Making more money - kutengeneza pesa zaidi

Making more money - kutengeneza pesa zaidi

bhikola

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,133
Reaction score
1,668
Habari wanajamii wenzangu,

Ninashukuru sana kwa michango yenu yote katika toipc iliyopita ya kununua gari kwa kutumia mkopo. Ni matumaini yangu mlijifunza jambo, ingawa kuna ambao walifikiri nimetoa vipaumbele. Hapana, ni matumaini yangu wewe kujengeka na kuwa njia bora zaidi ya kuwa na maisha bora zaidi kwa njia nafuu zaidi.

Back to topic, ni kwa jinsi gani unaweza kutengeneza pesa zaidi?
imekuwa kawaida kuwaona wastaafu wanapata kiinua mgongo kitamu lakini baada ya siku kadhaa wanakuwa as if hawakupata hata mia. Kwa wasanii na waburudushaji hali kadhalika, utashangaa ukiambiwa mikataba mtu aliyokuwa anasaign halafu yuko deadly broke.

Tumesikia watu katika mashindano (project fame, big kaka, bongo starehe sachi, na wale wanaokaaga maporini wa kipanya wale sijui wanaitwaje) na bahati na sibu kadhaa (kina fokodam, airtel, bingo nk) wakichota mamilioni ya shilingi, lakini ndani ya siku kadhaa wako empty. tatizo huwa ni nini?

1. wealth doesn't worth the name unless is sustainable. hilo ndo tatizo la kwanza. watu wengi wanapata fedha kwa msimu au kwa vipindi. kwa mfano unakuta mtu anapata lump-sum kwa mara moja then ndo nitolee. ukitaka kujua kama una sustainable wealth creation, angalia "money in" yako. unakuta mtu ana transaction moja tu ya money in zinazobaki ni money out money out money out, mpaka ije ile money in tena. sasa siku hiyo money in ikikata, ndo making money imeishia hapo. sustainability haipo.

2. Fees, taxes, and charges - angalia uwiano wa mapato na kodi, michango, na ada unazolipa. kama uwiano ni zaidi ya 1:3 basi liquidity yako iko chini sana (samahani hapa nakosa kiswahili kizuri cha kulieleza hili, lakini kama kuna wahasibu, na wale watu wa mabenk wakipita hata wanisaidie tu kulieleza hili.

kwa nini wakikuta Acid Test Ratio inazidi hiyo wanasema mtu hakoposheki?) - kwa mfano unakuta mtu anapata mshahara 2.1m lakini akikatwa kodi (payee) + nssf + nhif + raaw/cwt/tuico anabaki na 1.3m maana yake makato yanakaribia au kuzidi 8k. huyu mtu anapoteza pesa nyingi kuliko anazotengeneza na ndiyo maana mfanyakazi ni masikini kuliko mfanyabiashara.

3. Spending - hii kitu watu wengi watabaki kusema ni ishu za kipaumbele cha mtu, sijui bata batani, sijui na bla bla nyingine, lakini kubali kataa, the means justifies the end. so decrease your spending, and increase your earning. Ngoja nikupe stori moja bana ya waganga wa kienyeji siku moja katika hizi stori za waganga wa kienyeji kutoa utajiri, nami nikasafiri mpaka ukingani huko iringa (precisely mafinga).

Nilipofika kwa the most famous sangoma nikawa namstudy anachokifanya hasa kucreate utajiri. katika mengi niliyojifunza, kubwa lilikuwa moja tu. kubana matumizi. anachofanya anakupa masharti ambayo yatakufanya ufanye serving na upunguze spending. mfano atakwambia, ukisafiri kibiashara usile njiani, beba chakula chako, kama unapokwenda kuna ndugu usifikie hotelini fikia kwa ndugu, usibadilishe nguo kwa wiki nzima, usivae viatu vaa sendo tu, ufanye ngono mara moja tu kwa wiki tena jumapili, ukimaliza usiguse chochote mpaka uoge dawa hii. ma mengine.

Mh! So tufanyeje?
1. Tafuta njia za kupata pesa sustainably - fanya biashara, uzalishaji, uwekezaji.

2. Lipa kodi, fees, and charges kwa kiwango kidogo kadri inavyowezekana. matumizi yako binafsi yawe matumizi wa biashara au kampuni.

3. Budget vizuri pesa zako.


Siku njema
 
Sasa lazima watu wajifunze njia za kupata fedha zaidi
 
duh yan kwenye mambo ya maana coment chache kweli.

bado tuna changamoto kubwa.
 
Back
Top Bottom