Makarani 800 wagomea sensa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Source: Mwananchi | Waandishi Wetu

MAANDALIZI ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu yameingia dosari baada ya matukio kadhaa ya kukwamisha kazi hiyo kujitokeza katika mikoa mbalimbali, ukiwamo Dar es Salaam ambako zaidi ya makarani 800 wamegoma kula kiapo cha utii na kutunza siri.

Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mbali na makarani hao, vipeperushi vyenye ujumbe wa kutaka watu wagomee Sensa vimesambazwa mkoani Arusha, huku mkoani Tanga kukiwa na tukio la Sheikh mmoja kutiwa mbaroni kwa kusambaza vipeperushi vya aina hiyo.

Mgomo wa makarani
Makarani hao waligoma jana ikiwa ni siku yao ya mwisho ya mafunzo ya kazi ya kuhesabu watu na makazi. Makarani hao kutoka vituo mbalimbali kulikotolewa mafunzo hayo, walisema wameamua kugomea kiapo hicho kutokana na fedha zilizotengwa kwa ajili ya malipo ya kazi hiyo kuchakachuliwa kinyume na makubaliano.

Baadhi ya vituo ambavyo makarani wake wamegoma ni Shule ya Sekondari Makumbusho, Kambangwa, Shule ya Msingi Zawadi na vituo kadhaa vilivyopo maeneo ya Buguruni na Kawe.

Baadhi ya makarani hao walionekana wakiwa katika makundi, muda ambao walipaswa kuendelea na mafunzo yao kabla ya kula kiapo cha kushiriki Sensa kwa uaminifu na ukamilifu. Baadhi ya makarani ambao waliomba majina yao yasitajwe gazetini, walisema imekiuka makubaliano ya awali.

"Serikali imesema imetenga Sh141 bilioni kwa ajili ya Sensa. Sisi tayari tuliingia makubaliano nayo kwamba tunatakiwa kulipwa Sh35,000 kwa siku, kwa muda wa siku saba jambo ambalo limegeuka na kuwa kinyume."

"Ukipiga mahesabu fedha ambazo tungetakiwa kulipwa kwa siku hizo saba ni Sh245,000 lakini wao wamekuja hapa na kutupa Sh140, 000 tu. Hatuwezi kuendelea na kazi mpaka tulipwe fedha zetu."

Karani mmoja katika Kituo cha Sekondari ya Kambangwa, alisema wameamua kugomea kiapo baada ya kuona kuwa mpaka mafunzo yanahitimishwa jana, baadhi yao hawajalipwa chochote.

RC Dar: Watalipwa
Akizungumzia madai ya makarani hao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema mpaka jana mchana makarani wote walipaswa kulipwa awamu ya pili ya fedha zao. Alisema awamu ya kwanza ya malipo hayo ilifanywa katika siku tano za mwanzo."Kuna watu wamejichomeka katika zoezi hili, lakini kama kweli karani ameteuliwa lazima atalipwa pesa zake na kama imetokea amesahaulika basi afanye mawasiliano na mratibu wa Sensa wilaya anayotoka ili alipwe," alisema.

Sheikh mbaroni
Katika hatua nyingine Sheikh Juma Koosa (52) anashikiliwa na polisi wilayani Morogoro akituhumiwa kutumia kipaza sauti kuwatangazia wananchi wasishiriki Sensa.

Sheikh huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro, alikamatwa Agosti 19 mwaka huu alipokuwa kwenye Msikiti wa Miembeni, Mazinde mara baada ya kukaribishwa na wenyeji wake kuzungumza.Imedaiwa kuwa Koosa alitoa kitabu chenye kueleza sababu za kuwakataza Waislamu kutokushiriki Sensa mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema Sheikh huyo pia alikutwa na nakala 15 za kitabu hicho.Alisema alikamatwa kutokana na taarifa za baadhi ya waumini ambao walichanganywa na taarifa za mgeni huyo... "Baadhi ya waumini walikubaliana naye huku wengine wakimpinga. Hivyo mtafaruku ukajitokeza na ndipo wale waliopinga wakawasiliana na polisi ambao walifika na kumkamata."

Baada ya kukamatwa alipelekwa Kituo cha Polisi Mombo kwa mahojiano zaidi na kuhamishiwa Makao Makuu ya Polisi Wilaya ya Korogwe, baada ya kuwapo kwa dalili za baadhi ya waumini kuandamana kupinga hatua hiyo.Alisema, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.

CWT
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch amewataka walimu kutosita kudai masilahi yao kwa kuhofia Serikali kuwaondoa katika shughuli mbalimbali za kitaifa.

Oluoch alisema jana kwamba wanao ushahidi wa maandishi kuwa kuondolewa kwa baadhi ya walimu katika Sensa kumetokana na kushiriki kwao katika mgomo ulioandaliwa na CWT kwa lengo la kudai masilahi yao sekta nzima ya elimu nchini.

Alisema CWT bado ipo katika mchakato wa kukusanya takwimu kwa wanachama wake waliotolewa katika Sensa nchi nzima na imebaini kuwa Serikali imefanya hivyo kama njia ya kuwakomoa.

"Tumepata ushahidi unaoonyesha kuwa walimu wamekatwa kwenye zoezi la Sensa kutokana na kushiriki mgomo" alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo haitarudisha juhudi za walimu za kudai masilahi yao kwani madai yao ni muhimu.
 
hii sensa nazidi kuona kama tumekurupuka,
upepo wa siasa siyo mzuri, chama tawala kinatuhumiwa
kwa mengi likiwepo la ufisadi, utesaji, uchumi duni, ubabe,
ilitakiwa mambo yawekwe sawa kwanza, watanzania wa sasa
ni waelewa siyo wakuburuzwa buruzwa tu.
 
Makarani wenyewe walikuwa wakinyanyasika sana, sidhani kama wataifanya hii kazi kwa moyo...
 
kifungu gani cha sheria kitachonifunga mimi muislam nisie na akili kama wanavosema,muislam mpenda ubwabwa kama wanavosema,muislam muabudu majini kama wanavoniita,kipengele gani kitachonifunga kisheria kwa kuboycott kwangu zoez lote hili la sensa?
Mhojiwa halazimishwi kujibu bali hushawishiwa na ndivo ilivoandikwa kwenye hivi vitabu vya madodoso,,
serikali inishawish kwanza kuhusu tamko la uchochez wa dini la tbc na taarifa za uchochez za ofisi ya taifa ya takwimu kisha ndio nitoe taarifa zangu
miaka yote sikugoma why nigome mwaka huu pekee??
 
Makarani wenyewe walikuwa wakinyanyasika sana, sidhani kama wataifanya hii kazi kwa moyo...

Sio kunyanyasika tu kuna watu wamepachikwa wengi wasiostahili wamewekwa na wakuu wa zaoezi la Sensa yaani hadi sasa wameshaanza kugombana wao kwa wao.
 
Watajiju ndio raha ya kuchakachua, unajua Walimu walikuwa watu very responsible katika sensa miaka yote tena wao ni watumishi wa serikali hivyo hata akikosea kuna mahali pa kumpata sasa wamechukua mseto utakuja sikia kuna wengine hawakutokea kufanya kazi .
 
Ukitaka sikia vioja njoo Tanzania, makalani hadi wasiojua kusoma na kuandika pia wamo. Uozo umeanzia serikalini sasa hadi wajumbe wa nyumba 10 ni hakuna kitu.
 
Serikali itajutia kuwaengua walimu katika hili, maana walimu wao ni wapole wanyeyekevu hata wasip[olipwa kwa wakati wangeifanya hii kazi kwa moyo. Mi nakwambia katika sensa hii tutegemeee data nyingi za kupikwa. Masela lazima wapike tu hizi maana wengi wao wamefuata mshiko tu
 
kifungu gani cha sheria kitachonifunga mimi muislam nisie na akili kama wanavosema,muislam mpenda ubwabwa kama wanavosema,muislam muabudu majini kama wanavoniita,kipengele gani kitachonifunga kisheria kwa kuboycott kwangu zoez lote hili la sensa?
Mhojiwa halazimishwi kujibu bali hushawishiwa na ndivo ilivoandikwa kwenye hivi vitabu vya madodoso,,
serikali inishawish kwanza kuhusu tamko la uchochez wa dini la tbc na taarifa za uchochez za ofisi ya taifa ya takwimu kisha ndio nitoe taarifa zangu
miaka yote sikugoma why nigome mwaka huu pekee??

sheria ya takwimu namba moja ya 2002.
 
hii sensa nazidi kuona kama tumekurupuka,
upepo wa siasa siyo mzuri, chama tawala kinatuhumiwa
kwa mengi likiwepo la ufisadi, utesaji, uchumi duni, ubabe,
ilitakiwa mambo yawekwe sawa kwanza, watanzania wa sasa
ni waelewa siyo wakuburuzwa buruzwa tu.
Hata mimi Mamndenyi nilikuwa na mawazo kama hayo, kulikuwa na haja gani ya kufanya sensa sasa wakati nchi imekabiliwa na misukosuko kadhaa - madai ya wafanyakazi wa umma hayatekelezwi, mazingira yao ya kazi ni magumu, hakuna vifaa, ubovu wa majengo pamoja na hayo uozo wa kisiasa ikiwemo wizi wa mchana, kansa ya ufisadi kiasi cha wananchi kukosa imani kabisa na viongozi na serikali.

Tungekosa nini kama tungesubiri hali ya uchumi na kisiasa kutulia? Jawabu nililopata ni moja, kwenye sensa kuna mlo na watu walishajipangia kuneemeka, na ndio maana makarani wa sensa wanadhulumiwa hivi wa kijiona. Sitoshangaa wakiambiwa watie saini vocha mbili, moja ya 245,000/= nyengine ya 140,000/=. Na hiyo ni kwa mjini, vijijini usishangae wanalipwa 70,000/= tu.
 
Last edited by a moderator:
Ongopa sana fisi mwenye njaa hula kila aina ya mifupa.Dr .Slaa alisema juzi Morogoro ccm inachakachua hadi pesa za msaada za UKIMWI.Ifike mahali sasa serikali ichukue hatua kali mara moja kwa watu wanaondelea kuchakachua pesa za walala hoi.
 
Serikali ya wachakachuaji ni balaa, kwanza 35,000 kwa siku ni kidogo sana lakini bado wanataka kuichakachua tena!!
 
Wasitumie mgongo wa mgomo wa walimu kuwaengua walimu kwenye sensa,sema kuna maofisa wa serikali na wanasiasa walitumia mgomo ule kuihadaa serikali kuwa kama walimu watashiriki katika sensa watahujumu,na serikali ikaingia mkenge wakaona kama hoja ile inaukweli,kumbe wale maofisa walitaka wapate nafasi ya kupiga rushwa,mbona tuna ushahidi kibao kwa baadhi ya ma DC,MAMEYA,MADASI NK katika baadhi ya maeneo walikuwa wanauza zile nafasi kwa sh.100,000/.na zaidi kwa kichwa kimoja,mkitaka chunguzeni mtapata ukweli huo.
Kama walimu wana uwezo wakuhujumu sensa,mbona madaktari hawakuhujumu wagonjwa?kwani madai yao yalitekelezwa?acheni kuuhadaa umma,uroho wa pesa za rushwa ndo ulifikia hapo,acheni kuwaonea walmu.PINDA naye kalewa madaraka,nilimskia akijibu swali bungeni juu ya suala hili,eti tulitaka kuruhusu makundi mengine ya watu kushiriki,awali hamkulijua hilo? au ndo huo ulevi wenyewe wa madaraka,mmefunga shule watoto wa walalahoi wanakosa masomo eti sensa,sensa inazuia nini watoto kwenda shule?
 
Source: Mwananchi | Waandishi WetuMAANDALIZI ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu yameingia dosari baada ya matukio kadhaa ya kukwamisha kazi hiyo kujitokeza katika mikoa mbalimbali, ukiwamo Dar es Salaam ambako zaidi ya makarani 800 wamegoma kula kiapo cha utii na kutunza siri.Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mbali na makarani hao, vipeperushi vyenye ujumbe wa kutaka watu wagomee Sensa vimesambazwa mkoani Arusha, huku mkoani Tanga kukiwa na tukio la Sheikh mmoja kutiwa mbaroni kwa kusambaza vipeperushi vya aina hiyo. Mgomo wa makaraniMakarani hao waligoma jana ikiwa ni siku yao ya mwisho ya mafunzo ya kazi ya kuhesabu watu na makazi. Makarani hao kutoka vituo mbalimbali kulikotolewa mafunzo hayo, walisema wameamua kugomea kiapo hicho kutokana na fedha zilizotengwa kwa ajili ya malipo ya kazi hiyo kuchakachuliwa kinyume na makubaliano.Baadhi ya vituo ambavyo makarani wake wamegoma ni Shule ya Sekondari Makumbusho, Kambangwa, Shule ya Msingi Zawadi na vituo kadhaa vilivyopo maeneo ya Buguruni na Kawe.Baadhi ya makarani hao walionekana wakiwa katika makundi, muda ambao walipaswa kuendelea na mafunzo yao kabla ya kula kiapo cha kushiriki Sensa kwa uaminifu na ukamilifu. Baadhi ya makarani ambao waliomba majina yao yasitajwe gazetini, walisema imekiuka makubaliano ya awali.“Serikali imesema imetenga Sh141 bilioni kwa ajili ya Sensa. Sisi tayari tuliingia makubaliano nayo kwamba tunatakiwa kulipwa Sh35,000 kwa siku, kwa muda wa siku saba jambo ambalo limegeuka na kuwa kinyume.”“Ukipiga mahesabu fedha ambazo tungetakiwa kulipwa kwa siku hizo saba ni Sh245,000 lakini wao wamekuja hapa na kutupa Sh140, 000 tu. Hatuwezi kuendelea na kazi mpaka tulipwe fedha zetu.”Karani mmoja katika Kituo cha Sekondari ya Kambangwa, alisema wameamua kugomea kiapo baada ya kuona kuwa mpaka mafunzo yanahitimishwa jana, baadhi yao hawajalipwa chochote. RC Dar: WatalipwaAkizungumzia madai ya makarani hao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema mpaka jana mchana makarani wote walipaswa kulipwa awamu ya pili ya fedha zao. Alisema awamu ya kwanza ya malipo hayo ilifanywa katika siku tano za mwanzo.“Kuna watu wamejichomeka katika zoezi hili, lakini kama kweli karani ameteuliwa lazima atalipwa pesa zake na kama imetokea amesahaulika basi afanye mawasiliano na mratibu wa Sensa wilaya anayotoka ili alipwe,” alisema. Sheikh mbaroniKatika hatua nyingine Sheikh Juma Koosa (52) anashikiliwa na polisi wilayani Morogoro akituhumiwa kutumia kipaza sauti kuwatangazia wananchi wasishiriki Sensa.Sheikh huyo ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro, alikamatwa Agosti 19 mwaka huu alipokuwa kwenye Msikiti wa Miembeni, Mazinde mara baada ya kukaribishwa na wenyeji wake kuzungumza.Imedaiwa kuwa Koosa alitoa kitabu chenye kueleza sababu za kuwakataza Waislamu kutokushiriki Sensa mwaka huu.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema Sheikh huyo pia alikutwa na nakala 15 za kitabu hicho.Alisema alikamatwa kutokana na taarifa za baadhi ya waumini ambao walichanganywa na taarifa za mgeni huyo... “Baadhi ya waumini walikubaliana naye huku wengine wakimpinga. Hivyo mtafaruku ukajitokeza na ndipo wale waliopinga wakawasiliana na polisi ambao walifika na kumkamata.”Baada ya kukamatwa alipelekwa Kituo cha Polisi Mombo kwa mahojiano zaidi na kuhamishiwa Makao Makuu ya Polisi Wilaya ya Korogwe, baada ya kuwapo kwa dalili za baadhi ya waumini kuandamana kupinga hatua hiyo.Alisema, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote.CWTKaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch amewataka walimu kutosita kudai masilahi yao kwa kuhofia Serikali kuwaondoa katika shughuli mbalimbali za kitaifa.Oluoch alisema jana kwamba wanao ushahidi wa maandishi kuwa kuondolewa kwa baadhi ya walimu katika Sensa kumetokana na kushiriki kwao katika mgomo ulioandaliwa na CWT kwa lengo la kudai masilahi yao sekta nzima ya elimu nchini.Alisema CWT bado ipo katika mchakato wa kukusanya takwimu kwa wanachama wake waliotolewa katika Sensa nchi nzima na imebaini kuwa Serikali imefanya hivyo kama njia ya kuwakomoa.“Tumepata ushahidi unaoonyesha kuwa walimu wamekatwa kwenye zoezi la Sensa kutokana na kushiriki mgomo” alisema na kuongeza kuwa hatua hiyo haitarudisha juhudi za walimu za kudai masilahi yao kwani madai yao ni muhimu.
Kosa la kuwabania walimu linawatafuna
 
Back
Top Bottom