Makapuku Forum

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameikimbia Nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi wakati huu ambao bado maandamano makubwa kuhusu uchumi yakiendelea kufanywa na Wananchi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 kabla ya kukimbia na Ndege alikua amejificha baada ya umati kuvamia makazi yake siku ya Jumamosi.

Kiongozi mwingine aliyekimbia Nchi ni Waziri wa zamani wa Fedha Basil Rajapaksa ambapo vyanzo mbalimbali vimesema anaelekea Marekani.
 
Spika wa Bunge la Sri Lanka ametangaza kuwa Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe ameteuliwa kuwa Rais wa muda wa nchi hiyo baada ya Rais kukimbia nchi.

Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Kaimu Rais ambapo Spika amesema Rais Gotabaya Rajapaksa alimfahamisha kuhusu uteuzi huo chini ya Kifungu cha 37.1 cha katiba ya Sri Lanka, hata hivyo hakuna neno la moja kwa moja kutoka kwa Rais Rajapaksa mwenyewe kuwa amemteua Waziri Mkuu kukaimu nafasi yake.

Matangazo yote katika siku za hivi karibuni yametoka kwa Spika wa Bunge na Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa mujibu wa Katiba ya Sri Lanka, nafasi ya Raos ikiwa wazi, Waziri Mkuu ataapishwa na kukaimu kwa muda mpaka atakapochaguliwa Rais kutoka miongoni mwa Wabunge.

Uchaguzi huo unapaswa kufanyika ndani ya siku 30 baada ya Rais kujiuzulu, Spika wa bunge la Sri Lanka amesema uchaguzi unaweza kufanyika July 20, 2022.

Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa ameikimbia nchi hiyo kwa ndege ya kijeshi, huku kukiwa na maandamano makubwa kuhusu mzozo wa kiuchumi, Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 amekimbilia Maldives.
 
Profesa Lallan Kumar ambaye ni Mhadhiri wa Chuo kiitwacho Nitishwar nchini India ameamua kurudisha mshahara wake wa miaka miwili kwa sababu Wanafunzi hawajatokea darasani kuhudhuria somo analofundisha.

Vyombo vya habari nchini India viliripoti kuwa Lallan Kumar ambaye ni Profesa Msaidizi wa lugha ya Kihindi katika Chuo cha Nitishwar jimbo la Kaskazini la India la Bihar amerudisha kwa Chuo hicho mshahara wenye thamani ya £uro 25,108 ambazo ni sawa na Tsh. milioni 58.7, Ksh. milioni 2.9 “Hakuna Mwanafunzi aliyefika darasani ili kufundishwa sasa mshahara ni wa nini?” alisema Profesa Kumar.

NDTV India wameripoti kwamba Mkuu wa Chuo amesema madarasa yalitatizwa kutokana na janga la corona japo Profesa Kumar anasema kitendo cha Wanafunzi kutotokea kwenye madarasa yake kimemfanya aogope "kifo cha kitaaluma" kwenye kazi yake.

Wataje Waalimu wako wawili ambao wangerudisha pesa kama Profesa Kumar.
 
Wizara ya Afya kupitia kwa Mganga Mkuu wa Serikali Aifello Sichwale imethibitisha vifo vya Watu watatu ambao wamefariki kutokana na kuugua maradhi mapya ambayo bado hayajulikana jina lake Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

“Wizara ya Afya ilipokea taarifa toka kwa Mganga Mkuu Lindi kuwa Ruangwa kuna Ugonjwa usio wa kawaida kutoka Kituo cha Afya Mbekenyera, ambapo ndani ya siku 3 (tarehe 5 na 7 July 2022) walipokea Wagonjwa 2 wakiwa na dalili za homa, kuvuja damu (hususan puani), kichwa kuuma na mwili kuchoka sana”

“Wizara iliunda timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya dharura na Majanga, Epidemiolojia, Mkemia Mkuu wa Serikali, NIMR, Chuo kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliungana na timu ya Mkoa ikihusisha Idara ya Mifungo”

“Hadi hadi kufikia tarehe 12 Julai kulikuwa na jumla ya Wagonjwa 13, kati yao, 3 wamefariki, wawili waliokuwa wametengwa katika kituo cha Afya Mbekenyera, wamepona, wengine 5 wamejitenga katika makazi yao ya muda kwenye kitongoji cha Naungo, Kata ya Nanjilinji Wilayani Kilwa”
 
Staa wa soka Simon Msuva kesho Alhamisi anatarajia kuongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam na kuelezea kwa undani kilichotokea kati yake na Timu ya Wydad Casablanca ya Morocco ambayo alivunja nayo mkataba kisha akaishitaki FIFA ambako ameshinda kesi hiyo juzi.

Press Conference ya Msuva ambayo itafichua mengi ambayo Watanzania hawayafahamu pamoja na yale wengi wanayotaka kuyafahamu, itafanyika kwenye hoteli ya Hyatt ukumbi wa Zanzibar Jijini Dar es salaam ambapo Waandishi wote wa habari wanatakiwa kufika kabla ya saa nne na nusu asubuhi.

Juzi Shirikisho la Soka Duniani FIFA liliiagiza Club ya Wydad Casablanca kumlipa Msuva zaidi ya dola za kimarekani laki saba ( Tsh. zaidi ya bilioni 1.6) baada ya Mchezaji huyo kushinda kesi ya madai ya mishahara na signing fee, madai ambayo yalimfanya December 2021 asitishe mkataba wake wa miaka minne.
 
Club ya Simba SC imemtambulisha Mshambuliaji Augustine Okrah (28) Raia wa Ghana aliyekuwa anacheza Bechem United ya Ghana kwa kumpa mkataba wa miaka miwili.

Okrah msimu wa 2021/22 akiwa na Bechem United amefunga goli 14 katika mechi 32 za Ligi Kuu Ghana, huku akifunga goli 3 katika mechi 5 za FA ya Ghana.
 
PICHA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 13, 2022 amekutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar Es Salaam.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewaonya Makada wanaojipitisha kutengeneza safu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao bila ya kufuata utaratibu na kusema Chama kitawachukulia hatua kali, Chongolo amesema Watu hao wamekuwa wanapita kutafuta Wapambe waingie kwenye nafasi ili wawasaidie kwenye malengo yao ya baadae.

Chongolo ametoa onyo hilo leo jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la mafunzo ya uongozi na uwajibikaji kwa viongozi ngazi matawi na mashina wilaya ya Dodoma mjini.

“Kuna baadhi ya Watu wenye ndoto za nafasi nyingine, wako busy kupanga safu, kuna Watu wakimuona Antony Mavunde, Mavunde Simama, huyu ndio Mbunge mpaka 2025 wewe uwe unamwona mfupi, mrefu ndio huyu, huna nafasi ya kumchokoza wala kumwingilia na hiyo ni kwake na Wabunge wote Tanzania na Mimi ndio kazi yangu kuwalinda mpaka 2025 yoyote mwenye nia ya nafasi hiyo asubiri 2025"

“Niwaambie tunawajua, tunawaona, na mnayoyafanya tunayajua na Mimi ni kijana nitakuwa Katibu Mkuu muda mrefu sana poleni mnaofikiria kwamba 2025 nitakuwa sina fursa na nitakuwa siyajui mliyokuwa mkiyafanya, tutadeal na wao kwa kiwango kinachowastahili"
 
Polisi Kigoma wanamshikilia Asafu Lutebuka(30) Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamgeni Wilayani Uvinza kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito Mwanafunzi wake wa darasa la sita Veronica Alphonce (16) ambapo ni kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ramadhan Kingai amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa akimpeleka Mwanafunzi wake nyuma ya kichaka jirani na Shule hiyo kila baada ya masomo ya jioni na kufanya nae mapenzi na kwamba akikataa kesho yake anamchapa viboko.

"Wazazi baada ya kuona Mtoto wao sio kama walivyomzoea walienda kumpima na kugundulika kwamba alikua na mimba ya mwezi mmoja na nusu,na baada ya mahojiano binti huyo alimtaja mwalimu huyo kuwa ndie aliyekua akifanya vitendo hivyo na Mwanafunzi wake"

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma amesema Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu za upelelezi kukamilika.
 
Kijana mmoja (miaka kati ya 25 na 30) Raia wa South Africa ameripotiwa kufariki baada ya kunywa chupa nzima ya pombe aina ya Jägermeister kwa kugugumia chini ya dakika mbili katika shindano la unywaji pombe kupita kiasi huko Waterval, Limpopo Afrika kusini, mitandao ya Nchi hiyo imeripoti.

Kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao kijana huyo anaonekana akiifakamia chupa hiyo huku Watu wakimpigia makofi na kumshangilia ambapo Polisi wa Limpopo wamesema tukio hili limetokea katika kituo cha kuuza pombe za kienyeji ambapo Wateja walishiriki katika shindano la unywaji pombe lililokuwa na zawadi ya Randi 200 ambazo ni sawa na Tsh 27,625.
 
Polisi Mkoani Kigoma wanawashikilia Watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kumbaka Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Tanga mwaka wa kwanza ambaye inaelezwa alibakwa kwa nguvu na Vijana wanne.

Kamanda wa Polisi Kigoma Ramadhani Kingai amesema Mhanga alikamatwa kwa nguvu na kuingizwa ndani kisha kubakwa huku vijana hao wakifungulia redio kwa sauti kubwa.

"Mmoja ya Watuhumiwa aitwaye Bakari Hassani alikula njama na wenzake wengine walivyokaribia kwenye nyumba ambayo anaishi binti huyo walimkamata binti huyo na hatimaye kumuingiza kwenye nyumba waliyomfanyia ubakaji huku wakiwa wamefungulia redio kwa sauti kubwa ili kelele za binti kuomba msaada zisisikike, walipomaliza walikimbia"

RPC Kigoma amewataja Watuhumiwa waliofanya ubakaji huo katika eneo la Mrusi kata ya Heruchuni Wilayani Kasulu kuwa ni Julius Yolemino(24), Hemed miosho (24) na Bakari Hassani(21) na Mtuhumiwa wa nne ambaye anafahamika kwa sura na aliyebakwa na bado anasakwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…