MAKATO YA BENKI

Drayubu

New Member
Nov 16, 2019
1
1
Serikali Yeyote duniani Huwa Ina wajibu wa kuleta unafuu wa maisha Kwa wananchi wake. Kwa namna yeyote serikali inatakiwa kuhakikisha wananchi wake wanafurahia matunda ya kuwa wananchi katika taifa Hilo .

Binafsi ninasikitishwa Kwa mwenendo wa serikali yetu ambavyo imekuwa ikifanya Kwa siku za hivi karibuni. Tozo zimekuwa Kila Kona wakifikiri ndiyo njia pekee ya kuongeza Pato la serikali. Lakini Mimi ni waambie ukiweli, siku zote ndoo inayovuja haiwezi kujaa hata kama utaweka maji Kiasi Gani itaonekana imejaa Kwa muda lakini tundu linaendelea kutoa.

Njia pekee ya kuweza kunusuru taifa hili katika Hali mbaya ya uchumi ni;
1. Kuweka mpango mzuri wa ukusanyaji Kodi(siyo double taxation, mfno mfanyakazi atakatwa Kodi kutoka Kwenye mshahara, atakatwa Kodi kutoka Kwenye kuweka pesa benki, atakatwa Kodi Kwenye kutoa fedha, atakatwa Kodi Kwenye kutumia hiyo fedha). Huu ni uhuni wa Hali ya juu, ni wizi uliopita kiwango.

2. Kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, kundi na Taifa Kwa ujumla Kwa kuleta uwiano wa kiuchumi. Hapa nazungumzia kuondoa Kodi zisizo na Tija Kwa watumiaji bidhaa. Unapoongeza Kodi Kwa sababu ya kusingizia Kuwa sijui Vita ya Urusi na Ukraine imepekelekea kilakitu kupanda Bei siyo sahihi. Angalia Bei za mafuta Tanzania bara na Zanzibar Kuna uwiano Wowote? Hapa ndipo utakapo jua Kuwa Kuna shida, hakuna uwiano, hizi ni ni nchi Moja japo Kuna tofauti ndogo ndogo lakini haziwezi kuweka tofauti Kuwa kubwa Kiasi zilivyo hivi Sasa!.

3. Kuna pesa nyingi sana zinaendelea kufujwa na serikali inaona ni sawa tu. Ripoti ya CAG umeonyesha namna ambavyo fedha za umma zimekuwa zikifujwa, lakiji mpqka Leo hatuoni wahusika wakiwajibishwa. Hii inatoa taswira Kuwa Kuna Uwezekano Kuna mikono ya viongizi wakubwa serikalini katikabufujaji huu. Kwanini wahusika hawachukuliwi hatua? TAKUKURU wako wapi? Nimeona taarifa ikiwazungumzia TAKUKURU ambavyo wamebaina harufu za rushwa katika zoezi la upatikanaji wa nafasi za wahudumu katika zoezi la sensa huko jijini Mbeya, lakini najiuliza Kuwa TAKUKURU Huwa wanaona vitendo hivi kwa wqtendaji wa chini tu? Mbona ripoti ya CAG Huwa hawaitumii kuchunguza vigogo wanaohusika katika ufujaji Mali za umma? Tujitafakari Kama Taifa.

KATIBA MPYA NI LAZIMA, NI SASA!
 
Kama wasomi wetu ndo hao wakiteuliwa kwenye serikali wanashukuru aliyewateua na kumfananisha Mteuzi kuwa sawa na Mungu, hatuwezi kutoka hapa tulipo, kama waziri mwenye dhamana kwa uwezo wake na elimu yake ya uchumi kaona mahali pa kupata fedha za kuendeshea serikali ni tozoo every thing now is tozo basi tunashida kubwa sana, huku deni la Taifa linazidi kupaa!!! Yaani hatuna wasomi au wachumi wanaoweza kutusaidia, na hata akatokea mtu nje ya mfumo akashauri atakejeliwa tu, kama mnakumbuka maneno ya aliyewahi kuwa katibu mwenezi wa ccm akisema unaijua V8 wewe? We need reforms tukianza na katiba mpya then tume huru ili tupate watu competent. Pia tunaweza kujifunza baadhi ya majirani zetu wanavyofanya kwa baadhi ya mambo mazuri, kama kwa Rais wa Zambia na wenzetu kenya hasa kwenye maswala ya matumizi ya serikali na usimamizi wa fedha za umma.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom