Huwezi kujua hili kwa hakika bila kuwapa muda wa kutosha kujionyesha true nature yao ndani ya upinzani. Inawezekana wamekuwa mzigo hata CCM ndiyo maana wakatoswa.
Ndiyo maana wengine tunapendekeza wapewe muda mpaka 2015 waangaliwe.
Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM- ndipo wapewe nafasi hizi.
Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.
Nimegundua na nina ushahidi wa wazi kabisa kuwa hoja nyingi za Kiranga ama zimejikita kwenye ushabiki wa CCM au hazina hata chembe ya maslahi kwa wana mageuzi!
Kama kuchunguzwa watu wanao hama vyama ungeanza na kuwaambia kwanza CCM maana wao ndiyo walioanza kuchukua watu toka kwenye vyama vya upinzani na wengine hadi ikawapa hadi mamlaka ya kuongoza dola!
Tukianzia toka kwa Mbunge wa zamani wa chadema Aman Kaburu,Mbunge wa zamani wa CUF Msabaha,Mwenyekiti wa sasa wa Mkoa wa Dar Mzee Guninita na wengineo wengi waliopewa madaraka ya kidola hawa walikuwa upinzani;Je CCM iliwachunguza lini kabla hawajapewa vyeo?
Kiranga,anza kuishauri kwanza CCM ambayo ina dola kuliko kuja sasa kuiona CHADEMA kama haifai wakifanya vitu hivyo hivyo usivyovikemea CCM ikifanya!
Sikubaliani nazo kabisaaaaaaaaaaa.... lakini ukitaka kuremba kama unavyosema wewe hutafika popote. Huo ustaarabu unaotaka Afrika bado haijaufikia. Inabidi na Chadema nao wacheze kata funua.... ni hali halisi....
Utawaangaliaje wakiwa nje acha waingie wapewe kazi zitakazoifanya Chadema ione ubora wao.
Umenena kiongozi.....hii ndiyo njia ya kututoa hapa kwenda kule!Sikubaliani nazo kabisaaaaaaaaaaa.... lakini ukitaka kuremba kama unavyosema wewe hutafika popote. Huo ustaarabu unaotaka Afrika bado haijaufikia. Inabidi na Chadema nao wacheze kata funua.... ni hali halisi....
Kwa hiyo, ukinipa hii cowboy mentality ya "if you can't say nice things about us you are with the enemy" unanionyesha tu jinsi ulivyo simpleton. Mbona sijaona wafuasi wa CCM kunishutumu kwamba mimi ni goon wa CHADEMA ninapowashambulia?
Au mnataka niamini kwamba CHADEMA ni watu wa kulialia na hawawezi ku stand criticism ?
Bado hujasema kuwa, kwa vile wapinzani hawako tayari (unadai kuwa labda watakua tayari mwaka 2015) kuongoza nchi mwaka huu (kwa hiyo wasipewe kura) nani apewe uraisi wa Tanzania mwaka huu?
Unaweza kunionyesha hapo niliposema wapinzani wasipewe kura ? Mimi naweza kukuonyesha wapi nimesema wapinzani wapewe kura, post moja kati ya nyingi nilivyosema hivi ni hii hapa , naomba wewe unionyeshe wapi niliposema wapinzani wasipewe kura.
Wewe unataka niseme mara ngapi na kwenye threads ngapi ndiyo uridhike?
Kiranga said:Mazee ningependa watu wengi zaidi wa vote CHADEMA, only because naamini tunahitaji mabadiliko.
Lakini at the same time siamini kwamba CHADEMA watashinda urais au kuwa na majority ya viti vya bunge. Nisingependa kuona CHADEMA wanashuka chini kutoka asilimia za kura za urais walizopata 2005 (11%) wala kupunguza viti vya bunge.
Lakini for sure CHADEMA nao bado hawako ready for prime time, ndiyo maana naona ni bora kuwe na gradual change, wapate tough love hapa, kama wana moyo wa kujifunza waweze kujifunza, labda 2015 au 2020 wataweza kuchukua nchi with confidence.
makapi maana nini kwani kuna watu ambao ni safi wana uzalendo ambao hawakuhonga wapiga kura bado wanahitajika kwa wananchi na taifa kwa ujumla hivyo haya si makapi mfano thomas nyimbo ameshinda na akaondolewa kwa mizengwe je hili ni kapi?
Umesema hapa (emphasis is mine):
Mazee ningependa watu wengi zaidi wa vote CHADEMA, only because naamini tunahitaji mabadiliko.
Lakini at the same time siamini kwamba CHADEMA watashinda urais au kuwa na majority ya viti vya bunge. Nisingependa kuona CHADEMA wanashuka chini kutoka asilimia za kura za urais walizopata 2005 (11%) wala kupunguza viti vya bunge.
Lakini for sure CHADEMA nao bado hawako ready for prime time, ndiyo maana naona ni bora kuwe na gradual change, wapate tough love hapa, kama wana moyo wa kujifunza waweze kujifunza, labda 2015 au 2020 wataweza kuchukua nchi with confidence.
Kama ungekuwa unasoma posts zangu bila bias, ungegundua kwamba mimi ninaongelea universal first principles, ninaongelea rules kwa vyama vyote vya kisiasa na nimesema hivyo several times, it just so happens kwamba CHADEMA ndicho chama mbadala ndiyo maana tunakizungumzia sana, na kuichambua system iliyo irredeemably corrupt -as some would say- kama ya CCM ni beating a dead horse.
Kwa hiyo, ukinipa hii cowboy mentality ya "if you can't say nice things about us you are with the enemy" unanionyesha tu jinsi ulivyo simpleton. Mbona sijaona wafuasi wa CCM kunishutumu kwamba mimi ni goon wa CHADEMA ninapowashambulia?
Au mnataka niamini kwamba CHADEMA ni watu wa kulialia na hawawezi ku stand criticism ?
Malafyale....usije kufa kwa pressure bure ku-argue na huyu ndugu. Sidhani kama hata yeye mwenyewe anakijua kwa dhati anachokipigania na kukisema.Hoja zako toka ile ya "Dada Regina na Ubunge wa Kilombero" na hii ya "Uchakachuaji wa Wagombea wa CHADEMA wanahohamia toka CCM" zote sio tu ni legelege mno bali pia ni "baseless and meaningless"kwa sababu haujaonyesha hata point moja hai ku-back up your claims
Kimsingi hoja zako nimezitupilia mbali!
Malafyale....usije kufa kwa pressure bure ku-argue na huyu ndugu. Sidhani kama hata yeye mwenyewe anakijua kwa dhati anachokipigania na kukisema.
Kiama cha Kikwete kimefika, Nani amesema Chadema hakitapata wabunge wengi?
Duh! mkuu wangu umeogopa kuwa mmoja wa wendawazimu au?Unaposema "wengi" unamaanisha nini? katika system nyingine za kuhesabu kuna moja, mbili na nyingi, kwa hiyo unaposema "wabunge wengi" unamaanisha wengi zaidi ya wawili au wengi majority (51 + %) ?