Makapuku Forum

"Mwezi April Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Samia ya kuhitaji kukutana naye, Rais Samia amekutana na makundi mbalimbali ila kundi la Wanasiasa bado, tuna imani ya kukutana naye tumweleze mambo yanayosababisha ufa kwenye Taifa hili"

"Nia na lengo letu la kuonana na Rais Samia sio kwenda kumueleza mambo yetu binafsi, bali mambo mbalimbali ya kuendesha Nchi yetu vizuri, na tuko tayari kwa mazungumzo na Rais, lakini hatuko tayari kukutana na Msajili"

"Baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu katiba mpya, tulimwandikia Rais Mstaafu Kikwete barua ya hitaji hilo akakubali kukutana nasi, tukashauriana na mchakato uliishia ulipoishia, alipoingia Rais Magufuli tuliandika barua nne na zote hazikujibiwa"

"Moja ya kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuwasemea watu ambao hawana majukwaa ya kusemea mfano ni machinga na wengine, unapozuia mikutano ya vyama vya siasa maana yake umezua majukwaa ya Watu hao wasiseme na wasiwe na sauti za kusema"——— Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA-Bara
 
"Samia Suluhu Mimi ninakotoka hakuna Makabila, kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo lakini hata kwenye system ya makuzi, Shule na Siasa tunamshukuru Mwl Nyerere ametukuza bila kuangalia Makabila"

"Na mimi hapa siangalii kabila kwenye utendaji kazi wangu, sasa Watu wanafanya makosa ukiwashika ukiwawajibisha wanasema nimewajibishwa kwasababu ya kabila fulani, sina kabila, ukiniuliza kabila lako nani nitakuambia Mzanzibar"

"Hata kwenye utendaji wangu wa kazi sina kabila, uwe Mmakonde uwe mnani ukikosea kwenye kazi mimi na wewe wala sitokufumbia jicho, sasa kama umetoka ulikotoka ukitumbuliwa mimi wa kabila fulani hapana hiyo sumu mnaipeleka sana na naomba isimame, Samia Suluhu sina Kabila Mwl Nyerere alitufundisha kufanya kazi bila kabila"

"Miezi sita ya kipindi hicho tulitumbua wangapi na Mimi nimetumbua wangapi?, Mimi siangalii Kabila, TAMISEMI kwa mfano kuna Watanga wangapi?, Waziri (Ummy ) Mtanga, Katibu Mkuu Mtanga, sijui nani huko Mtanga, nikaletewa nikaambiwa Mama umeweka Watanga watupu nikasema waacheni wafanye kazi wakikoroga nawatumbua”

“Na maeneo mengine hivyohivyo unaletewa ooh Mama hapa hukupanga vizuri kuna huyu na huyu wanatoka eneo moja so what? wana sifa au hawana, wanazo waacheni wafanye kazi wakikosea nitawaondoa sipangi kwa Makabila naangalia uwezo" ——— Rais Samia Suluhu ameyasema haya leo akiwaapisha Viongozi Ikulu Dodoma.
 
"Sitegemei kumuona Mkuu wa Mkoa anaingia kwenye vitendo vya rushwa, sitegemei kuona wakuu wa mikoa mnakuwa waungu watu kule mliko, kazi zenu zina sheria zina miongozo zina kanuni zina kila kitu ambazo mnatakiwa kuzijua vizuri na mzifuate vema, mko kule kutumikia watu sio watu wawatumikie nyie," Rais Samia.
 
Wanaume wametakiwa kutoa taarifa za ukatili na vipigo wanavyopewa kutoka kwa wake zao au jamii inayowazunguka, ili wapate msaada.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Raphia Koshuma alisema hayo juzi katika mafunzo ya wenyeviti na watendaji wa vijiji yaliyotolewa na Shirika la Utetezi wa Haki za Binadamu (Ajiso) kupitia mradi wa Tuwalinde.
 
Bondia Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe ' amesema kwa sasa anapumzika kupanda ulingoni.

Mbabe ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano na Mwananchi Digital ikiwa ni siku moja baada ya kuchapwa na Tshimanga Kantompa wa DR Congo.

Bondia huyo namba mbili nchini kwenye uzani wa super middle amesema amelazimika kujipa muda wa kupumzika ili kujipanga upya.

"Mwakani ndio nafikiria nitarudi ulingoni, ila kwa sasa wacha nipumzike kwanza, nitulize akili, nijipange upya ili niwe na ujio mpya nitakaporejea tena ulingoni," amesema.
 
Hivi sasa mitandaoni kumeshamiri picha za mastaa wakijinasibu kujipunguza au kurekebisha baadhi ya maeneo ya miili yao.

Pia kuna wanaoshindana kutangaza dawa wanazodai zinapunguza miili .Leo nitawapa ufahamu kuhusu njia ambazo si sahihi kiafya kupunguza unene. Moja ni kushinda na njaa muda mrefu huku ukiendelea na kazi za siku. Hii siyo sahihi kwa sababu mwili unahitaji nguvu kwa ajili ya kufanya mambo mbalimbali kama vile kutembea na kufikiri.

Kinachotakiwa hapa ni kupunguza kiasi cha vyakula vinavyonenepesha vikiwamo vyenye sukari, mafuta na wanga nyingi. Kula zaidi wanga yenye mashudu kama vile dona, mchele wa kahawia, mikate ya ngano ya ata na mboga mboga, vyakula vya nyuzi nyuzi na protini ya kwenye mimea ikiwamo ya maharage, kunde na njegere.

Mbili, kufanya mazoezi kupita kiasi, Shirika la Afya duniani(WHO) linashauri kiafya kutumia saa 150 kwa wiki kufanya mazoezi mepesi kama vile kukimbia. Muda huu ni sawa na dakika 30 kwa siku katika siku 5 za wiki.
 
Agizo la kijinga kabisa hili.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imeahirisha hukumu ya kesi ya madai ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba hadi Oktoba 28, 2021 kutokana na kutokamilika kwa maandalizi ya hukumu hiyo.

Hukumu hiyo ya kesi namba 220 ya mwaka 2018 ilitarajiwa kutolewa na Jaji De Melo ambapo Membe alimshitaki Musiba na kumdai fidia ya Shilingi Bilioni 10 kwa tuhuma za kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.

Wakili wa Membe, Shundi Mrutu ameieleza millardayo kwamba hukumu itatolewa Oktoba 28, 2021 "Tumeambiwa maandalizi ya hukumu hayajakamilika”
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Isdor Mpango asubuhi hii ya Oktoba 12, 2021 ameondoka Dar es Salaam kwa treni ya TAZARA kwenda Mkoani Morogoro ambako anatembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la Julius Nyerere katika Mto Rufiji akiongozana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango.
 
1.Jermell Charlo-BINGWA WBO/IBF DUNIA
..
2.Brian Carlos-BINGWA WBC/WBA DUNIA
..
3.Magomed Kurbanov-BINGWA WBO INTERNATIONAL
..
4.Tim Tszyu-BINGWA WBO GLOBAL
..
5.Liam Smith-BINGWA WBA INTERNATIONAL
..
6.Erickson Lubin-BINGWA WBC SILVER
..
7.Brandon Adams-BINGWA WBC AMERIKA
..
8.Carlos Adames-ALIYEKUWA BINGWA WBO INTERIM
..
9.Terrell Gausha-ALIYEKUWA BINGWA WBC SILVER
..
10.Hassan Mwakinyo-BINGWA ABU/WBC AFRIKA.
..
TUANZE NA NANI HAPA..[emoji1]
 
Kwa sasa kwenye soka la wanawake tuna hatua nzuri kwa sababu tayari kuna ‘pipe line’ kuanzia soka la vijana U17, U20 na Senior kwa hiyo unaona mpira ni uwekezaji.

Kwa timu za wanaume hili daraja hakuna kutoka timu za vijana kwenda timu ya wakubwa. Mchezaji akipita timu ya vijana huko mbele atapambana mwenyewe kuingia timu ya wakubwa. Upande wa wanawake kuna daraja la wachezaji kupita, mchezaji anacheza U17 baadaye U20 halafu timu ya wakubwa.

Kuna wakati mchezaji wa U17 anacheza timu zote, ikiitwa timu ya U20 unamkuta na wakati mwingine anaitwa timu ya wakubwa ili kupata uzoefu hata kama hachezi lakini kuangalia tu inamsaidia.

Inawezekana wanachokitumia walimu kwenye timu za vijana za soka la wanawake ndio kinatumiwa hadi timu ya wakubwa kwa hiyo mchezaji hawi mgeni na mbinu zinazotumika kwenye timu hizo. Na hiyo ndio faida ya kuwa na benchi la ufundi linaloingia kwenye timu tofauti za Taifa.

Lakini unaweza kukuta timu za wanaume ni tofauti, kila watu wana namna ambavyo wanafanya kazi. Tunatakiwa kuwa na mfumo mmoja kuanzia chini hadi juu.

- Amri Kiemba akijibu swali la Alex Luambano kuhusu soka la wanawake
 
Mchezaji kama Feisal Salum ‘Fei Toto’ ana njia ndefu, anaweza kucheza ligi yoyote mimi kama kocha nimemuangalia ni kijana ambaye kama atakuwa ‘serious’ atafika mbali.

Mchezaji mwingine ni Meshack Ibrahim (Kgera Sugar) ni mchezaji mzuri pia anaweza kucheza ligi yoyote halafu ni kijana ambaye yupo kwenye mchakato wa kujifunza na anafurahia.

Mimi napenda vijana ambao ni wasikivu na wanapenda kujifunza hawaoni wanajua kilakitu. Mwingine ni Mwijage huyu ni kijana wangu mdogo namuona mbali baadaye na ana maisha marefu kwenye soka.

- Francis Baraza, Kocha Mkuu Kagera Sugar.
 
SILAHA YA @nover_d_40 NI NIDHAMU

Francis Baraza anajivunia kiungo wa kimataifa wa Tanzania Novatus Dismas ambaye kwa sasa anafanya vizuri, Baraza amesema nidhamu ndio kitu kimemfikisha hapo alipo.

“Wakati naingia Biashara United Novatus alikuwa anataka kuondoka, nikaambiwa sababu ilikuwa ni kukosa nafasi ya kucheza. Nikaongeanae kwa kirefu (tukiwa wawili) nikamwambia abaki.”

“Ni mchezaji mzuri mwenye nidhamu, mchezaji yeyote nidhamu ikiwa juu anaweza kucheza popote. Tanzania kuna vipaji lakini wengi hawajitambui.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…