dosama
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 912
- 957
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk. Mohamad Reza Rahimi, atawasili jijini Dar es Salaam kesho tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi hapa nchini, ambapo atalakiwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Gharib Bilal.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Irani nchini, Mohsen Movahedi, alisema wakati wa ziara yake, Dk. Rahimi ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali mbili za kisasa huko Kigamboni na Mkoa wa Magharibi Unguja.
Jumatano ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali ya Kigamboni itakayogharimu sh. bilioni 1.5 na Alhamisi atakuwa Zanzibar kwa jukumu kama hilo katika ujenzi wa hospitali itakayogharimu sh. bilioni mbili, alifafanua Balozi Movahedi na kuongeza kuwa, keshokutwa pia atazindua zahanati mpya ya Msasani ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Iran.
Akitoa ratiba ya ziara hiyo, Balozi Movahedi alisema mapema Jumatano, Dk. Rahimi ataonana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam, kabla kuzumgumza na mwenyeji wake, Dk. Bilal na kisha kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Lengo kubwa la ziara ya Dk. Rahimi hapa Tanzania ni kukuza mahusiano ya kidiplomasia na kihistoria kati ya Tanzaania na Iran. Ni katika msingi huo Iran imetoa msaada wa ujenzi wa hospitali hizo mbili, pia itaweka vifaa na kuanza kuendesha chuo cha mafunzo stadi cha Zanzibar, alisema balozi huyo wa Iran nchini.
Kwa upande wa Zanzibar, Dk. Rahimi atakutana na kufanya mazungumzo ya kina na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharrif Hamadi na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Iddi Seif.
.
Interejensia ya Jf naomba msaada kuna nini nyuma ya pazia?