[emoji524]TUOMBE:
Baba yetu Mtakatifu Mungu uketiye mahali pa siri tunaliinua jina lako Takatifu Asante kutuamsha salama leo IJUMAS Tarehe 12 Oktoba 2018 tukiwa salama na Afya njema ..Asante kwa neema na rehema tele Baba Asante kwa familia ndugu jamaa na marafiki wote asante kwa huduma njema katika maisha yetu.Tunaomba toba kwa makosa yote tunayotenda kwa mawazo,maneno, matendo Uturehenu twakusihi .Tunajikabidhi mikononi mwako tutakase Baba tuwe barua njema kwa wengine watusome vyena.Tupe moyo wa unyenyekevu na msaada kwa wengine tujaze upendo usio na mwisho.Bariki kazi za mikono yetu..Endelea kutuponya Baba,endelea kubariki mashamba,mifugo na shughuli zote zituzalie matunda mema.
Tunaomba siku ya leo ikawe njema na kukupendeza ...tujaze shukurani kwa kila tunalopitia tukuone wewe.
Bariki wasafiri nchi kavu,majini,angani waende na kurudi salama.wabariki watoto na wajukuu wawe salama epusha utekaji ambao unaleta hofu kwa kila mmoja wetu tulinde miili na roho zetu.imarisha amani na mshikamno ili popote tulipo pawe mahali pema na salama pa kuishi.Roho Mtakatifu kaa nasi daima.Tunaomba yote katika jina la Yesu Kristo Amen
IJUMAA NJEMA YA BARAKA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE[emoji257][emoji257]