Makanisa ya kiroho mnatupeleka wapi?

hebu toka huko uwe huru kufikiri tofauti na ulivyokuzwa na kukomaa na mafundisho ya kimapokeo na kihafidhina
Naona umekabwa na kiazi kikavu...

Shusha na haya maziwa..
2 Wathesalonike 2:15
Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
 
Ukitoka hapo unasema kanisa katoliki wezi wakati ukiumwa unaenda kutibiwa kwenye hospital zao
Hizo hosp ni kitega uchumi cha kanisa na mbaya zaidi siku hizi wanachukua ruzuku ndefu serikalini
 
Wakiwa watu wazima watabatizwa maana ufahamu wao
Unaweza niambia watu 3000 waliobatizwa na Petro siku ya Pentekoste kwwmba walikuwa ni watu wazima pekeee(Thibitisha)....

Je! Unazungumziaje kisa kisa cha Paulo na Sila kuwabatiza familia nzima ya Mlinzi wa Gereza....Je Wataka kuniambia hiyo famila kulikwa hakuna watoto...

Pita hapa..

Matendo ya Mitume 16:33-34
Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.
Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.

Msome hapa St. Paul akiwaandikia Epistle Wakristo walioisho Korinto(Uturuki ya Sasa)

1 Wakorintho 1:16
Tena naliwabatiza watu wa nyumbani mwa Stefana; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine.




Nipo...
 
Hizo hosp ni kitega uchumi cha kanisa na mbaya zaidi siku hizi wanachukua ruzuku ndefu serikalini
Waislamu bana......hii tabia yenu bado hamjaacha...

Kanisa lipokee ruzuku ili iweje...??? Kasome MOU uje hapa tena
 
Ukitoka hapo unasema kanisa katoliki wezi wakati ukiumwa unaenda kutibiwa kwenye hospital zao
Sio mbaya, utachangia kujenga shule ila watasomesha wenye uwezo......
Utachangia ujenzi ila utatibiwa kwa gharama zako.
 
kiongozi anzisha uzi unaohusu ubatizo mimi nitasimama kwa upande wa maji machache kama msemavyo na nitakupa maandika mwisho tupate kuelimisha. Usisahau kunitag
 
Naona umekabwa na kiazi kikavu...

Shusha na haya maziwa..
2 Wathesalonike 2:15
Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
Mapokeo Yanayozungumzwa Hapo Ni Neno La Mungu Lisilogoshiwa. Siyo Mapokeo Ya Kihafidhina Ya Kidini.
 
Bado hamjifunzi hata muambiwe vueni na gagulo zenu mtawapa, kutwa mnaibiwa na mnawapa ila pembeni hamuachi kulalamika.

Na mtaibiwa milele na mtakufa mkipiga kelele za kuibiwa. Hamuwajui Deci nyinyi inavyoonekana
 
Nipe maana ya ubatizo
Ubatizo Maana Yake Ni Kuzika Matendo Ya Kale(dhambi)na Kufufuliwa. Ni Ondoleo La Dhambi. Hapa Kuzika Haiwi Ardhini Bali Ni Kuzamisha Kwenye Maji Mengi. Ni Ishara Ya Kuzika Utu Wa Kale Na Kuibuka Na Utu Mpya. Njia Hii Inapaswa Kila Mfuasi Wa Kristo Aitimize.Rejea Marko Mtakatifu 16:116, Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini atahukumiwa. MATENDO YA MITUME 2:38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Na ubatizo katika Roho Mtakatifu Unamaanisha Mtu Kuokolewa Kwa Neema na kuzaliwa upya, mambo mapya(tabia) kwa kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu. MATHAYO MT. 28:19. Basi, enendeni,mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. HOJA IENDELEE KUJIBIWA KWA HOJA MARIDHAWA.
 
KWANI TUNATIBIWA BURE? KWANI SHULE ZAO TUNASOMA BURE? KWA TAARIFA YAKO VITEGA UCHUMI VYAO TUNAJENGA SISI THEN TUNALIPISHWA SISI TENA KWA BEI KUBWA ZAIDI BILA KUJALI MICHANGO YETU. TUMIA KICHWA CHAKO VZURI KUFIKIRI
Ukitaka kushuhudia hiyo nenda KKKT Kimara
 
Blind faith,yaani utoe tu,wala usijishughurishe na kujua hizo fedha zinatumikaje,kwa vile zinapokewa na "mpakwa mafuta wa Bwana" wewe usijari hata akizifanyia ufisadi,wewe mtoaji utakiwi kuhoji,Mungu atamuadhibu,
Kama imani yako ndio hii,pole sana,
 
Blind faith,yaani utoe tu,wala usijishughurishe na hiyo fedha inavyotumika,
Huyo anayepokea "mpakwa mafuta" wa bwana,hata akizifisadi,wewe usihoji,Bwana Mungu atamuadhibu kwa wakati wake,
Sadaka isaidie yatima,wajane(wasio na uwezo wa kifedha),sio itumike kununua magari ya kifahari na kujenga nyumba ya mchungaji,wakati waumin ni hohehae hawajiwezi hata kwa mlo mmoja,
Kanisa,lijiusishe na kuwanyanyua wananchi,waumini wake kiuchumi,
 
Mathayo 6
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.

2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.

3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;

4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi

 
Mapokeo Yanayozungumzwa Hapo Ni Neno La Mungu Lisilogoshiwa. Siyo Mapokeo Ya Kihafidhina Ya Kidini.
Hahaha....nakurudia....


Mapokeo ni nini...???


Tafadhali ili tuende pamoja naomba unijibu maswali ninayokuuliza...



Nipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…