Makapuku Forum

Makapuku Forum

Screenshot_20211016-050221_Opera%20Mini.jpg
 
Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS limedai kuhusika na shambulizi lililowaua Watu 41 kusini mwa Afghanistan ambapo Washambuliaji wa kujitoa muhanga walishambulia msikiti wa madhehebu ya Shia wakati wa swala ya Ijumaa ambapo zaidi ya Watu 70 walijeruhiwa.

Watu walioshuhudia wamesema walisikia milio ya risasi na milipuko ambapo Askari mmoja aliyekuwa akiulinda msikiti huo amesema wenzake watatu walipigwa risasi wakati Washambuliaji hao walipokuwa wakiingia msikitini kwa nguvu.

Shambulio hili limetokea wiki moja tu baada ya mlipuko mwingine wa bomu uliodaiwa kufanywa pia na tawi la Kundi la Dola la Kiislamu - IS na kuua Watu 46 katika msikiti mmoja kwenye mji wa Kunduz kaskazini mwa Afghanistan.
Screenshot_20211016-141007_Instagram.jpg
 
Mtanzania Kelvin John (18) anayecheza Timu ya vijana ya KRC Genk ya Ubelgiji amezidi kung’aa ndani ya Timu hiyo baada ya jana kufunga magoli mawili kwenye ushindi wa 6-1 vs Standard de Liege katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana Ubelgiji wenye umri chini ya miaka 21 (Pro League U-21)
Screenshot_20211016-141243_Instagram.jpg
 
Polisi wa Uingereza wamesema kitendo cha Mbunge wa Uingereza David Amess kuuwawa jana kwa kuchomwa kisu ni cha kigaidi huku wakisema uchunguzi wa awali umebaini “motisha inayoweza kuhusishwa na msimamo mkali wa Kiislamu.”

Mbunge huyo mhafidhina mwenye umri wa miaka 69 alichomwa kisu akiwa ndani ya kanisa akishauriana na Wapiga kura wa jimbo lake katika kijiji kidogo cha Leigh-on-Sea mji wa Essex, mashariki mwa London.

Polisi kwenye mji wa Essex wamesema wamemkamata Mshukiwa mmoja ambae umri wake ni miaka 25 na wamekipata pia kisu chenyewe, vilevile wamesema kifo hiki ni cha pili tangu mwaka 2016 cha Mwanasiasa kuuawa akikutana na Wapiga kura.
Screenshot_20211016-141338_Instagram.jpg
 
Kwasasa tunafanya mazoezi kwaajili ya kutengeneza miili ya wachezaji lakini pia na kurekebisha pale palipopungua,

lakini hayo yote yanalenga safari kwaajili ya mechi ya marejeano ambayo tunategemea kwenye tarehe 20 tutasafiri kutoka hapa Tanzania kuelekea Libya.

Ukweli usiopingika Al Ahly Tripoli ni wazuri na siyo wazuri tu ila wanajua fitna, na fitna yao ni kubwa sana tofauti na mtu anaweza kufikiri, hayo tunayafahamu vizuri lakini ndomaana tumekuwa na Mwalimu ambaye pia ni mzuri.

Hakuna mtu asiyefahamu Nchi za Kiarabu zinapokuwa Katika mashindano wanapokuwa nyumbani, kwaiyo nidhamu kubwa inahitajika sana kwa timu, nidhamu ya hali ya juu.

Lakini umakini wa kupindukia maana lolote linaweza likatokea kwaiyo tahadhari zote tumezifanyia kazi maana haziji kwa miujiza zinakuja kwa kuzitengeneza na Kwa kujiandaa kwa watu mwisho zikaingia kichwani, kwaiyo kwa hizi siku tano ambazo tutakuwa hapa Dar es salaam, tutakuwa tukitengeneza akili za watu, tabia za watu, mitazamo ya watu lakini na hali halisi ya timu zenyewe tutachezaje tukiwa kule.

Ujue kule hatuendi kucheza, sisi tunaenda kulinda lakini tutafute hata goli moja tu itakuwa afadhali, tulipate mapema itakuwa basi.

Wachezaji wote wako fiti na Watanzania wategemee maendeleo kwani tumekusudia tuendelee Kwani tunataka tuvuke hii hatua na tutaivuka kwasababu, watu wanatutia moyo, watu wana imani na sisi, watu wanatuombea, watu wanatuthamini kwaiyo tunaomba sapoti yao wote katika Dua ili tuweze kusonga mbele kwani siyo sisi tu ni pamoja na Watanzania wote

- Frank Wabare, Afisa Habari Biashara United.
Screenshot_20211016-141827_Instagram.jpg
 
“Kuna muda José Mourinho anakupigia simu na kuuliza unafanya nini sasa hivi, alikuwa akifanya hivyo mara nyingi katika kudumisha mahusiano yake na wachezaji wake” Jesse Lingaard, mchezaji wa Manchester United
Screenshot_20211016-142053_Instagram.jpg
 
“Starehe zipo lakini zisiharibu utaratibu wa kazi na maisha ya kila siku ya mchezaji. Kila jambo liwe na kipimo na kiwango chake.

“Huwezi kujiamulia kufanya mambo kienyeji ukadhani kwamba utafanikiwa, nidhamu ya kazi haswa kwa mchezaji mkubwa mzawa ni kitu cha msingi sana kwavile inamsaidia kujijenga ndani na nje ya uwanja.”
Screenshot_20211016-142648_Instagram.jpg
 
Kocha msaidizi wa Azam, Vivier Bahati katuhakikishia SA kuwa HAWATISHWI na rekodi hiyo ya Pyramids na wamejipanga kuwatupa nje ya mashindano hayo.
Screenshot_20211016-143313_Instagram.jpg
 
AJIB, GADIEL KAMA CHAMBO
.
Simba wajanja sana kimataifa. Kumbe juzi buana walitanguliza wachezaji wanne Botswana kama chambo ili kuwavuruga Jwaneng Galaxy.
.
Jamaa wakajaa wakajua ndiyo imewasili kumbe ndiyo kwaanza majembe yapo Boko yanajinoa.
.
Inaelezwa kwamba Ibrahim Ajib, Gadiel Michael, Ally Salim na Jimmyson Mwanuke walitangulia na viongozi kama kuzuga tu na kuwachanganya wapinzani.
.
Kikosi cha Simba, kimefikia katika hoteli ya Avan iliyopo Gaborone ambayo inasifika kwa utulivu wa hali ya juu, usalama na ufahari ambapo gharama kwa kila chumba ni Dola 110 sawa na Sh250,000.
Screenshot_20211016-143810_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom