Makinika na mijusi wa ndani ya nyumba!

UFUNUO 21:8

Imethibitisha juu ya uwepo wa wachawi.

Ikiwa huamini kuwa wachawi wapo, Muulize shangazi Yako Kwa HEKIMA na upole, atakuthibitishia.

Uliza vizuri uambiwe kitovu chako kilipokatwa kilipelekwa wapi.
Mkuu Rabbon

Shangaazi yake ni mchawi mpaka amthibitishie?
 
Nimeanza kukaa na paka nikiwa na miaka6 akawa analala juu ya neti yangu. Alikufa kwa kuumwa, yule paka alikuwa hawezi kuamka mpaka anione nimeamka kwanza, wonderful enough nakumbuka napelekwa shule ananisindikiza mpaka getini halafu anarudi.

Katika viumbe ambavyo vina upendo wa ajabu ni MBWA. Anaweza kukupenda zaidi ya anavyojipenda. Mzee wangu alileta mbwa wale wa urembo aliwatoa kwa rafiki yake. Ilifika extent mpaka mtu akiwa ananifokea ana react vbaya mno.

Hizo stori sijawahi kuziona kwangu na nimeanza kukaa na hivyo viumbe nikiwa mdogo.
Ndugu huyu amewakosea sana mbwa na paka bora

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Elezea wewe Kwa angle unayoijua,

Hapa jamvini, tupo kupeana knowledge.

Hebu tiririka.
Hio heading ya thread yako ulioiweka ingetosha kufikisha ujumbe.

Ulipokuja kuharibu ni kuvipa hatia viumbe vya Mungu.

Zingatia hii misemo .

1.Mchawi mtu paka katumwa
2. Bunduki haiui watu, watu wanaua watu


Kisu kinaua lakini haimaanishi tusikitumie jikoni.


Mungu akufungue ufahamu sasa mjinga wewe.
 
Kwa Iringa hutumia sana Panya. Nao ni viumbe vitumikavyo kwenye issue za kiroho pia. Ni antena ya kichawi.
Kuna wachawi humu wanapinga Kwa nguvu Ili wasojua Elimu hii wasitilie maanani,

Pia Kuna watoto ambao shule zimewafanya kutokujua yaliyo upande wa pili.

KAZI yetu ni kufichua Siri za adui, Kupambana katika Ulimwengu wa Roho na kuwahubiri watu INJILI ya ufalme, waokoke.

Ubarikiwe.
 
Hio heading ya thread yako ulioiweka ingetosha kufikisha ujumbe.

Ulipokuja kuharibu ni kuvipa hatia viumbe vya Mungu.

Zingatia hii misemo .

1.Mchawi mtu paka katumwa
2. Bunduki haiui watu, watu wanaua watu


Kisu kinaua lakini haimaanishi tusikitumie jikoni.


Mungu akufungue ufahamu sasa mjinga wewe.
Najua nilichokiandika.

Wewe ikiwa una Maarifa ongeza.
 
Salaam, Shalom!!

UTANGULIZI.

Ndani ya nyumba zetu, Pana mijusi yenye RANGI nyeupe tofauti na mijusi wa nje. Na KAZI ya mijusi KIMWILI Huwa ni kutafuta na kula WADUDU watambaao na warukao nk nk.

MADA: MAKINIKA NA MIJUSI/ UPANDE WA PILI WA MIJUSI YA NDANI YA NYUMBA.

Kuna mjusi alikuwa akiishi ndani ya nyumba yetu, na tulimchukulia kawaida tu kama mijusi wengine. Tukiwa sebuleni utamuona juu katulia tulii anatuangalia,

Tukiingia chumbani, yupo, Kuna time tulitilia mashaka ,lakini sababu hatukuwa na HAKIKA kuwa Si mjusi wa kawaida, tulipuuza.

Siku moja tumelala, usiku, nikajikuta kwenye vita kubwa sana katika Roho, nilikuwa napambana na mijusi wakubwa sana, mijusi giant ambao nilikuwa napambana nao Hadi JASHO linanitoka,

Nilikuwa nakemea, Kwa Jina la YESU, Damu ya Yesu, vita ilikuwa Kali sana, nilijiuliza kwanini Leo vita imekuwa Kali sana tofauti na vita za siku zingine, niliemdelea kukemea.

Nikiwa katika vita nikashtuka na kuamka, kumbe, mke wangu pia alikuwa akipambana vita kama yangu nae aliposhtuka tukaanza kuulizana nini kilikuwa kinatokea,

Tulijiuliza labda ni wachawi walikuwa wametuvamia, tulipowasha taa, tulishangaa sana kumkuta mjusi ambaye alikuwa akikaa juu ya dari, ameingia ndani ya neti yetu ametulia pembeni mwa Kuta ya Net. Baada ya kumvizia tumuue, alituponyoka na kukimbia.

Tangu siku hiyo, Niko makini sana na mijusi wa aina hiyo ndani ya nyumba na WADUDU wenye kutilia mashaka sababu mijusi wanaweza kutumiwa kama Antenna za kichawi. Yaani unarushiwa makombora Toka kuzimu kupitia mjusi au paka au mbwa au mdoli uliyenunua au kumfuga mwenyewe!!

Pia mijusi ndani ya nyumba wanaweza kukaribisha mapepo ambayo yanaweza kushambulia kupitia mwili wa mjusi.

Pepo halina mwili, hivyo likipata mdoli au kinyago ndani ya nyumba Yako, hupata Mahali pa kukaa na kukushambulia Kwa karibu na nguvu zaidi. Vita ya Wana wa Mungu ni katika Ulimwengu wa Roho, Vita zetu huanzia Rohoni kabla ya kuja mwilini.

SOLUTION.

1. Hakikisha huweki vinyago, midoli ndani ya nyumba. Mapepo yanaweza kuingia ndani ya vinyago na ukapata vita direct Kutokea vitu hivyo.

2. Acha mara Moja kufuga paka na kuishi naye ndani ya nyumba, paka au mbwa, Pepo anaweza kuwaingia na akawatumia kukuattack.

3. Puliza dawa ya kuua mijusi na WADUDU ndani ya nyumba, maana nyumba ya kuishi haipasi kuwa makazi ya chawa, mende, kunguni, viroboto, mijusi ,panya nk nk.

NB: Si mijusi wote ni kama niliyepambana nae Mimi, ni kukupa tu tahadhari kutokupuuzia mambo!!

ANGALIZO: Usilale bila kufanya maombi, funga milango Yako Kwa Damu ya Yesu, zungusha ulinzi katika anga lako na ardhi unayomiliki.

Ikiwa hujaokoka fuatisha Sala hii:
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA. NINAOMBA UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI, NIWEZESHE NIISHI MAISHA MATAKATIFU. Amen


Mungu akubariki.

Amen
Aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea.
"Sijui aliwaza nini Afande Sele kuimba huo msitari?
 
Mimi nadhani paka huwa anasaidia sana hasa jirani na makazi yako kuna nyoka,atawapunguza sana.
Kufuga paka au mbwa ni tofauti na kuishi nao ndani ya nyumba.

Wengine wanalala na vijibwa vidogo chumbani.

Mbwa lake Banda nje Afanye KAZI ya ulinzi nje.

Afu wafuga paka wengi ni wachawi, fuga kuku utamla sup
 
Back
Top Bottom