Makapuku Forum

Makapuku Forum

C5b9ggQWUAAATtI.jpg
 
4badf8464cd9e4fd39aac7864133fdd1.jpg



Chelsea anaendelea kukimbia tu hakuna tabu hapo..... Tabu ni kwa wale wanaomkimbiza. Kinachowafanya Chelsea wawe hapo walipo ni kujua namna ya kuumaliza mchezo pamoja na Yule ng'olo kantelele na hazard wake basi.

Huu ni muda wa kuvaa jezi za Chelsea na kuvua mashati na blauzi zenu..... Mpaka sasa hivi jezi ya kante haijafika sokoni kwetu.... Kama anavyofanya shughuli na kuipata nayo ni shughuli.

Best player on the field ng'olo kante..... Kamfanya fabregas afanye kazi rahisi katika wakati mgumu katika nafasi ya matic... Ng'olo Kante wachache sana wanaopigiwa makofinna wazungu.

Chelsea 3-1 Swansea city.....
 
3d81cd80b8a7a15868ac4d6c49066777.jpg


The same Yanga the same problem 10 man na kushindwa kupata ushindi kwa mara nyingine tena.....
Yanga ni wazuri sana katika timing score na kuuanza mchezo ila wanatatizo katika kuumaliza mchezo , hili ni tatizo la kwanza la Yanga katika michezo mikubwa..... tatizo la pili ambalo GL naye amelishindwa ni kuutawala mchezo wakati timu pinzani wapo pungufu.

Uwepo wa Kamusoko katika kiungo cha Yanga, Yanga walichukua himaya yote ya kiungo na kuanzia hapo Yanga wakaonekana kuwamiliki Simba.... Walichokikosa Yanga ni Said Ndemla wao katika benchi kuja kuchukua nafasi ya Thaban Kamusoko tu na sio Juma Makapu sababu tayari ndani kulikuwa na Justine Zulu.....

Mipango ya Simba ilianza kufia katikati mwa uwanja, sehemu ambayo Kamusoko alikuwa ameweka kambi, kilichowabeba Simba ni faida ya kuwa na Said Ndemla wao katika bench.

Said Ndemla ndio mtu wa kwanza aliyeanza kuwarudisha Simba mchezoni. Kamusoko ndio mtu wa pili aliyewarudisha Simba mchezoni.... Na mwisho shiza kichuya ndio mtu wa mwisho kuwarudisha Simba mchezoni.

Alichokifanya bukungu ndicho kilichowapa ushindi Simba.... Hapa lawama imetumika kuliko fedheha......

Mwamuzi ameonekana kuumudu mchezo sababu mchezo ulitawaliwa na nidhamu na ufundi sana kwa timu zote mbili..... Credit kwa Mwamuzi. Hapa wachezaji wamefundishika vema.

Saimon Msuva alikuwa vizuri sana katika zile one against one kama alivyokuwa Laudit Mavugo.... Credit kwao katika mchezo huu.

Kichuya punguza sifa umewafanya wenzetu walale bar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom