wa Kigeni na Lugha ya Kiswahili

Makocha wa Kigeni na Lugha ya Kiswahili

IL Capitano

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2014
Posts
216
Reaction score
123
Nimekua mfuatiliaji wa mahojiano ya makocha kabla na baada ya mechi katika ligi mbalimbali hususan ligi za ulaya nilichogundua wenzetu kama kocha katoka nje ya nchi hiyo inachukua muda kidogo kujifunza lugha ya nchi anayofundisha soka mfano ni makocha Pep Guardiola na Carlo na mahojiano atakayofanya yatafanyika kwa lugha ya nchi hiyo.

Cha ajabu katika nchi yetu sijaona kitu kama hicho tena wengine wamekaa muda mrefu ku mbuka Maximo na mh. Phiri hali hii imenifanya nijiulize:

1.Hakuna kanuni ya kuwabana makocha wa kigeni kujifunza lugha yetu adhimu ya kiswahili?

2.Lugha yetu bado ipo chini ya kiwango kwa maana ya kukosa maneno ya kutosha?

3.Dharau kutoka kwa makocha kutotaka kujifunza lugha?

Wadau tuelimishane kwa hili
 
Utajifunzaje wakati kesho unafukuzwa??????
 
Mbona maximo alikaa miaka zaid ya miaka 3 lakini ameondoka na maneno ya kuokoteza
 
Kuna walakini na vipaumbele vyetu, hadi leo sisi wenyewe tunadhani kuwa kusema Kiswahili ni dalili za ushamba, kutoelewa na sio lugha ya mawasiliano kimataifa.

Bila kuondosha mtazamo huu bado itakuwa kazi bure! Si makocha pekee, hata wachezaji na wafanyakazi wa kada zingine wanaokuja nchini huwa hawalazimishwi kujifunza lugha!
 
Umegusia
kitu cha muhim sana sijui tuna mapungufu gani sisi!ilitakiwa kuwe na utaratibu wa lazima kujifunza lugha kuna faida walau mbil hv moja kuongeza ajira kwa wafundishaj wa lugha na pili walau kutanua lugha kwa nchi zilizo mbali.
 
Jambo la lugha ni pana kuliko unavyoliona kaka, lugha ni chombo cha kuunganisha, chombo ch ufahari na chombo cha kuteka mawazo. Mwanafasihi mmoja alipata kusema tuache kufikiri kwa lugha za kigeni... Fikiria mwanafunzi anakosa maarifa ya msingi kwa kuwa tu amelazimika kujifunza kwa lugha ngeni, ngumu na isofanana na lugha yake mama!

Tukiushinda ukoloni wa utamaduni tutapiga hatua pakubwa sana!
 
For sure..mm nadhan tunakosa utashi katika hilo..emancipation from mental slavery ni kazi na hatutaweza kabisa
 
Back
Top Bottom