Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20250614_062705_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20250614_062720_Opera%20Mini.jpg
 
Paka wakubwa hawazalishi tena lactase, ambayo ni enzimu muhimu kwa kumeng’enya lactose.

NB: Lactose ni sukari inayopatikana kwenye maziwa, na bila ‘lactase’, paka hawezi kuyameng’enya vizuri — jambo linaloweza kumsababishia matatizo ya tumbo kama vile kuharisha au gesi.
Screenshot_20250616_142942_InstaPro2%20.jpg
 
Katika kila kundi la Clownfish, samaki aliye na nguvu zaidi hubadilika jinsia na kuwa jike, na huwa ndiye jike pekee anae endeleza uzao. M

Dume anayefuata kwa kuwa na nguvu zaidi ndio huwa mwenza pekee kwa huyo jike. Ikiwa jike atakufa, dume huyo mwenye nguvu zaidi hubadilika na yeye kuwa jike, na dume mwingine kutoka kwenye kundi mwenye nguvu zaidi huja kuchukua nafasi.
Screenshot_20250616_143040_InstaPro2%20.jpg
 
Ifikapo umri wa miaka 2 hadi 3, watoto wengi huanza:

- Kutambua jinsia yao wenyewe (ikiwa ni mvulana au msichana).

- Kutambua jinsia ya watu wengine.

- Kuonyesha tabia zinazohusiana na jinsia yao — kama kupendelea aina fulani ya vitu vya kuchezea, mavazi, au shughuli zinazohusiana na jinsia yao katika tamaduni zao.

Hii haimaanishi kuwa wanaelewa kabisa utambulisho wao kijinsia, bali huanza kuwa na hisia ya utambulisho binafsi kulingana na jinsia yao, na mara nyingi huiga tabia wanazoziona kwa watu wazima au wenzao wa jinsia moja.

Mfano:
Mvulana wa miaka 3 anaweza kusema, “Mimi ni mvulana” na kupendelea kuchezea ‘toy’ za magari au kwa msichana anaweza kusema pia nae, “Mimi ni msichana” na kupendelea kucheza na midoli n.k

Screenshot_20250616_143430_InstaPro2%20.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom