Makapuku Forum

The Role of New and Social Media in Tanzanian Hip-Hop Production ni utafiti (survey) iliyofanywa na Msia Kibona Clark na ilionesha kuwa kati ya mwaka 2013/14 mwanamuziki FidQ aliongoza kwa kutumia mtandao (new media) kuwasilisha kazi zake.

Ni utafiti mzuri kuusoma, unaweza kuupata kwenye Google scholar
 
Moja ya wimbo ninaokubali sanaaa!

...nami huwa siuchoki kuusikiliza, nimekulia enzi za kina Gangwe Mobb na WWA (Weusi Wagumu Asilia) na bado naamini Jide ni mwanamuziki bora kabisa-kiushairi na kuwasilisha ujumbe wa muziki kwa hisia
 
Msomi wa UDSM Felician Tungaraza mwaka 1993 aliandika chapisho lake la kisera na kuonesha kuwa vikundi vya kijamii (social networks) vimesaidia sana katika kusaidia kukwamuana miongoni mwa watu wanaofahamiana. Chapisho lake linaitwa social network and Social Care in Tanzania na lilichapwa katika machapisho ya taasisi iitwayo Social Policy and Administration nambari ya chapisho ISSN 0144-5596

FYI

Machapisho mengi hupewa namba ISSN (International Standard Serial Number) na ISBN (International Standard Book Number) ni kwa ajili ya vitabu
 
Binamu bwana uwe hata unagoogle bwana

Shimo jeusi ( Kiingereza: black hole ) ni jina kwa eneo kwenye anga la ulimwengu lenye graviti kubwa kiasi kwamba hata nuru haiwezi kutoka nje yake.

Nadharia ya uhusianifu inatabiri ya kwamba gimba lenye masi kubwa iliyokandamizwa katika eneo dogo litasababisha "shimo jeusi". Eneo hili lazungukwa na upeo usioonekana lakini mipaka ya upeo huu ni kama mstari ambao kila kitu kinachoupita hakiwezi kurudi tena kwa sababu kinavutwa mno na graviti ya shimo jeusi.

Eneo hili laitwa "jeusi" kwa sababu nuru yote inayofika upeo huu inamezwa kabisa hakuna inayorudishwa tena.

Kwa hiyo hadi sasa haikuwezekana kutazama shimo jeusi moja kwa moja. Lakini wataalamu wa
fizikia waliwahi kuyatabiri mashimo haya.

Katika miaka ya nyuma astronomia imeangalia mahali pengi ambako mwendo wa nyota za eneo fulani si kawaida unaelezwa kwa kuwepo kwa shimo jeusi katika sehemu hizi maana yake graviti yake inaathiri mwendo wa nyota au mawingu ya gesi ya angani na kuzivutia kwake.

Mwendo huu wa magimba katika mazingira ya mashimo meusi unaonekana kwa wanaastronomia.

Inaaminiwa ya kwamba shimo jeusi linatokea wakati wa kufa kwa nyota kubwa lenye masi inayozidi masi ya jua letu mara tatu au zaidi.
 
Reactions: Obe
...nami huwa siuchoki kuusikiliza, nimekulia enzi za kina Gangwe Mobb na WWA (Weusi Wagumu Asilia) na bado naamini Jide ni mwanamuziki bora kabisa-kiushairi na kuwasilisha ujumbe wa muziki kwa hisia
Kumbe binamu we mdogo hivi khaaaa
 
Reactions: Obe

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…