Makapuku Forum

MSUVA ATUA SAUDI, KULAMBA MILIONI 28 KWA WIKI
.
Mtanzania [emoji1241] Simon Msuva (28) amejiunga na klabu ya Al Qadsiah ya Saudi Arabia [emoji1210] kwa mkataba wa mwaka mmoja.
.
Msuva amesaini mkataba huo utakaomfanya alipwe mshahara wa $ 12,000 kwa wiki (Sh 28 milioni). Wa mwezi atakunja $ 50,000 (Sh 117m)
 
AMAZULU WAMENOGEWA KWA SIMBA
.
Klabu ya Amazulu inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini [emoji1221] wameamua kujilipua tena baada ya kunasa saini ya Rally Bwalya [emoji1268] sasa wamerudi tena kwa kutuma Ofa nono wakihitaji saini ya kiungo mwingine wa Simba, Sadio Kanoute (25) [emoji1159]
.
Ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa kina viungo wakabaji saba, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Erasto Nyoni, Nassor Kapama, Thadeo Lwanga, Victor Akpan na Sadio Kanoute.
 
AKPAN APEWA NAMBA YA WAWA
.
Kiungo mkabaji wa Simba, Victor Akpan [emoji1184] amekabidhiwa majukumu mapya baada ya kupewa jezi namba sita [6] aliyokuwa anavaa beki wa zamani wa timu hiyo, [emoji1081] Pascal Wawa.
.
Akpan amepewa jezi aliyoanza kuitumia tangu ametua ardhi ya Tanzania akiitumikia Coastal Union ambayo ameifanyia makubwa na kuishawishi Simba kumwaga mamilion ili waweze kupata saini yake.
 
POCHI NENE HII YA SAKHO HAIJAWAHI TOKEA
.
Winga hatari, Pape Ousmane Sakho [emoji1211] amewashtua mabosi wa Simba baada ya Mabingwa wa Afrika Wydad Casablanca [emoji1173] kutuma ofa ya donge nono ili kumng’oa Msimbazi.
.
Kwa mujibu wa Maghrib Foot, Wydad wametuma ofa ya Dola 800,000 (Sh1.8 bilioni) wakimtaka Sakho, taarifa zinasema kuwa viongozi wa Simba wapo tayari kumuachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 waliyemsajili msimu uliopita kutoka Teungueth FC.
.
 
[emoji1081] | WAWA [emoji3591] SINGIDA BIG STARS [emoji294]️
.
Beki wa kimataifa kutoka Ivory Coast aliyeagwa na Simba kwa heshima, Pascal Wawa [emoji1081] amerejea nchini na kutua Singida Big Stars.
.
Taarifa za kuaminika kutoka kwenye chanzo changu ndani ya Singida BS ilieleza nyota huyo kajiunga na timu hiyo, ikiwa ni pendekezo la kocha Pluijm na msaidizi wake, Mathias Lule aliyekuwa akiifundisha Mbeya City.
.
Baada ya Wawa kutua nchini usiku mwingi juzi alijiunga rasmi na timu hiyo moja kwa moja katika maandalizi yanayoendelea jijini Arusha.

………..
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Wakiuliza ni nani pembeni yake, waambie ni Augustin Azuka, wakiuliza ni nani waambie ni JAY JAY OKOCHA, ndio alikuwa fundi sana mpaka akapewa jina mara mbili

Wakiuliza ilikuwaje huyo mtoto pembeni akasimama nae? Kwanza waambie anaitwa Pape “THE PAPA OF STUNNERS”Ousmane Sakho kutoka Senegal [emoji1211] ambaye alicheza Simba

Wajukuu watauliza ilikuwaje sasa akawa hapo? Waambie ulikuwa ni mwaka mmoja ambao alipiga goli bora sana pale Taifa dhidi ya Asec Mimosa ya Aziz Ki, kwenye michuano mikubwa Afrika na sio kombe la Kuku pale Ketaketa huko Ulanga, Morogoro

Watauliza ulikuwa mwaka gani Babu? Ee bhna wewe futa kwanza machozi kisha waambie, ni mwaka ambao baridi ilikuwa kali sana Dar Es Salaam, mwaka ambao mpaka Kariakoo walivaa masweta, naam ndio mwaka huo

Kwani hilo bao lilikuwaje Babu? Futa tena machozi kisha waambie, ilikuwa krosi hatari sana ya Mjukuu wa Mbaraka Mwinshehe, ilikuwa krosi ya Mluguru wa Morogoro @shomari_12_kapombe moja kati ya beki bora kizazi kile

Babu mbona unalia sana? Wajukuu zangu nalia kwakuwa naumia, nadhani japo sina uhakika niliishi kuishuhudia Simba bora zaidi kuwahi kutokea ambayo hamtopata bahati ya kuiona kwakuwa its once in a lifetime

Pole sana Babu tunakuhurumia sana! Hapana Wajukuu zangu jihurumieni ninyi ambao hamkupata kuishi kuliona bao hilo, hamkupata kuishi kumfahamu hata Clatous Chama kutoka Zambia, au Aishi Manula wa Morogoro

Nawahurumieni ninyi na vizazi vyenu kwakuwa hamkuwahi kupata kuiona Simba bora kuwahi kutokea, endeleeni kuenjoy na simulizi za @gharib_mzinga23 @mwakalobo_jr pale Youtube ya AZAM TV, lakini sisi tuliishi kuyaona

Mzinga yupo zake Kilwa hivi sasa kazeeka, yule Mwakalobo karudi zake Mbeya anakula pombe na Wanyakyusa wenzake, ziko wapi zile nyakati??

 
Picha ambazo haziuzwi popote na hazinunuliki popote, hazipatikani kila sehemu na hazipigwa kirahisi

Picha ambazo unazipata kutokana na kuwa bora, picha ambazo Cameraman anatulia kama wewe na Mkeo au Mumeo, picha ambazo zinatazamika kama “BABY NISHUKIE WAPI”

Picha ambazo sio Cameraman anaweza kuzipiga! Picha ya SIMBA na BAYERN MUNICH
 
[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr

Kasimama mbele ya Magwiji wa soka la Afrika, kakumbatiwa na Nahodha wa Senegal Sadio Mane, kakumbatiwa na Kocha na Legend wa Senegal Aliou Cisse

Kafunga bao bora dhidi ya klabu bora moja wapo Afrika, ASEC Mimosa kisha kaitwa jukwaani na kapewa tuzo na Gwiji wa mpira JAY JAY OKOCHA wa Nigeria [emoji1184]

Kahutubia soka la Afrika kisha kabeba tuzo yake na kushuka kwenye stage, akaacha kumbukumbu kuwa anacheza Simba ya Tanzania na alifunga kwenye dimba lenye jina la Rais wa tatu wa Tanzania [emoji1241]

Mabibi na Mabwana ni filamu fupi ya dakika tano ya Mfungaji wa bao bora Afrika, PAPE OUSMANE SAKHO wa Simba na Senegal [emoji1211]
 
Raheem Sterling in Chelsea kit [emoji419] usajili ambao Kocha Thomas Tuchel aliutaka sana, bila shaka anakuja kutatua shida kwenye suala la Mawinga, naamini ni ingizo zuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…