Makapuku Forum

Wasanii mbalimbali wa muziki (Tanzania All Stars) walipokuwa wakiimba wimbo wao wa maombolezo ulioandaliwa chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye shughuli ya kuaga kitaifa mwili wa aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli inayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

PumzikaBaba
TutaonanaBaadae
 
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt John Magufuli Mama Janet Magufuli akilia kwa uchungu wakati zoezi la kitaifa la kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa #Magufuli likiendelea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Machi 22, 2021.

RiPMagufuli View attachment 1731653
 
JPM AACHA WATOTO SABA, WAJUKUU 10

"Kuhusu familia Hayati John MAGUFULI alifunga Ndoa Takatifu mwaka 1989 na Mama Janeth Matias (Magufuli) mpaka mauti yanamfika ameacha Mjane na watoto Saba (Suzana, Edna, Joseph, Jesca, Ruth, Jurgen na Jeremiah) pamoja na wajukuu 10" Profesa Palamagamba John Kabudi.

KutokaDodoma
PumzikaBaba
 
UGONJWA WA MOYO ULIMSUMBUA KWA MIAKA 10

"Hayati John MAGUFULI alifariki kwa ugonjwa wa moyo "matatizo ya mfumo wa umeme" tarehe 17 Machi 2021 majira ya Saa 12 jioni akiwa na miaka 61 ugonjwa huu umemsumbua kwa zaidi ya miaka 10" Profesa Palamagamba John Kabudi.

KutokaDodoma
PumzikaBaba
 
Hivi hata picha zao zipo kweli??
 
Jesca ndiyo anajulikana sana...
 
“Nina masikitiko makubwa yaliyojaa uzuni kwa kuondokewa na ndugu na rafiki yangu Magufuli. Msiba huu ni mzito, hauwagusi watanzania pekee yake, kupotea na kuondoka kwa Dk Magufuli kumetingisha Bara la Afrika ." Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi

RIPMagufuli
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…