Makinda kwa fix!!!!!

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
SPIKA wa Bunge, Anna Makinda, amekanusha madai kuwa amepata nafasi hiyo kupitia mkono wa mafisadi na kwamba Mungu wake alikuwa mlangoni kwake.

Hii si mara ya kwanza kwa Makinda kukanusha madai hayo yanayotolewa kupitia baadhi ya vyombo vya habari, vikidai kuwa ameingia katika nafasi hiyo kwa nguvu na ushawishi wa watu wenye fedha, ili kutengeneza mazingira ya baadaye ya kisiasa.

Hata hivyo akizungumza katika chakula cha jioni alichowaandalia waandishi wa habari za Bunge katika Hoteli ya New Dodoma juzi, Spika huyo alisema hajawahi kufikiria kuwa na urafiki na mtu yeyote ambaye ana tuhuma na wala hafikirii kuwatenga kwa kuwa yeye ni mtu wa watu wote.

"Mimi nitafanya kazi kwa kujiamini zaidi na kwa maslahi ya Watanzania wote maana mimi ndiye spika, wala siigizi kwa sababu niliingia pale kwa lengo la kuwatumikia wabunge kwa hiari yangu si kwa nguvu ya mtu,"alisema Makinda.

Spika huyo alisema hata katika kipindi cha kampeni za uspika zilizofanyika mwishoni mwa mwaka jana, alielezwa kuwa baadhi ya wagombea wenzake walikuwa wakifanya kampeni kwenye mabaa lakini aliendelea kupiga magoti na kumuomba Mungu wake kwa kuwa hakuwa na fedha.

Makinda alisema kipindi chake cha wa miaka mitano ya kuliongoza Bunge, anatarajia kukifanya chombo hicho kuwa kimoja na chenye malengo na maslahi ya nchi na si kwa watu binafsi.

Kuhusu waandishi wa habari za Bunge, aliwataka kuwa makini na kutumia kalamu zao kuiunganisha nchi kwa wimbo mmoja bila ya kuleta machafuko.

Alisema kalamu zao zinaweza kuleta mafanikio makubwa kama zitatumika vizuri na kwa kufuata misingi ya taaluma yao.

Waziri huyo wa zamani wa habari, alisema nia yake si kutaka kuwafunga midomo waandishi bali kuwafanya wasimame katika maadili.

"Sina nia ya kuwafunga midomo waandishi wa habari, nataka wawe huru kuandika habari kwa faida ya Watanzania kama ni kuonya, nataka waonye na kama ni kukosoa wakosoe pia lakini iwe ni kwa kila jambo ambalo ni la kweli bila kumuonea mtu," alisisitiza.
Souce; Mwananchi
 
Nafikiri anaona uhai wake hauko mashakani tena baada ya Rostam kujiengua hivyo anaweza kuongea hivyo mbele ya waandishi wa habari.
 
Wana JF,
Wote tunafahamukwamba tangu uhuru hakuna Spika wa Bunge Tanzania amezuiwa na chama kuingia kwenye kinyang'anyilo cha uchaguzi, wengine walikaa mpaka wakafa, hata mzee wetu Msekwa baada ya kutangaza kustaafu, na kulipwa maluplupu ikiwa pamoja na Benzi zito aliguka na kujitupa uwanjani ambako aliangushwa vibaya, lakini hukuzuiwa.
Affirmative kusaidia wanyonge kwenya jamii sawa, lakini kiti cha Spika si zawadi. Rejea mizengwe ilivyo kwenda. mzee wa vijisenti akasema yeye ni kiongozi safi anafaa kugombea, TAKURURU ikasema naaam, si wote tunamjua mkuu wa pale anakotoka, alikofanya kazi zama hizo na waliomweka alipo. Waingereza wakatia kitumbua mchanga, roho mbaya hawa, eti oh, mambo bado, mahakama uingereza hajatoa hukumu na kumfutia mashitaka Mzee wa vijisenti kama TAKURURU ilivyodai. Wajanja, soma mafisadi, wakasuka kikasukika, oh zamu wa wanawake, ebo, kwa nini Usipika, na siyo Katibu Mkuu wa Chama, Jaji Mkuu, Mkuu wa Polisi, Waziri Mkuu na hata rais!!!!!!!!!!!!1 Bwana Shibuda alipojotokeza kugombea uraisi kwa ticketi ya chama cha mapinduzi akaambia, bwana aliyeko Magogoni lazima amalize ngwe yake, na aliyeko mjengoni hana ngwe?
Jamani tusidanganywe huyu mama alibebwa si siri, kibaya zaidi ni kwamba alibebwa na wabaya wa Sitta, period.
 
Inabidi achunge maneno yake, wenzake waliofanya hivyo wana-data zote, wakiamua kuzimwaga hadharani kama mikataba ya UDA ataweka wapi uso wake? Ikiwa kama hizo tuhuma ni za kweli? Kuna fununu kuwa team ya L.A, ilimfuata hadi kijijini kwake kule sijui ni Manda au wapi njombe huko, na fungu zito ili akubali kuwania nafasi hiyo, kwani mwanzoni alitamka kuwa hawezi fany hivyo kwa kuwa anamuheshimi sana mzee 6, lakini ushawishi wa vijisenti ukawa mzito zaidi.
 
BADO HAJAONESHA HILO LA KUWATUMIKIA WABUNGE, LABDA KUWATUMIKIA WANA CCM BUNGENI. Amekuwa akichakachua kanuni na kuwanyima nafsi za kuzungumza wasio wa CCM kwa manufaa ya magamba
 
Awashukurt akina Chenge, Jk, Makamba, na Lowasa. Hawa jamaa walihakikisha Six harudi hapo, na kuhakikisha mwenye hedhi kulikalia kiti cha usipika
 
Back
Top Bottom