Duh! mkuu wangu umeogopa kuwa mmoja wa wendawazimu au?
Ndio sawa na kusema hao Ma Psychiatrists, wengi wao ni wendawazimu wenyewe..Psychiatrists wanatuambia characteristic moja common ya wendawazimu ni kujiona wao wako sawa na ulimwengu mzima pembeni yao ulio tofauti nao umejaa wendawazimu, kwa hiyo ogopa sana mtu anayerusharusha hili neno "wendawazimu" kirahisi rahisi.
Ndio sawa na kusema hao Ma Psychiatrists, wengi wao ni wendawazimu wenyewe..
Tatizo lenu mnataka a simplistic approach, CCM mafisadi, kwa hiyo yeyote anayetaka kuitoa CCM rafiki yetu, yeyote anayekuwa critical kwa yeyote anayetaka kuitoa CCM ni adui yetu na rafiki wa CCM.
Hamuwezi kujiuliza kwamba hata katika vita hii ya kupigana na ufisadi kuna mafisadi wanachukua nafasi na kujifanya ni wapinzani, na kama mtakubali kila kitu bila kuuuliza mtajikuta mnamtoa fisadi mmoja na kumuweka fisadi mwingine.
Kuwa critical ni lazima, kama tunakuwa critical kwa CCM, kwa nini tusiwe critical kwa CHADEMA ?
Hayo hayo makapi yenu safari hii yanawamaliza... hakuna kulala mpaka kieleweke....kwanza kuitoa CCM halafu kuchuja makapi. Swali la kizushi: Kama ni makapi mbona mnayaogopa?
Huwezi kusema mtu ni kapi wakati umemfukuza kwa roho mbaya yako tu yaani hayuko kwenye system fulani ya ndani ya CCM, ilhali kura ya maoni inaonyesha anatakiwa. Ndio maana hayo makapi yanahama na wafuasi lukuki.
Safari hii mmekwisha kila mbinu imedhibitiwa sasa mnahaha! Welcome ''makapi''..Hameni wote waacheni wenye CCM yao.
Mkuu mwenzangu Wa Mjengoni;
Mgombea kama Thomas Nyimbo wa jimbo mojawapo la Njombe,au Hussein Bashe wa Nzega au hata Mzee Ramole wa Moshi-Mjini hawa wote waliongoza kwenye kura za maoni ndani ya CCM lkn kamati kuu ya CCM ikawaona hawana sifa kwa vigezo wanavyovijua wenyewe na kupuuza kabisa kura za wana CCM wa majimbo yao waliyowapa ridhaa ya kuwa wagombea wao;kam wagombea kama hao niliowataja juu wakija CHADEMA basi tuwape miaka 5 ya kuwachunguza?!
Kiranga na wenzako hamjaeleweka na sidhani kama mtaeleweka;tufafanulieni iweje aliyeongoza kura za maoni CCM akija CHADEMA tumchunguze wakati kuja kwake ni nafasi ya wazi ya CHADEMA kuongoza kiti bungeni?
Kuhama vyama ni hali ya kawaida, uchaguzi wa Marekani uliopita mgombea wa Democtrat Leberman aliama na kujiunga na Repablica na kugombea huko, hivyo si kitu cha kushangaza.
Kwa taarifa zako zaidi ya asilimia 90 ya viongozi wa vyama vya upinzani walitoka ccm. Kwa hiyo CHADEMA kuwapokea ni kuhimarisha democrasia nchini. Pia maeneo walipopewa nafasi ni yale maeneo ambako CHADEMA na vyama vingine hawakuwa na wagombea makini, hivyo watapeperusha bendera yao na kukuza chama kujulikana zaidi kwa wananchi, kama walivyofanya akina Dr. Slaa.
Ninashangaa sana jinsi ambavyo CHADEMA inapoteza umakini wake. Swala la members wa CCM kuhamia CHADEMA linachukuliwa kirahisi sana lakini halipaswi kuchukuliwa hivyo. Taarifa zisizo rasmi ni kuwa kuna mamluki lukuki wametumwa kuibomoa CHADEMA, wengine wameshawapokea na kuwakubali kuwa wagombea wa ubunge na udiwani. Time will tell. Washinde wasishinde lengo lao ni moja tu "kuhakikisha CHADEMA sio tishio tena kwa CCM kwa gharama yeyote".
Ni lazima CHADEMA wakubali kuwa ili kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima kuwaandaa wanachama wao muda mrefu ili kuongoza sio chama tu bali dola pia. Sio mtu anakurupushwa huko akiwa na ngeu, anahema na amekunjwa suruali, kisha anawatupia kadi ya CCM wakati hamkumpa nyie, na kumkabidhi kadi ya chama bila ya yeye kujua hata sera ya CHADEMA inasema je. Kisha kesho yake mnampa barua inayoonesha kuwa ndie mgombea wa CHADEMA. This is nonsense kwa chama makini na chenye nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
Sikatai kuhusu uzalendo wa baadhi ya waliohamia CHADEMA, na wala sitathubutu kuuhoji, ila ninahoji ukosefu wa subira. Mambo mazuri huivishwa kwa moto wa muda. Naogopa pale CHADEMA itakapogeuka ccmb, kama ambavyo TLP ya Mrema imegeuka.
Kwa ushauri wangu CHADEMA wawekeze zaidi kwenye wanachama vijana, wawape mafunzo ya Uzalendo, Uadilifu, Ubunifu na hali ya kuthubutu. Itachukua muda mrefu lakini itakuwa na matokeo ya kudumu na ya muda mrefu yenye kukijenga chama na Taifa kwa ujumla.
I love my country & i respect patriotism & intergrity.
Shoo gap,
Nimeupenda sana mtazamo wako - Makapi ya sisiemu yanapokuwa ngano kwa chadema.
Ni kweli kabisa kwa mswahili, mswahili ngano ni ile ilikwisha kuwa processed na unga wake mweupe ndio bora na chakula, pasipo kufahamu kwamba ni Makapi ya ngano ndio yenye high in fible na nutrition zaidi ya huo unga mweupe.
Pili, ikiwa hawa wanaopokelewa ni makapi ya ngano, ni ubora gani wa hiyo ngano ilobakia CCM umeutazama kama sii kwa ubora wa kutengeneza chakula ulokizoea?...yaani Chapati na Mandazi!. ina maana unazungumzia kitu kilichokuwa bora kulingana na ufinyu wa ubunifu wa chakula bora kiasi kwamba unayaona makapi hayawezi kupika Chapati wala mandazi.
Well Chadema wanakuiletea mapishi ya kitu kinaitwa - Cereals.. Ni ngano yote inatumika hakitupwi kitu.
Wadhungu wanasema A brand natural of whole grain wheat with high fiber.... Ushindi ni Lazima
...........Ukiangalia sana hapa utagundua kuna tofauti kati ya watu wanaoamini katika sera za vyama na wanaoamini katika personalities, watu wanaoamini katika sera za vyama kama mimi watataka kuhakikisha kwamba hawa wagombea kweli wanajikita katika sera za vyama, hili litaweza kuhakikishwa na muda tu.
Kwa wale wanaoangalia personalities bila kujali sera za vyama hivi, of course unaweza kutangaza kuhama CCM asubuhi na jioni ukatangazwa mgombea ubune wa CHADEMA.
Tatizo linakuja kama mtu anakuja katika chama bila kuwa na mapenzi ya sera, kesho akishaingia mjengoni anaweza kurudi kwao CCM kisiasa akawa ana vote nao CCM, na kuwapa ramani ya vita, kwa hiyo CHADEMA wanaweza kujiona wanajua kumbe wakawa wanaungua na jua.
tafsiri ya makapi ni pana sana. Ukipembua mchele yale mapumba yanayotupwa ambayo huwa ni kiasi kidogo na kubaki mchele mwingi hii ni tafsiri moja. Pia ukichukua udongo na kupembua dhahabu ambayo ni kidogo na kutupa udongo ambao ni mwingi hapa makapi ni huu udongo.
Hawa watu wanaohama ccm ni dhahabu, hawakutumia rushwa ndio maana hawakupata kuteuliwa ccm. Ukitaka ubunge kupitia ccm ni lazima uwe tajiri (yaani uwe na hela nyingi za takrima). Kama huna hutapata haijarishi wewe ni malechela au ntagazwa.