Makapuku Forum


Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amekana kwamba amekosana na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, lakini anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anahitaji kucheza maeneo tofauti katika klabu hiyo.. (Guardian)
 

Manchester United haijakiubaliana kuhusu mkataba mpya wa kumzuia mshambuliaji wake Anthony Martial ,22, kuondoka katika uwanja wa Old Trafford , huku raia huyo wa Ufaransa akiendelea na mazungumzo na klabu hiyo.(Goal)
 
Everton imekataa dau la muda wa mwisho la £25m kutoka RB Leipzig kumnunua mshambuliaji Ademola Lookman, 20, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka kumnunua raia huyo wa Uingereza kurudi katika uwanja wa Red Bull Arena. (90min)
 

Jurgen Klopp amemuonya kipa wa Liverpool Simon Mignolet, 30, kuwa tayari kuchezeshwa baada ya kipa mpya Alisson. Raia huyo wa Ubelgiji sasa atachezeshwa baada ya kipa Alisson. (Mirror)
 
Mmiliki wa Watford Gino Pozzo amekataa dau la £125m kuuza asilimia 35 ya klabu hiyo kwa Prolific Media Holdings, ambayo imekita kambi mjini New York. (Times - subscription required)
 
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa hatojaribu kuwashawishi watu kusalia ambao hawataki kusalia akiongezea kwamba sio tatizo iwapo klabu hiyo itapoteza wachezaji wawili au watatu kwa kuwa klabu hiyo ina wachezaji chungu nzima katika taasisi yao ya mafunzo ya soka.(Telegraph)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…