Kwa taarifa yako Makapuku family:
Marafiki walichanganya bangi na majivu ya Tupac na kuvuta
MSANII wa muziki wa Hip hop Tupac Shakur aliyepata umaarufu mkubwa duniani na kupoteza maisha kwa kupigwa risasi katika ugomvi uliohusisha kurushiana risasi mwaka 1996 nchini Marekani katika jiji la Las Vegas, alikumbukwa na kundi aliloanzisha la Outlawz kwa kuchanganya majivu ya mwili wake na bangi na kisha kuvuta kama sigara.
Katika mahojiano na televisheni ya VladTV, kundi la The Outlawz walithibitisha uzushi uliokuwa ukisambaa kuwa kundi hilo lilichanganya majivu ya Tupac na bangi kisha kuvuta “smoked him out” kama heshima yao ya mwisho.
Kwa mujibu wa gazeti la The Independent la nchini Uingereza na
The Outlawz Insist They Smoked Tupac, mmoja wa wasanii wa kundi hilo, Noble, alithibitisha kwa kusema, “Ndio ni kweli kabisa…tulikuwa katika kumbukumbu na familia yake pamoja na mama yake .