Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Jtatu Kuelekea Pasaka

Nikutakie maandalizi mazuri ya Pasaka maana ndo tuumelianza juma la Pasaka na kwa maana hiyo salamu yangu kwangu na 'wishes' zote za kujiandaa vema ndo zinahusika hapa.

Nakusalimia Lyon Lee najua unapiganisha juu na chini uvuke mipaka utuachie mimbwa yetu ya pale ghorofa la wasakakodi. All the best.

Muziki sasa, natumaini ulikuwa na wikend njema.

Shikamoo binamu
 
Tafasiri Unavyoweza: Waraka Uimbwe, Anayeandikiwa Hajui Kusoma

Tunaelekea kwenye Pasaka, siku inayoambatana na sherehe kubwa kabisa kwa waumini wanaoamini katika kufa na kufufuka kwa Masihi, Yesu. Ni juma la kujitafakari na ikiwezekana kuanza upya na ndiyo maana madhabahuni wale wote walioaminiwa kuchunga 'kondoo' wanatuasa kwa kutoa matamko ya kutuongoza 'kufufka' upya. Matamko haya kwa njia ya waraka yanawatenga wasomi wasiopenda kusoma na kwa kutopenda kwao kusoma wamegeuka wajinga (ujinga ni kutokujua kusoma na kuandika). Na bahati mbaya wajinga wengi ndo wanaongoza taasisi tulizokubaliana kutoa uhuru wetu tuishi kama watu makini. Tafasiri Unavyoweza.

Mada ngumu hii, waraka hauna mchezo, unakuja na moto, waraka umekaa kama upanga ukatao kuwili na mpini ni wa moto, hauangalii unachokata na aliyeshika wote mnahusika na msipousikiliza mtaungua. Nimesoma waraka wa Pasaka, unavutia kusoma lakini je wote wahusika wanaotakiwa kuusoma wanausoma au ndo watabaki kusema kama msemaji wa serikali ambaye yeye kakiri hajausoma na ameulizwa ajibu kuhusu waraka akaishia kusema anawatakia Pasaka njema. Jibu la msomi asiyependa kusoma na ndo tunao wengi wa aina hii, PhD ni aina nyingine ya 'probably headed for divorce'. Tafasiri Unavyoweza

Kwa namna watawala wetu walivyojitanabaisha kuwa aina ya watawala wasio na uwezo wa kujibu hoja na kutumia mabavu (rejea kulazimisha kumkamata mchungaji kule kanda ya kaskazini, sheick Ponda na wengineo) kujibu hoja basi waraka huu wasipewe wasome, hawajui kusoma waraka na kwa hiyo tuwasaidie kwa kuuimba, kuuchezea michezo ya jukwaani (pushups hazihusiki ila kurusha miguu kwa mtindo wa mapanga shaa unaruhusiwa). Ikiwezekana tuandamane huku tukiuimba waraka huu maana tulisoma sisi wakafaulu wao na wakitupiga au kutuua rambirambi watazila wao. Ndo kawaida ya kiongozi mlafi. Tafasiri unavyoweza
 
Nko byeee kbsa
a6f8da146a654ffa519ae5757a4a0471.gif
 
Muziki: Jtatu Kuelekea Pasaka

Nikutakie maandalizi mazuri ya Pasaka maana ndo tuumelianza juma la Pasaka na kwa maana hiyo salamu yangu kwangu na 'wishes' zote za kujiandaa vema ndo zinahusika hapa.

Nakusalimia Lyon Lee najua unapiganisha juu na chini uvuke mipaka utuachie mimbwa yetu ya pale ghorofa la wasakakodi. All the best.

Muziki sasa, natumaini ulikuwa na wikend njema.

Mopao mokonzi.
 
Back
Top Bottom