Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
- "Upinzani hauwezi kuiua CCM ila CCM itajimaliza yenyewe kwa tabia yake" - Anne Makinda
CCM mazingira ya Kujiondoa yenyewe
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kujiondoa chenyewe madarakani kutokana na tabia ya baadhi ya viongozi kutanguliza maslahi binafsi badala ya chama na wananchi kwanza. Makinda alitoa kauli hiyo juzi wakati akiwasalimu wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Njombe, waliokutana mjini hapa.
Utapeli, Rushwa kuiua CCM
Alisema utapeli ndani ya CCM unatisha na watu hawataki kujenga utamaduni wa ujamaa na kujitegemea na kusisitiza iwapo wanachama watashindwa kujitegemea, chama kitakufa. Alisema hata rushwa kwenye uchaguzi wa CCM inachangiwa na baadhi ya viongozi wasiopenda kufanya kazi na kutegemea kuchuma pesa za rushwa kutoka kwa wagombea. Rushwa ndani ya chama inatokana na tabia hii ya watu kushindwa kufanya kazi halali za kujitafutia kipato na kuishia kuwarubuni wagombea na kuwaomba fedha kwa ahadi ya kuchaguliwa. Iwapo wana CCM wataendelea kuomba fedha katika uchaguzi ni mwanzo wa kuua chama na hata vyama vya upinzani haviwezi kuiua CCM ila CCM itajimaliza yenyewe kwa tabia yake, alisema.
Wabunge si ATM Machine
Alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya wapiga kura wa jimbo lake ambao wamekuwa wakimchangamkia na kumsalimia na mwisho wa salamu, huishia kuomba pesa. Makinda amewataka viongozi wa CCM kurejea misingi ya kiapo cha mwachama na kukifanyia kazi kiapo hicho ambacho kinatamka wazi kuwa sitatumia cheo changu kwa maslahi yangu na iwapo kiapo hicho kitaendelea kukiukwa kwa baadhi ya viongozi wanaochaguliwa kugeuza nafasi zao ni mitaji ya kuombaomba fedha kwa wabunge, chama hicho hakitadumu. Mimi mwenzenu jana baada ya kumaliza mkutano wa mapokezi ya Mangula nilianza kucheza ngoma na muziki na wananchi waliofika katika mapokezi hayo, cha ajabu wengine walikuwa kukisalimia na kuniomba pesa ....sasa hii ni hatari sana kama watu wamekuja wenyewe katika mapokezi baada ya kumaliza mkutano, wanamvamia mbunge na kumwomba pesa, alisema Makinda.
Kutokana na hali hiyo, Spika Makinda aliwataka wanachama wa CCM kufanya kazi na kuwa na shughuli nyingine za kuwaingizia kipato badala ya kuendelea kuwavizia wabunge na kuwaomba pesa na wasipopewa wamekuwa wakiwachukia na kukichukia chama. Makinda aliwataka pia wajumbe wa mkutano huo kuwa na miradi ya kiuchumi au kujiunga katika kilimo badala ya kuendelea kuomba fedha kwa wabunge. Alisema hivi sasa watu wamechoka kuombwa fedha na hata waliokuwa wakikisaidia chama, pia wamechoka hivyo lazima CCM ijitegemee kwa kuwa na miradi ya kiuchumi.