Niwatakie mandalizi ya ijumaa kuu pamoja na pasaka njema
Tutafakari njia zake
Natuenende kwa kufuata matendo ya tunae adhimisha siku yake leo
Mdau...asante sana mdau wa ukweli. Hivi ijumaa kuu ndo hatuli nyama eeeeh, ila kunywa inaruhusiwa? Nauliza tu ili nisije nikaingia majaribuni mapema kabla ya siku yenyewe
Mdau
haturuhusiwi kura nyama
Kula kama hukufunga unaruhusiwa kama ulifunga unaendelea na ratiba ya kufunga mpaka pasaka yenyewe
Kunywa unaruhusiwa ila sio vilevi
Kama ijumaa anaona inamsumbua aikaushie aendelee kama alivyo zoea maana mambo ya imani yanahitaji ujikane mwenyewe...duh, hapa anko wangu atapata asazi (ulcers)
HapanaTranscend ndiye kaanza wewe umemalizia
Hivi alikuja?
Teh teh teh...Binamu Obe nakuona unanikwepa kwepa ila sawa mimi napambana na kazi yetu tumalize usajili wa kampuni yetu japo kwenye masharti naona wanasumbua tupunguze kidogo ila tutafanikiwa kwa hiyo waache wale wanaoweka vitu bondii sisi magar ,sijui hatutakii wanaume waache waweke bondi wanawake wao kwenye kampuni yetu
[emoji113] [emoji113][emoji112] [emoji112] [emoji112]
Obe binamu bhanaaaah sasa ulitaka nifunge zote kweliii we mwenyewe ulianza ukachemka kama mm leo nimejikuta nasahau kuwa nyama leo sio vizuri kula na mimi ndo maana niliamua supu nipewe mchuzii tu ....
Binamu nimeona nyayo zako lakin unajua leo nimepewa kitengo cha mapokezi ya bombadiaaaa yetuuu ...najua unajuaaa
Asante kwa mziki
Binamu asante nakutakia maandalizi mema ya pasakaMuziki wa Mdhamini: Ijumaa Kuu
Ninadhamini kipengele hiki mwenyewe na ninakutakia Ijumaa kuu njema wewe BlessedHope , Shunie , Tumosa , ABJ , Clkey , demi , Valentina , husna muba , Lyon Lee , Nyagei , Transcend , Mndali ndanyelakakomu , dumejeuri , SHIMBA YA BUYENZE , mzeewakungoa , makaveli10 , Mwifwa na wewe Kapuku unayefurahia siku ya leo na weekend yote kwa ujumla wake wa Pasaka
Binamu asante nakutakia maandalizi mema ya pasaka
DaahHapana
Shemeji[emoji113] [emoji113]
Jana niliomba kibao cha Yoriyori vipi mitambo haiko sawa mtaasisi?Muziki: Ijumaa Kuu Bila Ukuukuu
....ninakuandikia Kapuku mheshimika nikijiaminisha kabisa umekuwa na wakati mzuri tangu Jumatatu ilipoanza na leo ni Ijumaa (TGIF). Ila ujue Ijumaa hii ya leo iko tofauti kidogo na ijumaa nyingine, hii inaitwa Ijumaa Kuu kwa sababu ndo Wakristo (wafuasi wa Kristo Yesu) wanakumbuka kufa, yaani mpaka muda huu, Yuda keshachukua mlungula (possibly akaenda kujirusha maana tayari ana vipande thelathini) na yule majeruhi Malchus aliyekatwa sikio na Simon Petro sasa hivi anaganga sikio lake. Psaka ina mengi na yote ni kutukumbusha kuoshwa kwa dhambi na kuanza upya.
Nimeongea na anko Lyon Lee leo kaamua kufunga, yaani katika siku 40 wengine tunakomaa kufunga yeye anafung siku ya mwisho eti kisa ni kwa kuwa anayecheka mwisho ndo anacheka sana. Akili za mjomba anazijua mwenyewe na mimi sina lolotela kufanya maana haya ni mambo ya ukoo.
Muziki sasa, nikutakie wakati mzuri leo na malalamiko ya Side muuza mishkaki karibu na kanisa ni ya kujitakia maana leo wateja wengi hawagusi vitu vya damu, wanatembea na damu, hawali nyama labda atengeneze mishkaki ya maharage na matembele. Ijumaa Kuu Njema