Makapuku Forum

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema hakutokuwa na ununuzi wa umeme wa LUKU kwa siku nne kuanzia Agosti 22 - 25, 2022 kila siku kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata katika mfumo wa LUKU.

Meneja Mwandamizi wa TEHAMA wa TANESCO, Cliff Maregeli amesema matengenezo haya yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa LUKU na amewataka Wananchi kununua umeme wa kutosha mapema katika kipindi hiki kujiandaa.

"Shirika linashauri Wateja wake kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii” #MillardAyoUPDATES

UPDATE: 15:38

TANESCO imetangaza kuahirisha zoezi hili na kusema “Tutawajulisha pale tutakapokuwa tayari kuendelea na zoezi hilo, Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza”
 
mauaji ya wivu wa kimapenzi yamekua mengi sana
 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema linatarajia kubadili jina la ugonjwa wa homa ya nyani ambapo sasa limetoa fursa kwa Wananchi wa dunia kupendekeza jina lisilokuwa na unyanyapaa kwa ugonjwa huo unaoenea kwa kasi.

Hadi sasa Watu 31,000 wameambukizwa duniani kote na wengine 12 wamekufa ambapo kwa wiki kadhaa Shirika hilo limekuwa likielezea wasiwasi wake kuhusu jina linalotumiwa kwa ugonjwa huo.

Wataalamu wanaonya kuwa jina hilo linaweza kusababisha vitendo vya unyanyapaa kwa nyani ambapo hivi karibuni nchini Brazil kumeripotiwa vitendo vya Watu kuwashambulia tumbili kutokana na hofu ya ugonjwa huo.

Virusi hivyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza kwenye nyani waliohifadhiwa kwa ajili ya utafiti nchini Denmark mwaka wa 1958 lakini ugonjwa huo ukagundulika kwa mara ya kwanza kwa Binadamu mwaka 1970 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 
Mahakama ya Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe imemuhukumu miaka 30 jela Mwanaume aitwae Joseph Mwajombe (33) Mkazi wa kijiji cha Lulanzi, kwa kosa la kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 15.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo James Mhoni amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 7, 2022 baada ya kutoka kumpakia Binti huyo kwenye pikipiki yake akitoka shuleni hadi eneo la jirani na nyumbani kwao alikomfanyia ukatili huo.

Hakimu amesema alipofika kwenye eneo hilo ambako kuna bwawa alimwambia Binti yake kuwa amewasiliana na Freemason ambao walibandika tangazo lao kwenye nguzo ya umeme ambao wamemuagiza afanye naye mapenzi ili apate utajiri hivyo akamuomba binti yake huyo amkubalie.

Hakimu amesema Mtoto huyo alikataa kufanya hivyo ndipo Baba huyo akampiga na kumuingilia kimwili kwa nguvu na baadaye kumrudisha binti huyo nyumbani kisha akaondoka kuelekea kusikojulikana na ilipofika usiku Binti alishindwa kuvumilia na kuanza kulia huku akimsimulia Mama yake kilichotokea ambapo Mama huyo akatoa taarifa upesi kwa Mtendaji wa kijiji aliyeongozana na Mgambo kumsaka na kumkamata Mtuhumiwa na kumpeleka Polisi ambako alikiri kutenda kosa hilo.
 
James Msengi Mkazi wa Tabora anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 amenusurika kifo baada ya kujaribu kujiua kwa kujikata na kisu shingoni akiwa kwenye kituo cha Mabasi cha Msamvu mkoani Morogoro.

AyoTV na millardayo.com zimefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro alikolazwa Majeruhi huyo ambaye amesema alikuwa anasafairi kutoka Dar es salaam kuelekea kwao Tabora lakini alipofika katika kituo hicho cha mabasi aliamua kujikata kwa makusudi shingoni kwa lengo la kujiua kutokana na ugumu wa maisha ambao ulisababishwa na kukosa ajira.

Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Scholastika Ndunga amethibitisha kumpokea Majeruhi akiwa katika hali mbaya na kutokwa na damu nyingi shingoni ambaye alianza kupatiwa matibabu na sasa anaendelea vizuri.

Shuhuda wa tukio hilo Mzee Ibrahim Omary ambaye Majeruhi alitumia kisu chake cha kuuzia miwa kujikata koromeo amesema kuwa Mtu huyo alifika katika eneo analofanyia biashara na kutaka auziwe muwa ambao haujamenywa lakini walishangaa baada ya kupewa kisu akaanza kujichinja.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…