Makapuku Forum

• Umewahi kutalii Bagamoyo ? ni moja ya sehemu za Tanzania zenye vivutio vingi na vyenye historia.... moja ya vitu utavyokutana navyo ni Mti huu wa ubuyu unaotajwa kufikisha miaka mia tano na hamsini ambapo Watu mbalimbali huuzunguka ubuyu huu kwa imani kwamba kitendo hicho kitawaongezea umri wa kuishi na inaelezwa kwamba yeyote ataeuzunguka kinyume chake basi atakua amejipunguzia siku za kuishi..........
 
Dar es Salaam. Jaji Joachim Tiganga leo Jumatano Novemba 17, 2021 ameahirisha mara tatu kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu kwa sababu tofauti ikiwemo kuruhusu mawakili wa pande zote kujadiliana.

Awali Jaji Tiganga aliahirisha kesi hiyo kwa muda kwa ajili ya kwenda kukagua kilichomo kwenye diary aliyokutwa nayo shahidi wa Jamhuri kizimbani.

Mara ya pili Jaji alilazimika kuahirisha kesi hiyo ili kuruhusu majadiliano na mawakili wa pande zote juu ya maudhui waliyoyaona kwenye diary hiyo.

Hata hivyo, kesi hiyo itaendelea baada ya majadiliano ya tatu kukamilika
 
Moto kichaa kwenye mashamba ya miti katika wilaya za Mkoa wa Iringa umetajwa kuwa tishio kubwa kwa wawekezaji na wakulima.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu mkoani Iringa, baadhi ya wakulima wa mazao ya misitu na wawekezaji wamesema karibu kila siku kuna msitu unawaka moto huku kukiwa hakuna vifaa vya uzimaji.

Wakati hoja hiyo ikizungumzwa, moto mkubwa umeteketeza zaidi ya heka 100 katika msitu ulio kwenye kata ya Ukumbi wilayani Kilolo.
 
Huenda ukashangaa kuona picha za mwanamke wa kimarekani akiuza maandazi na aina nyingine za vyakula lakini hii ni kawaida, kwa mwanamke huyu anaepatikana maeneo ya Kaunti ya Kisumu Kenya, anayefamika kwa jina la Silvia Bichanga ambaye amekuwa maarufu kwa jina la "mzungu wa maandazi".
 
YANGA kupitia kwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mbata imethibitisha kuwasiliana na Berkane ya Morocco kuangalia uwezekano wa kumsainisha Clatous Chama.

Lakini akaenda mbali zaidi kwa kusisitiza kwamba si Chama tu hata staa yoyote wakimtaka kwenye dirisha dogo wanampata na mkwanja wanao wa kutosha Jangwani.

Staa huyo wa Zambia aliuzwa na Simba kwa Berkane hivikaribuni, huku ikielezwa kuwa kwenye mkataba wake wa miaka mitatu kuna kipengele kinachoibeba Simba. Inaelezwa kuwa Berkane wakitaka kumuuza lazima wawasiliane na Simba kwanza kama wanamtaka au hawamtaki kabla ya kumuuza pengine.
 
Maana ya neno Jigolo ni mwanamume aghalabu kijana anayelipwa fedha na mwanamke aghalabu tajiri mwenye umri mkubwa kupita wake ili kuwa mpenzi wake.
Andika maana yako ya Jigolo
 
Wanamuona mzungu muuza mandazi kumbe mwenzao yupo kwenye special mission kama wale waliyokamatwa hapa Tanzania Moro huko...
 
NCHIMBI: PRESHA YA MASHABIKI IMENIONDOA YANGA
.
Mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi amefunguka sababu za kushindwa kuwa mcharo ndani ya Yanga, ni presha ya mashabiki na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.
.
“Siwezi kutaja ni timu gani hadi sasa zimenifuata, ila baada ya dirisha dogo nitaonekana uwanjani na natarajia kuwa bora zaidi kwani nitapata timu ambayo nitakuwa na uhakika wa kucheza mara kwa mara,” amesema na kuongeza;
.
“Kushindwa kufanya vizuri Yanga haina maana kiwango changu kimeisha, sio kweli nilienda timu yenye presha na kukosa muda wa kucheza mara kwa mara. Nina imani nikipata timu itakayonipa nafasi ya kucheza nitarudi kwenye ushindani,”
.
Nchimbi amesema yupo kwao Tunduru na anafurahia maisha
 
SIMBA: Kwa Chama Tumeshikilia Mpini
.
Mmoja wa viongozi wa Simba jana amefunguk kwamba Yanga wanajifurahisha kwani kwa mujibu wa makubaliano ya Mnyama na Berkane, Chama HAWEZI kuuzwa popote ndani ya miaka mitano ijayo bila Simba kuhusishwa.
.
Kigogo huyo amedai kwamba kama wao watakuwa hawamhitaji Chama ndipo watawaruhusu Berkane kumuuza popote, lakini si ndani ya ardhi ya Tanzania.
.
Lakini ameweka rekodi ni ngumu watani wao kwa sasa kufanya usajili bila wao kujua kwani tayari wana mtu wao pale Jangwani.
 
Billiant atangaza kustaafu Zimbabwe
.
Bishoo na Staa wa Kazier Chiefs, Khama Billiat (31) ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Zimbabwe
.
Billiant ameitumikia timu yake ya taifa mechi zaidi ya 40 na kufunga mabao 17.
 
Farhan Jr

Napitia text ya Profesa hapa! Leo hajanipigia simu ila kaniachia texts tatu WhatsApp maana yupo busy na vikao huko Dodoma!

Prof anasema;

Mwanangu Farhan we all dream to have the team of the Drogbas! Kuna muda watoto wetu wanafanya kila kitu walicho nacho mguuni ila wenzetu kuna muda wanafanya kila kitu kilichopo kichwani

Prof anasema hata Misri walikuwa wanapata wakati mgumu kuelekea world Cup kwakuwa kuna muda hawakuwa na wachezaji wengi Ulaya, walicheza kwa tamaduni za Kiarabu tu ndio maana walitamba AFCON ila World Cup ilikuwa ndoto

Una Ivory Coast yenye wakina Drogba kibao wanatamba Ulaya, wanajua nini kinahitajika kwenye mechi za presha na mpira wa malengo kwakuwa wanapikwa hivyo na vichwa vyao vipo hivyo!

Taifa Stars ni timu nzuri na Vijana wana vipaji vikubwa sana ila wanapaswa kutoka wengi kwenda nje ili kuwa na kitu cha ziada kichwani, ijapo wamepambana sana! Ila still we need to have the team of Drogbas!

Kwenye umri wa miaka 20+ Tayari Kijana Feisal Salum anakuonesha ana kila kitu cha kuondoka ndani ya nchi na safari ya kwenda Magharibi, lakini nani anajali?

Huwezi kuwalaumu Yanga Afrika maana wamempa platform, huwezi kumlaumu Feisal maana tayari ameonesha, tulaumu Agencies za mpira na TFF ni muda wa kubadili set up na kuunda mahusiano mazuri na Kampuni za Mawakala na timu nje ya nchi, iwe rahisi kupata masoko ya vijana

Ifike wakati tuitazame Zanzibar kwa jicho la pili kama ambavyo Ujerumani iliitazama Ruhr Region (Ukanda wa viwanda) kwa jicho la pili, kwenye nchi lazima kuwe na sehemu moja ambayo ni kitovu cha vipaji, Zanzibar naiona hivyo

Kijana wangu nasikia kwenye harambee ilipatikana BILLION 1.6 Yes ndio pesa kama hiyo ipatikane nyingine wakajenge Academy Kigoma, Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Zanzibar, Dar Es Salaam na Pemba

Nchi iwe na Technical centres zake na Academy zake atleast kila Kanda kuwe na Mkoa mmoja wa kimpira, UMISETTA ziwe Kikanda na vipaji vipelekwe maeneo husika, tuanzie chini kwenda juu! Inawezekana maana soka ni biashara kubwa tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…