FARHAN KIHAMU
Huwa napenda sana kumsoma Emiliano Butragueno na falsafa zake kuhusu mpira, kisha Washindi kama Pep Guardiola, Wajivuni kama Jose Mourinho na Wajuzi kama Zinadine Zidane bila kusahau hekima kama za Carlo Ancelloti.
Kwa Butragueno aliwahi kusema mpira ni mchezo wa nyakati na timu ikipoteza atasemwa hata Mlinzi wa klabu ili mradi ipatikane sehemu ya kushikia lakini ukweli ni kuwa mpira una matokeo yake na maajabu hutokea, upe heshima mpira usilaumu.
Kwa Upara Pep Guardiola yeye mara zote anaamini Mashabiki au watu wa mpira wana tabia ya kukinai kisha kuhukumu, Simba inaweza kufungwa halafu mjadala ukawa Aishi au ghafla Zimbwe, au Bocco mzee ama Kapombe amechoka, hapo wamekinai hata kama hakuna uhalisia, Pep huwa hasikilizi Mashabiki kwakuwa anawajua.
Jose Mourinho mjivuni sana lakini its okay to be arrogant! Sioni sababu ya Simba kupoteana kisa mechi mbili, waliwahi kuwa na nyakati ngumu kama hizi na bado walipenya, waliwahi kuwa kundi moja na Vita, Ahly na JS Saoura, nani aliwapa nafasi Simba? Lakini walipenya.
Wala huhitaji propaganda ama Afisa Habari akuhamasishe bali rekodi zipo wazi na vitabu vinajieleza! Ilishawahi kuaminika Simba hatoki mbele ya Zamalek, ilitokea nini? Ilishawahi kuaminika Simba ana wazee wengi, je wamecheza robo ngapi? Nani anawazidi Afrika Mashariki? Ni sahihi kuwa na kiburi kwakuwa Historia ipo na ndio njia ya kupita nyakati ngumu.
Timu ambayo imetoka kufanya vizuri playoffs inakuwaje mbaya ghafla!? Timu ambayo imefanya pre season vizuri inakuwaje mbaya ghafla? Na kama Shabiki unaamini vipi kirahisi kuwa timu mbovu? Lazima uheshimu nyakati kwenye mpira, ni kawaida kila timu inapitia.
Mashabiki, Wanachama na Viongozi wanapaswa kutulia na kuwa ushirikiano kama Wavuta Sigara! Football is a game of Mathematics, zinahitajika tu hesabu nzuri ili wakae sehemu nzuri, haipaswi kuiondosha Simba kwenye michuano.
Hard times, create strong People and character! Time to wake the Lion and he has to roar, sure he has to! Another day, another fight!