Makamu wa Rais kwa mujibu wa Katiba

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

47(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muunga no;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini
au yuko nje ya nchi.

(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya
37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja.

Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Makamu wa Rais atakuwa amechaguliwa.

(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

Baada ya kupatikana Makamu wa Rais, vipi Makamu huyu ataiwakilisha Zanzibar katika mambo ya muungano na yake ya sio kuwa ya muungano kuyatafutia uvumbuzi?

Makamu huyu ili apate ile dhana ya kwamba anaiwakilisha Zanzibar katika muungano, basi ilitakiwa office yake iwepo Zanzibar, na asimamie yale mambo ya muungano kwa upande wa Zanzibar na kutatua kero zote za muungano.

Lakini leo hii ile dhana ya kuwa tuna muungano wa usawa haipo, Zanzibar haina uwakilishi kwa nafasi ya Makamu kwa ufasihi, Makamu wetu amekuwa akipangiwa kazi Tanganyika, kusimamia miradi Tanganyika iliyokuwa ya muungano na isiyokuwa ya muungano.

Ndani ya mfumo huu tulionao bado Zanzibar haipati uwakilishi kama tunaohitaji Wazanzibar.
 
Zanzibar imekuwa mzigo kwa Tanganyika inalelewa inalishwa na Tanganyika kila kitu ni Tanganyika
 
Back
Top Bottom