[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Natamani kuwaelewa mnaposema Clatous Chama sio Mchezaji wa mechi kubwa ila swaumu yangu itaonekana si kitu kama nikikubaliana na hilo
Nakubali vipi Mchezaji aliyewalaza Nkana Red Devils, akawaonjesha mpira AS Vita, akacheza kama hatocheza tena dhidi ya JS Saoura kisha miamba ya Afrika Al Ahly, nakubalije juu ya Mchezaji wa Chipolopolo
Natamani tena kuwaelewa kuwa Chama sio mchezaji wa mechi kubwa lakini aliondokaje huyu kwenda Berkane bila kuperform kwenye mechi kubwa za michuano ya Afrika?? Natamani kuwaelewa ila hapana
Natamani kuwaelewa kuwa Chama mnasema sio yule tena, lakini hapana! RS Berkane wakati Chama yupo fit kucheza walienjoy mpira wake mkubwa na kiwango chake kikubwa haikuwa rahisi kumruhusu aondoke
Nafahamu namna Berkane walisumbua, nafahamu namna gani Berkane walipambana ili Chama asalie kwenye timu, nafahamu kwanini Simba walikubali arejee licha ya kutocheza Shirikisho, ilikuwa mapambano ya zaidi ya miezi mitatu
Kuna wakati tusihukumu watu kisa derby! Maana tutahukumu wangapi? Tutakubaliana tukisema Feisal ni wa kawaida!? Kwakuwa hajashine kwenye derby!?? Tutasema Mayele ni wa kawaida kwakuwa derby mbili goaless?
Natamani sana kuwaelewa mnaposema Chama sio mzuri wakati timu inashambuliwa, lakini hapana! Niambieni kama kuna Mchezaji wa aina ya Chama (Ballers) ambao ni wazuri timu ikiwa haina mpira, jibu ni HAPANA
Natamani sana kukubaliana nanyi kuhusu Chama ila hapana, naomba niseme FORM IS TEMPORARY BUT CLASS IS PERMANENT
Nakubali kutokubaliana ni sahihi tu kutokubaliana, tukubali kutokubaliana