BIOCENTRISM -
@deokitasa -
Hii Nadharia Inaeleza Kuhusu Kufikiri Kuhusu Mawazo Yako Yaani Pindi Unapo Waza Kuhusu Jambo Fulani Unatakiwa Pia Uwaze Kuhusu Yale Mawazo Yako, Kwa Maneno mengine Hata Wewe Mwenyewe Haupaswi Kujiamini, Inaeleza Pia Kuhusu Muda, Nafasi Na Kujielewa -
Nadharia hii Inaeleza kwamba Binadamu Tunaishi Angalia Tayari Tumesha Kufa, Ni Ngumu Kuingia Akilini Eh? Sawa Labla Inawezekana Ndio Kufa Kwenyewe huko.
Kwa mfano Nikikuambia kuwa we hapo ulishakufa tayari utapinga vipi? Hebu jiulize aliyelala na anaota anafukuzwa na simba, Hujitahidi kukimbia ili aokoe maisha yake huku akijua kuwa hayo ndo maisha yake halisi nawala sio ndoto tu. -
Akiamka ndo anajua kuwa kumbe ilikuwa ni ndoto hata asingekimbia asingeuawa na simba wa ndotoni. Hivyo amepambana kwa hasara. yaweza kuwa hata mi kuandika hapa ikawa ni mwendelezo wa ndoto katika kifo changu, Yaani nilishakufa na haya ndo maisha ya kifoni, ndivyo Anavyo maanisha Bwana Robert Lanza Au? -
Au Tuseme vipi! Kwamba Nafasi Na Muda ni vitu ambavyo vinatumiwa na akili yetu ili kutufanya tuhisi huu uwepo lakini ukifa hakuna Muda na kifo hakipo katika Ulimwengu Huo Usio na Muda (timeless world)!? Sisi tunaona mtu amekufa na tumezika, Lakini Biocentrism ina Tuambia uhalisia hauko hivyo. -
Bila shaka swali lako kubwa ni kwanini? Maisha Yetu Ni mfululizo
Wa Ndoto Isiyo Kamilika /Timia Ni Ndoto yenye Episode nyingi sana Tunazo zitegemea kuziona zinatokea na Tusizo tegemea Zina tokea tu pasina kukusudia na kwa Nafasi.
Bado Hauja Elewa? Tusichoshane, Ina wezekana Mimi ninaye andika Na Wewe Unaye soma Tupo kwenye Biocentrism (Wafu Tulio Hai) hivyo ni vigumu kuelewana. -
Mawazo Yangu Ya Mwisho Kabisa Yananileta Hapa, Kutokana na mambo mbalimbali Tunayo kutana nayo Sisi kama binadamu Ndiyo yanayo Tufanya kuwa watu Tulio hali kwa mfano Misongo Ya Mawazo, Magonjwa, Furaha Iliyo Pitiliza, Mishituko nk Una Fahamu kuwa Roho zetu zina piga sana misele? -
Ukitaka kuthibitisha hilo Jiulize kwanini Kuna Bilocation, Aura Reading, Death Warning, Apportation, Precognation, Cognation Dreams, Remote viewing, Retrocognation, Scrying, presque vu, Déjà Entendu, Jamais vu na Déjà vu? Lakini Roho Haifi. -
MWISHO