Makapuku Forum

Katika dondoo za bbc. ..



[emoji117] Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya NASA wapinga mahakamani ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta, kesi yao kuanza kusikilizwa leo

[emoji117] Watu takriban elfu 2 wameokolewa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi katikja mji wa Houston baada ya kimbunga kinachofahamika kwa jina la Harvey
kuukumba mji huo

[emoji117] Zao la alizeti ni moja kati ya mazao yanayolimwa mkoani Dodoma nchini Tanzania ambapo hutumika kama zao la chakula na biashara.

[emoji117] Serikali ya Kenya imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Kuanzia leo, yeyote atakayepatikana akiitumia, akiiuza ama kuitengeneza atatozwa faini ya dola elfu arobaini ama kifungo cha miaka minne jela

[emoji117] Maafisa wa masuala ya usalama barani Afrika wanakutana nchini Uganda katika mkutano wa tatu kuhusu kikosi maalum cha haraka cha Afrika kinachopambana dhidi ya migogoro

[emoji117] Kwa mara ya kwanza Mwishoni mwa juma, Zanzibar iliandaa msafara wa magari ya zamani ambayo yaliwahi kutumiwa katika miaka ya sitini na hamsini


Hii picha imejipostiiiiiiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…