Shoo gap,
Nimeupenda sana mtazamo wako - Makapi ya sisiemu yanapokuwa ngano kwa chadema.
Ni kweli kabisa kwa mswahili, mswahili ngano ni ile ilikwisha kuwa processed na unga wake mweupe ndio bora na chakula, pasipo kufahamu kwamba ni Makapi ya ngano ndio yenye high in fible na nutrition zaidi ya huo unga mweupe.
Pili, ikiwa hawa wanaopokelewa ni makapi ya ngano, ni ubora gani wa hiyo ngano ilobakia CCM umeutazama kama sii kwa ubora wa kutengeneza chakula ulokizoea?...yaani Chapati na Mandazi!. ina maana unazungumzia kitu kilichokuwa bora kulingana na ufinyu wa ubunifu wa chakula bora kiasi kwamba unayaona makapi hayawezi kupika Chapati wala mandazi.
Well Chadema wanakuiletea mapishi ya kitu kinaitwa - Cereals.. Ni ngano yote inatumika hakitupwi kitu.
Wadhungu wanasema A brand natural of whole grain wheat with high fiber.... Ushindi ni Lazima
Mbona Mwera wa Tarime kaenda CUF na wamempa ugombea ubunge? Au ni kwa CCM tu kwenda Chadema? Any way by the way chadema hamna kitu hiyo ni nguvu tu ya soda.
Nasikitika sana kwa muda wa miaka mitano ijayo slaa hatakuwepo kwenye siasa kama ilivyokuwa kwa mbowe miaka mitano inayoisha. Inauma.
Bahati mbaya huwezi kupata dona kutoka ktk ngano! Ktk ngano hakitupwi kitu hata zile pumba za majani yake hupewa farasi wakala.Bob,
Kuna makapi ya kusema tunaweza kupata nutrition kama za dona, halafu kuna chuya za kupalia watu na kuwaua.
Ndiyo maana nikasema CHADEMA - na kwa kweli chama chochote kile- kinahitaji muda kupembua nafaka wapi, makapi yanayoweza kufaa kwa kutoa virutubisho wapi, na chuya zinazoweza kuwapalia watu wapi.
Kazi ya kuchambua haitaki papara na kuharakisha, ama sivyo CHADEMA "wataula wa chuya".
Nimekuwa nikisema more or less the same thing hapa, wanaotoka CCM sasa hivi waangaliwe mpaka at least 2015, kama wameonekana kwamba wamefuata kazi ya chama -na sio kutafuta ubunge kwa sababu wameshindwa kura za maoni CCM- ndipo wapewe nafasi hizi.
Vinginevyo CHADEMA itakuwa inaalika chaos.
hivi huwa wanachukua makapi kwa sababu chama hakina uwezo wa kuzalisha ngano yake wenyewe?
sijaona bado mantiki ya kuchukua makapi kisha ukayapa thamani ya zaidi ya ngano yenyewe hata kama yanafaida.
Tafsiri ya makapi ni pana sana. Ukipembua mchele yale mapumba yanayotupwa ambayo huwa ni kiasi kidogo na kubaki mchele mwingi hii ni tafsiri moja. Pia ukichukua udongo na kupembua dhahabu ambayo ni kidogo na kutupa udongo ambao ni mwingi hapa makapi ni huu udongo.
Hawa watu wanaohama CCM ni dhahabu, hawakutumia rushwa ndio maana hawakupata kuteuliwa CCM. Ukitaka ubunge kupitia CCM ni lazima uwe tajiri (yaani uwe na hela nyingi za takrima). kama huna hutapata haijarishi wewe ni Malechela au Ntagazwa.
Mkuu wangu kiswahili safi makapi ni mabaki ambayo kwao wote hayana faida lakini inategemea na mtu unayataka makapi hayo ili kutengeneza kitu gani..hapa tunazungumzia CCM na ngano yao na hakika aMakapi ya ngano ndiyo yenye fible zaidi ya hjuo unga mweupe (kina Rostam).. makapi ya ngano are brown na hakika yana nutrition kwetu ktk mapishi mapya kuliko hizo chapati na mandazi za CCM.Huwezi kuiona kwa vile wewe ni mtetezi wa chama cha makapi oooppss mafisadi