Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Jenga Bahari Kwenye Mto

Wengi wetu tunaijua bahari kwa namna tofauti, kwa kuiona au kuisikia. Vyovyote vile, bahari inabaki kuwa ni umbo kubwa ambalo ukomo wake hauelezeki kwa maneno ukatosha. Usemi kuwa bahari haina mwisho unaelezea ukubwa na kina cha bahari ambayo inabeba meli, ngalawa, mashua, manowali na taja chochote kinachosafiri majini. Bahari hupwa na kujaa. Bahari ni kubwa tofauti na mto ambao huwa ni mdogo na maji yake yanatembea, hayajatuama kama maji ya ziwani. Inawezekana hujaelewa nataka kuwasilisha nini jioni hii lakini unaruhusiwa kutafasiri unavyoweza.

Katika maisha wengi wetu tumekuwa tukiota ndoto kubwa, tunawaza makubwa tuyapate (dream big) na tunasahau kabisa kuwa makubwa mengi tunayowaza hatuko nayo karibu, yako mbali. Bahati mbaya sana wakati tunawaza na kuota makubwa, tunashindwa kuheshimu ndoto ndogo tulizoshikilia mkononi. Na kutokana kuwaza makubwa tusiyoweza kufikia basi tunajikuta tunaendekeza njia za mikato na kujiingiza kwenye rushwa na kharam nyingine nyingi.

Kwa taarifa yako tu, maji ya mto hayatuami, hutembea muda wote na kumwaga maji yake baharini, ukubwa wa bahari usikufanye ukadharau umuhimu wa mto. Shikilia kidogo ulichonacho, kifanyie kazi kiusahihi na kitakupa mambo makubwa. Tafasiri Unavyoweza
 
Asante binamu barikiwa
 
katika ubora wako kapuku mwenzangu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom