Makapuku Forum

1942 - Eusebio anazaliwa.

Ni straika wa zamani wa Ureno mzaliwa wa Msumbiji. Anachukuliwa kama mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea Ureno.

Aliibuka mfungaji bora katika komne la dunia la mwaka 1966 lililofanyika pale England kwa Malkia.

Alifariki mwaka 2014.
 
1947 - Tostao anazaliwa.

Nyota wa zamani wa Brazil, anatajwa kama mmoja ya viungo bora wa uchezaji kutoka Brazil.

Alikuwepo Kikosini wakati Brazil ikitwaa kombe la Dunia la mwaka 1970 pale Mexico. Alikuwepo na akina Pele, Jaizinho, Carlos Alberto Torres na wengineo katika timu bora kabisa kuwahi kutokea kwa mujibu wa FIFA.
 
1967 - David Ginola anazaliwa.

Winga wa zamani wa Newcastle United, Tottenham na timu ya taifa ya Ufaransa.

Anatajwa kama sababu ya Ufaransa kushindwa kufuzu kombe la Dunia la mwaka 1994, baada ya Ufaransa kufungwa mechi ya mwisho ya kufuzu 2-1 na Bulgaria.

Mpira ukiwa unaelekea dakika za lala salama, alipewa pasi akaipoteza wapinzani wakachukua mpira wakaenda kufunga, Ufaransa akashindwa kufuzu. Akalaumiwa sana na Kocha wake wa wakati huo Gerald Houllier.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…