Makamu wa Rais ana kazi gani?

Makamu wa Rais ana kazi gani?

I salute you guys!
Ningependa kujua,hivi kazi halisi ya makamu wa raisi katika jamuhuri yetu ya tz ni ipi?
Ni kweli kwamba raisi akiwa nje ya nchi au out of office yeye ndo anakaimu kiti?
>Je makamu wa raisi naye anakaa ikulu/anaofisi pale ikulu?
Baada ya kufuatilia sana nimeona akiwa anakata utepe tu katika miradi mbalimbali.

Na kusubiri kama kifo kitatokea aweze kuwa na 1
 
Makamu wa rais ni mtawala kutoka zanzibar alieteuliwa na wazanzibar kwa ajili ya kuja kuwatawala watanganyika.kazi yake ni kuwatawala watanganyika.
 
Mwacheni mzee wa mkasi.. nasikia yy kila aendako lazma awe na mkasi kwenye koti lake la suti.

Mkuu kuna shangingi moja limetengwa kwa kubeba mkasi tu. Mashangingi matatu yanabeba walinzi alioachichiwa na Sheikh Yahaya
 
makamu wa raisi kazi yake kuzunguka mikoani kukagua hali ya siasa na CCM kwa ujumla na raisi kazi kuzunguka nje ya nchi kuomba misaada
 
Inachekesha ila ndo ukweli wenyewe, pia huyu jamaa hana mvuto wa kisiasa
Hapo mkuu umekosea,
Mzee wa utepe huwa anatumia mikasi mikubwa kama ya mafundi cherehani. sio vidogo kama hivi hebu kuwa na heshima kidogo kijana
 
Makamu wa rais alikuwa marehemu Dkt Omar tu
Huyu jamaa alikuwa anaogopewa kila kona na alikuwa mchapa kazi.
Siou huyu babu miwani yeye ni kukata utepe na nasikia siku hizi kapata dili mpya ya kufuturisha.
 
Asalaam,
Katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya uliomalizika kwa awamu ya kwanza, nimebahatika kuhudhuria mikutano miwili katika wilaya ya Bagamoyo na mmoja katika wilaya ya Bukoba. Nilitoa maoni yangu katika mikutano miwili kati ya hiyo mitatu.
Kitu nilichotilia mkazo ni hiki cheo cha "MAKAMU WA RAIS". Kwa kweli binafsi sioni sababu za msingi za kuwa na Rais, makamu wake, na waziri mkuu kwa wakati mmoja. Nimegundua ni uharibifu wa mapato kuwa na taasisi nyingine yenye wizara mbili, huku mkuu wa taasisi hiyo akiishia kusoma magazeti, kualikwa kwenye warsha, na kukata utepe. Pia Makamu wa Rais wa sasa ameishia kuvikwa mataji ya maua na kutoa hutuba kama mhitimu wa shule.
Ndugu zangu watanzania, nawaomba mkipata nafasi katika awamu inayofuata ya utoaji maoni, mlizungumzie jambo hili, kwakua, Rais ni Mkuu wa nchi na Mkuu wa serikari na pia ni Amri Jeshi Mkuu., Waziri Mkuu ni mtendaji mkuu wa shughuli za serikali na msimamizi wa serikali bungeni. JE?
Makamu wa rais anaumuhimu gani?
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
 
Makamu wa Rais ana majukumu ya kusimamia Mazingira pia suala ambalo ni mhimu na nyeti sana.angelikua mtu active yeye angekua na nguvu kubwa sana hasa katika masuala ya mipango miji na usafi wake bahati mbaya sana..ndio hivo nae ni the same ccm...
 
Rais,na waziri Mkuu wanatosha.Either uwe na makamu wa Rais usiwe na waziri mkuu au Uwe na waziri mkuu usiwe na makamo wa Rais.Tunakua na watumishi wengi sana ili hali tuu maskini
 
Asalaam,
Katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya uliomalizika kwa awamu ya kwanza, nimebahatika kuhudhuria mikutano miwili katika wilaya ya Bagamoyo na mmoja katika wilaya ya Bukoba. Nilitoa maoni yangu katika mikutano miwili kati ya hiyo mitatu.
Kitu nilichotilia mkazo ni hiki cheo cha "MAKAMU WA RAIS". Kwa kweli binafsi sioni sababu za msingi za kuwa na Rais, makamu wake, na waziri mkuu kwa wakati mmoja. Nimegundua ni uharibifu wa mapato kuwa na taasisi nyingine yenye wizara mbili, huku mkuu wa taasisi hiyo akiishia kusoma magazeti, kualikwa kwenye warsha, na kukata utepe. Pia Makamu wa Rais wa sasa ameishia kuvikwa mataji ya maua na kutoa hutuba kama mhitimu wa shule.
Ndugu zangu watanzania, nawaomba mkipata nafasi katika awamu inayofuata ya utoaji maoni, mlizungumzie jambo hili, kwakua, Rais ni Mkuu wa nchi na Mkuu wa serikari na pia ni Amri Jeshi Mkuu., Waziri Mkuu ni mtendaji mkuu wa shughuli za serikali na msimamizi wa serikali bungeni. JE?
Makamu wa rais anaumuhimu gani?
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
Mkuu JJB nashukuru kuwa umewasilisha maoni niliyokuwa nayo. Pamoja na hilo, naisubiri hii tume nami niongezee lile la rais kuingilia mhimili wa mahakama.

Kuna watu wengi ambao wamehukumiwa kunyongwa baada ya mahakama kuwakuta na hatia ya kuua kwa kukusudia. Adhabu kwa watu hawa zimeshindwa kutekelezwa kwa kuwa rais hajakubali (Kusaini) utekelezwaji wa hukumu hizi. Huu ni mzigo kwa taifa kwani watu hawa wanakula tu na kulala pasipo kufanya kazi yoyote wakisubiri adhabu yao ya kunyongwa ambayo haitekelezwi.

Katiba iweke bayana kuwa mahakama ikitoa hukumu kusiwe na chombo kingine nje ya mahakama kuingilia hukumu iliyotolewa, na pasipo rufaa iliyokatwa adhabu itekelezwe mara moja.
 
Sasa kikifutwa kazi ya kutembea na mikasi ya kukata utepe atafanya nani?
 
Ungejenga hoja yako kivingine lakini sio " ... hana umuhimu ...". Utaona umuhimu wake pale Rais "atakaposhindwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na ugonjwa au mapenzi ya Mwenyezi Mungu"; yaani, hapo nchi itakapokosa kamanda mkuu - tutageuka Somalia mara moja.

Hoja yangu hapa sio Makamu wa Rais, bali tupe mbadala mwingine wa nani achukue majukumu ya Rais endapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Tunayo mifano ya hivi karibuni kabisa kule Malawi na Ghana tumeona Makamu wa Rais wakichukua madaraka baada ya marais wao kufariki.

Makamu wa Rais ni muhimu kwa kua Rais anaposhindwa kuongoza kwa sababu zilizoainishwa katika katiba,makamu huchukua madaraka katika kipindi cha mpito.Na hii ipo nchi nyingi tu.Hata marekani yupo Joe Biden,alikua Dick Chenney na wote ni wazee wa mikasi.Ni vema makamu wa Rais akawa sio mtu mwenye uchu wa madaraka ili kupunguza msuguano kama ilivyokua kwa Obasanjo na Atiku Abubakar mpaka walikaribia kukunjana mashati
 
Mkuu JJB nashukuru kuwa umewasilisha maoni niliyokuwa nayo. Pamoja na hilo, naisubiri hii tume nami niongezee lile la rais kuingilia mhimili wa mahakama.

Kuna watu wengi ambao wamehukumiwa kunyongwa baada ya mahakama kuwakuta na hatia ya kuua kwa kukusudia. Adhabu kwa watu hawa zimeshindwa kutekelezwa kwa kuwa rais hajakubali (Kusaini) utekelezwaji wa hukumu hizi. Huu ni mzigo kwa taifa kwani watu hawa wanakula tu na kulala pasipo kufanya kazi yoyote wakisubiri adhabu yao ya kunyongwa ambayo haitekelezwi.

Katiba iweke bayana kuwa mahakama ikitoa hukumu kusiwe na chombo kingine nje ya mahakama kuingilia hukumu iliyotolewa, na pasipo rufaa iliyokatwa adhabu itekelezwe mara moja.

Ktk maoni yangu niliyotuma kwa tume kupitia barua pepe nimeweka suggestion hiyo kwa red
 
Asalaam,
Katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya uliomalizika kwa awamu ya kwanza, nimebahatika kuhudhuria mikutano miwili katika wilaya ya Bagamoyo na mmoja katika wilaya ya Bukoba. Nilitoa maoni yangu katika mikutano miwili kati ya hiyo mitatu.
Kitu nilichotilia mkazo ni hiki cheo cha "MAKAMU WA RAIS". Kwa kweli binafsi sioni sababu za msingi za kuwa na Rais, makamu wake, na waziri mkuu kwa wakati mmoja. Nimegundua ni uharibifu wa mapato kuwa na taasisi nyingine yenye wizara mbili, huku mkuu wa taasisi hiyo akiishia kusoma magazeti, kualikwa kwenye warsha, na kukata utepe. Pia Makamu wa Rais wa sasa ameishia kuvikwa mataji ya maua na kutoa hutuba kama mhitimu wa shule.
Ndugu zangu watanzania, nawaomba mkipata nafasi katika awamu inayofuata ya utoaji maoni, mlizungumzie jambo hili, kwakua, Rais ni Mkuu wa nchi na Mkuu wa serikari na pia ni Amri Jeshi Mkuu., Waziri Mkuu ni mtendaji mkuu wa shughuli za serikali na msimamizi wa serikali bungeni. JE?
Makamu wa rais anaumuhimu gani?
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.

Mkuu uko sahihi kabisa, na mimi ndo mtizamo wangu, tatizo wanasiasa wanakomalia hizi nafasi ziwepo ili wapate ulaji tu lakini kiukweli ni mzigo kwa kodi zetu
 
Wakuu
Kuna kitu kinaitwa Muungano.
Hapa mjadala unakwenda kama vile Tanzania ni nchi moja. Tanzania ni Muungano wa nchi mbili. serikali ya Muungano inasimamia mambo ya muungano na pia inasimamia mambo ya Tanganyika.

Tuendelee na mjadala tukiwa na wazo hili kichwani.

Ingelikuwa tunazungumzia serikali ya Tanganyika tu basi makamo wa Rais ni cheo cha kutupa jalalani tu.

Lakini mkuu Dudus post #6 pia ametoa nukta muhimu ya kuizingatia.
 
Mkuu uko sahihi kabisa, na mimi ndo mtizamo wangu, tatizo wanasiasa wanakomalia hizi nafasi ziwepo ili wapate ulaji tu lakini kiukweli ni mzigo kwa kodi zetu

mkuu, bajeti ya mzee wa mikasi mfukoni ni takriban sh bilion tisa. bajeti kwa ajili ya mikasi na tepe. tehe.
 
Back
Top Bottom