Makamu wa Rais azindua Mbio za Mwenge

Makamu wa Rais azindua Mbio za Mwenge

Hainiingii akilini kufuta sherehe za uhuru na Muungano ukabakiza mwenge wa uhuru wa kuzinsua shimo la choo na miradi isiyona tija!
 
kinachoboa unatembezwa na CCM kupitia mifuko yetu.
 
Na laana ya mwenge itaendelea kututafuna,,,hii imekuwa kama nguvu flan za giza,,,tusimlaumu sana MAGU anaweza kuwa amefungwa ufaham juu ya hili,,,maombi yanaitajika aisee
 
Yani huu mwenge nikiutazama halafu nkarudi na kumuangalia Raisi wangu Basi nahsi mheshimiwa ana Tamko ju yake
 
Mimi najua utamu wake,
1) wakimbiza mwenge wanachinjiwa ng'ombe na mbuzi bure
2) Fedha za halmashauri (magari na wafanyakazi vinatumika including kutumia fedha zisizohusika)
3) Kila unapolala mwenge lazima kuwe na mkesha - music, pombe na wanawake - UKIMWI njenje
4) Allowance tamu kwa wote.....
5) Ongeza zako.....
6. Ni ishara ya matumaini, upendo na umoja wa taifa letu
 
Samia.jpg

Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano.

By Matern Kayera, Mwananchi Digital

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo.

Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alimnukuu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere akisema kuwa nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau.

Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano. Alisema utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa.

“Kaulimbiu ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa, washirikishwe na wawezeshwe,”alisema Makamu wa Rais na kuongeza kuwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hawajatumika ipasavyo kutokana na sababu mbalimbali.

Alizitaja baadhi ya sababu au changamoto zinazowakabili vijana nchini kuwa ni ukosefu wa ajira, uwezo mdogo wa kuajiri kwenye soko la ajira, ukosefu wa mitaji rafiki kwa vijana, maeneo ya kufanyia kazi pamoja na mitazamo hasi kwa baadhi ya vijana kwa kuchagua kazi.

Makamu wa Rais pia amewataadharisha vijana kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya. Amesema vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 ndiyo wanaongoza kwa kuathiriwa na maambukizi ya ukimwi. Amesema athari za ukimwi na madawa ya kulevya kwa vijana ni kubwa lakini pia zinaongeza mzigo kwa jamii na serikali katika kuwatibu, kuwahudumia na kuongezeka kwa vifo.

Kwa upande wake, Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, amemtambulisha George Jackson Kijimba kuwa ndiye kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akisaidiana na wakimbiza mwenge wengine watano. Alisema sherehe za kuhitimisha mbio hizo za mwenge wa uhuru zitafanyika mkoani Simiyu tarehe 14 Oktoba mwaka huu.
 
Ni kuwaonea watu na viongozi wa dini wanakaa kimya, siwataki hawa watu . Wao ndio wa kuwasemea watu sio wananyamaza kwa vile yao yanawanyookea
 
Hii miradi inayozinduliwa kila mwaka ingekuwa na mafanikio au manufaa huenda leo Tanzania ingelikuwa ni moja ya nchi tajiri sana na wananchi wake wanaishi maisha mazuri sana.

Lakini gharama za mafuta ya magari, mafuta ya mwenge wenyewe, posho za wakimbiza mwenge; hii ni pesa nyingi sana endapo kama serikali wangetafakari na kuufuta kabisa huu ukimbizaji wa mwenge wa uhuru, hii pesa ingetumika katika shughuli za maendeleo na pia utengenezaji wa madawati katika shule zetu.

Wanafuzi wasingekaa chini kwa asilimia fulani:-

Primary School TZ.jpg

Shule 1.jpg

Serikali wangetafakari gharama za ukimbizaji wa huu mwenge na wangeamua kubana matumizi haya yasiyo na lazima, HOSPITALI ZETU ZINGEKUWA NA HUDUMA BORA ZAIDI KULIKO SASA. WAGONJWA WASINGELALA MZUNGFU WA NNE:

Wajawazito_Temeke_Hospital.jpg

WAGONJWA_ZAHANATI_KISAKI[1]_.JPG

Endapo kama serikali wangetafakari gharama na kubana matumizi katika ukimbizaji wa huu mwenge,
TUNGEBORESHA BARABARA NA PIA KUEPUKA MAFURIKO:-
Mafuriko DSM 1.jpg

Endapo kama serikali wangefafakari gharama za ukimbizaji mwenge na kubana haya matumizi yote;
MAISHA YA WATANZANIA VIJIJINI NA PIA MIJINI YANGEBORESHWA:-
MAISHA BORA.jpg

Endapo kama serikali wangetafakari na kubana matumizi haya yasiyo na lazima:

HUDUMA ZA JAMII IKIWEMO MAJI MAFI NA SALAMA ZINGEPATIKANA KWA WANANCHI WOTE MIJINI NA VIJIJINI. UWEZO HUO TUNAO:-

Maji ni uhai.jpg

Maji Kisima.jpeg

SERIKALI ITAFAKARI, ICHUE HATUA........................
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!​
 
Kwa kweli kwa suala la mwenge ni bora ukakae makumbusho, yaan naona ni bora tungesherehekea siku za uhuru kwa magwaride kuliko mbio za mwenge, alaf pesa ya mbio hzo ikaenda kufanya mambo mengne kabisa
 
Hii miradi inayozinduliwa kila mwaka ingekuwa na mafanikio au manufaa huenda leo Tanzania ingelikuwa ni moja ya nchi tajiri sana na wananchi wake wanaishi maisha mazuri sana.

Lakini gharama za mafuta ya magari, mafuta ya mwenge wenyewe, posho za wakimbiza mwenge; hii ni pesa nyingi sana endapo kama serikali wangetafakari na kuufuta kabisa huu ukimbizaji wa mwenge wa uhuru, hii pesa ingetumika katika shughuli za maendeleo na pia utengenezaji wa madawati katika shule zetu.

Wanafuzi wasingekaa chini kwa asilimia fulani:-

View attachment 340048

View attachment 340050

Serikali wangetafakari gharama za ukimbizaji wa huu mwenge na wangeamua kubana matumizi haya yasiyo na lazima, HOSPITALI ZETU ZINGEKUWA NA HUDUMA BORA ZAIDI KULIKO SASA. WAGONJWA WASINGELALA MZUNGFU WA NNE:

View attachment 340051

View attachment 340052

Endapo kama serikali wangetafakari gharama na kubana matumizi katika ukimbizaji wa huu mwenge,
TUNGEBORESHA BARABARA NA PIA KUEPUKA MAFURIKO:-
View attachment 340053

Endapo kama serikali wangefafakari gharama za ukimbizaji mwenge na kubana haya matumizi yote;
MAISHA YA WATANZANIA VIJIJINI NA PIA MIJINI YANGEBORESHWA:-
View attachment 340055

Endapo kama serikali wangetafakari na kubana matumizi haya yasiyo na lazima:

HUDUMA ZA JAMII IKIWEMO MAJI MAFI NA SALAMA ZINGEPATIKANA KWA WANANCHI WOTE MIJINI NA VIJIJINI. UWEZO HUO TUNAO:-

View attachment 340056

View attachment 340057

SERIKALI ITAFAKARI, ICHUE HATUA........................
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!​
Maisha bora kwa kila mtanzania
 
Samahani hivi Kenya kuna mwenge? Kama hakuna kwanini wametupita maendeleo
 
Mwenge unaleta ajira kwa vijana......bwabwabwabwabwaaaaaa!!.....
 
Back
Top Bottom