Mambo kama uyajuavyooo nipo upajuapo sema kuna ka giza shawishiiiii..nashukuru mjomba, mambo yanaendaje lakini?
Mambo kama uyajuavyooo nipo upajuapo sema kuna ka giza shawishiiiii
Uko poa binamu ?? Nina salamuu kutoka lushoto kama sio mbeya
Sasa unabishana na mimi binamuuuu...sio mbeya, ni Lushoto nina uhakika na najua ulifaidi
HAPPY WOMENS DAY View attachment 707641
[emoji123] [emoji123] [emoji123] [emoji123] [emoji126] [emoji126]Asante mdau kwa kutupia kumbukumbu hii humu.
Hongera kwa wanawake wote wa Makapuku Forum, nyie ni mashujaa (sheroes) na mnalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo
[emoji15] [emoji15]
Shikamoo[emoji120] [emoji120]Mr obe naomba wimbo wa sweet mother!!! Sijui kaimba nani hata
Mr obe naomba wimbo wa sweet mother!!! Sijui kaimba nani hata
Unataka ninyima nini mieShikamoo[emoji120] [emoji120]
Asante Mr obe...wimbo wa zamani sana na haujaisha utamu,ulichezwa mwaka 1974 nimezaliwa nimeukuta ukiwa na miaka kumi radioni uliimbwa na Nico Mbarga (sio Nico Zengekala aliyeimba Solemba), huyu alikuwa ni Mkameroon upande wa baba na mama Mnigeria.
Nitaucheza
Asante sanaMuziki: Umeumbwa na Bahati
...hakuna namna na ni lazima niseme, kama kuna siku ambazo nimewahi kumuona anko wangu Lyon Lee akiwa mpole, kajituliza na aunt yangu basi ni jioni ya leo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kimataifa. walinikaribisha kama mgeni mwenyeji. Nikusalimie Kapuku wewe na kukutakia wakati mzuri tunapoenda kuikamilisha siku ya wanawake kimataifa.
Kuna changamoto nyingi zinapitiwa na wanawake katika kufikia usawa wa kijinsia katika maeneo mbalimbali iwe ndani ya nyumba, ofisini na kwenye jamii nzima. tunajua kwa namna gani wanawake wanakuwa na wakati mgumu kujikomboa kiuchumi, kielimu, kiutamaduni na kimaamuzi.
Nitaongelea kiutamaduni ambapo inafikia wakati mwanamke anakuwa hana uhuru wa kuamua avae nini, yaani mwili wake halafu wanaume ndo wanampoangia cha kuvaa na mjoma wangu asipobadilika kwenye kumpangia mavazi aunt yangu basi wote tumkataze kukaa anageukageuka nyuma akipishana na wanawake waliopendeza kwa mavazi wanayoyapenda wao.
Muziki sasa, niliwataja wanawake wote wa MF kwenye kipengele cha Tafasiri Unavyoweza, ninyi mnatupa sababu ya kuwa na tabasamu humu ndani
BarikiwaMuziki wa Mdhamini: Mama Yangu Ni Mwanamke
...ni bahati iliyoje nikikupa siri ambaye inawezekana ulikuwa huijui. Ninakuambia kwa sababu wewe ni nmtu mzuri na kila wakati unanipa sababu ya mimi kuja hapa makapuku Forum na kufurahia, siri yenyewe ni ndogo sana, niliitunza siku nyingi ila leo nitakuambie na ukiweza katangaze wengine wajue kuwa mama yangu ni mwanamke.
Tufurahie muziki wa mdhamini Sakayo ambaye anataka tufurahi pamoja naye, hakusema anaudedicate kwa nani lakini kwani kuna ubaya kufurahia muziki unaochezwa kwa jirani?
Nitaweka clip mbili za wimbo mmoja, mmoja ni 'original version' na nyingine ni umeimbwa upya 'remix'
Originale
Remix