Wengi wetu tunafahamu kwamba miongoni mwa waliotangaza nia za kugombea Urais Nchini Ufilipino wakati huu ni pamoja na Bingwa wa mchezo wa ngumi duniani Manny Pacquiao ambae leo amewasilisha fomu za kuthibitsha kuwania urais wa Ufilipino na kuwa mwanasiasa wa kwanza kutangaza rasmi kwamba atagombea nafasi hiyo ya juu kabisa kwenye uchaguzi utakaofanyika mwakani.
Wengi wanatamani kufahamu ni vitu gani au ni vipaumbele gani alivyonavyo Pacquiao iwapo atashinda kiti cha Urais........ anasema vita yake ya kwanza itakua ni kuushinda wa Wananchi, kupigana na ufisadi na kushughulikia janga la COVID 19, kuimarisha huduma za intaneti na kushusha gharama za umeme Nchini humo.
Ingawa Pacquiao ni Mwanachama wa Chama tawala cha PDP-Laban kinachoongozwa na Rais Rodrigo Duterte, Pacquiao atagombea kupitia Chama chake cha People's Champ Movement kufuatia mvutano baina yake na Duterte ambaye muungano wake umeweka nia ya kumsimamisha Mgombea mwingine.