Makapuku Forum

Bwana wetesi wangu wamezidi kuwa wengi ni wengi wanaonishambulia ni wengi wanaoiambia nafsi yangu hana wokovu huyu kwa Mungu

Na wewe Bwana u ngao yangu pande zote utukufu na mwinua kichwa changu

Kwa sauti yangu namwita Bwana naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu

nalijilaza nikalala usingizi nikaamka kwa kuwa Bwana ananitegemeza

Sitayaogopa makumi elfu ya watu waliojipanga juu yangu pande zote

Bwana uinuke Mungu wangu uniokoe manaa umewapiga taya adui zangu wote, umewavunja meno wasio haki

Wokovu una Bwana Baraka yako na iwe juu ya watu wako

ZABURI 3:1:8
Muwe na usiku mwema damu ya Yesu iwalinde usiku wote
 
Asante my dear shunie lee
 
Makapuku haijawahi kuwa na bahati mbaya, hilo la kwanza. Uwepo wake tu hapa kama ilivyo mimi, wewe, yule na hata anayesoma unalifanya jukwaa hili kuwa zuri na la kipekee na ni bahati mbaya sana kwa ambaye hatembelei hapa😀
Umeongea vyema hope kiroba bado hujaongezeaa kutoka mafichoni

Muhimu kwanza tuheshimu chetu/vyetu kwanza ....
 


Amen mtumishi mpya! Ubarikiwe kama tunavyobarikiwa
 
DARASA HURU LA KAPUKU. .(DHK)

Hujambo kapuku mpendwa ni usku mwingine kupitia jukwaa letu pendwa na kuheshimu ombi la mwekahazina kisheti Nyagei tuone hili tatizo la Endometriosis. ..

Karibia mda wako mi thamani tosha ...

Endometriosis ni hali inayotokea ambapo tissue za ndani ya ukuta wa mfuko wa uzazi yaani uterus kujitokeza nje nikimanisha zinakuwa kwa nje katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. ..hapa namaanisha ndani ya uterus mpaka fallopian tube ...sio ugonjwa ni just disoders na inatokea kwa sababu mbalimbali japo kuna nadharia nyingi ...

.....Hii hali inasababisha maumivu makali katika tumbo la mwanamke hasa kipindi cha siku zao au kipindi wanafanya tendo la ndoa ...

Kiukwelii hii hali ni muhimu kuwa makini nayo kwani impacts zake ni kibwa hili jambo lisipochukuliwa hatua na mbaya zaidii kila mwezi mwanamke anapoingia hedhi /menstruation hizi sehemu kwa nje nazo huwa zinavunjikavunjika na kuwa katika mzunguko hapa ndo maumivu yanapokuwa makalii na mzunguko wa siku unakuwa sio wa kawaidaa...


Hili hii hali wengi huwa wanaichanganya na cancer jambo ambalo sio kwelii make japokuwa kunakuwa kama kuna uvimbe kwa nje ya uterus , ovary na fallopiana tube

Muhimu hii hali unaweza ukaigundua mapema hapa ndo wakina mama umuhimu wa kuongea na watoto wao ata wewe mdau wa kiume ni vizuri ukashare baadhi ya mambo na mtoto wa kike japo kimaadili tutasema tuwaachie wakina mama ..ok shunie ...tumosa na wote wa hapa kazi kwenu make vipo viashilia vinavyoweza kuonesha dalili za hii hali mfano .
...maumivu makali wakatiwa tendo la ndoa

....kuingia kwa siku nyingi kwenye hedhi kuliko kawaida ...ni baadhi ya mambo muhimu ya kuwa makini nayo...

CHANZO CHA HII HALI...

Kiukwelii wanasayansi bado wanaumiza kichwa kujua chanzo cha hii hali ni nini make zipo nadharia mbalimbali ambazo wengi wanadai kuwa ndo chanzo ...

Mfano ....kuna wanaoamini katika baadhi ya nadharia kama implantation theory ambayo wengi wanadai kuwa baadhi ya chembe hasa zile zinazoitwa endometrium ambazo ndo zinapatikana katika ukuta wa mfuko wa uzazi hasa kipindi cha hedhi zinaweza kutoka kuptia kupitia katika mirija ya falopiani na kwenda kujishikisha nje ya kuta za baadhi ya sehemu katika mwili jambo ambalo linapekea hizi tissue kukua na kusababisha hii hali...

Wengine wanaamini kuwa hii hali inaweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine japo ni nadharia na hii theory ina maswali yasiyojibika ...make hii hali inatokea hasa msichana anapovunja ungo....

Wengine wanaamini katika hii concept ya metaplasia nikimanisha uwezo wa cell ndani ya mwili kuweza kuchange kutoka aina moja ya cell kwenda nyingine ila nayo ni nadhariaa...

Ila all in all chanzo kikuu bado hakijajulikana ukiacha hizo nadharia ...

IMPACTS...

kama nilivosema hii hali sio cancer na mojawapo ya matokeo kiujumla ni mabaya ...

Ila inasababisha kuchelewa kwa mwanamke kutunga mimba japo endapo atafanikiwa kuwa mjamzito hakuna madhara kwa mtoto ila kwa miezi ya kwanza ya mimba hali inakuwa tete maumivu ni makali mno...

Kuna mengi ya kuongelea kuhusu hii hali ila leo kwa ufupi ni hayo...

Tuwapende mama zetu na wake wetu...


take your time ....
 
Amen
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…