Makapuku Forum

1/ je wajua mpira mkubwa zaidi uliotengenezwa kwa kutumia rubber band?

Achana na mipira hii ya kawaida tuliowahi kuiona, Joel Waul raia wa United States of America hapa akionekana na mpira alioutengeneza uliovunja rekodi za dunia

Alitumia zaidi ya rubber band 700,000



Mpira huu una uzito wa 4,097 kg (9,032 pounds) ulipimwa huko Launder hill, November 13,2008

Wakati anavunja rekodi hii Joel alikua na umri wa miaka 27



Madame S
 
2/ pata kufaham maajabu ya dunia nami niko hapa kukujuza zaidi, je wamjua mbwa mwenye masikio marefu zaidi duniani

Anaitwa Tigger bloodhound masikio yake yana urefu wa 34.92 cm (13.75 inches) masikio yote mawili kulia na kushoto



Mbwa buyu alikua akimilikiwa na Bw. Bryan pamoja na mkewe Bi. Christina wa huko St Joseph, III



Kwa bahati mbaya mbwa huyu alifariki mwaka 2009 baada ya kuingia rasmi kwenye kitabu maarufu cha orodha duniani "Guiness Book of Records" 29 September 2004

Madame S
 
3/ je wajua pizza kubwa zaidi duniani?




Eneo la mzunguko wa pizza hii ulikua na ukubwa upatao 1,261.65 square meters sawa na (13,580.28 square feets) iliyoandaliwa na Dovillo Nardi, Andrea Mannocchi, Marco Nardi, Mattlo Nardi, na Matteo Giannotte (wote wakiwa wanatokea Italy) sehem inaitwa Fiera Roma huko Rome, Italy

Pizza hii ilioewa jina la "Ottavia" likiwa na maana ya "watoto wa kiume saba"


Pizza hii pia, iliingia rasmi Guinness Book of Records 13 December 2012

Madame S
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…