Muziki Wikend: A Lady In Red
Jumamosi ya zamani, si unalijua hili Kapuku muheshimika ambaye bila kupoteza wakati ninakusalimia nikiwa na tabasamu kabisa. tabasamu langu lina sababu mbili kubwa, kwanza leo ni wikend na nimetoka kuungana na maveterani wenzangu kufanya mazoezi na baada ya mazoezi tukaenda kugonga supu na bia. Huwa nawashangaa wanaotushangaa kuwa tunafanya mazoezi au tunasaka hamu ya bia, mbona wao wakimaliza wanaenda kula chapati mbili na chai? Tuendelee kushangaana tu, maana hatuvunji sheria.
Sababu ya pili ya tabasamu langu ni kwa sababu wewe, yeah, you Kapuku uko hapa. Ujue kuwepo kwako hapa kunalifanya jukwaa hili kuwa la kipekee sana na linavutia sababu tu wewe una mvuto, ulimbo, sumaku na zaidi unajua mengi japo huchoki kujifunza. Karibu sana
moneytalk , hapa utafurahia, utapata maarifa, burudani na utani. tunajua kabisa umekuja na vitu adimu kulifanya jukwaa hili kuwa poa. na hata kama umekuja kupita tu, sio kesi maana tunakufurahia.
Muziki sasa, sio tu unamuona mdada au mmama kapendeza na nguo yake nyekundu unaanza mawazo yako ya kichawi ooh mganga wa mvua au ana majini. Nguo nyekundu humtoa bomba sana mwanamke anayeivaa kistaha yaani unaruhusiwa kumuita bombadia. Sasa na vidume nao wakivaa red ndo utashangaa hujafika mtaa wa tano tu radi zinakuvurumsha. Hongera sana kwa wadada mnaovaa red.